UVUMI
Hivi karibuni baada ya Elon Musk kuununua mtandao wa Twitter kuliibuka uvumi kwamba bilionea huyo amepanga kurejesha akaunti zote za Twitter zilizofungiwa, kasoro ile ya aliyekuwa Rais wa Marekani kuanzia mwaka 2017 hadi 2021, Donald Trump.
Kichwa cha habari cha taarifa hiyo kinasomeka kwa Kiingereza: “Elon Musk States Intention to Restore Every Banned Twitter Account, ‘Except For Donald Trump’, huku ikifuatiwa na maandishi yasomekayo kwa Kiingereza: "It may seem petty but I just don’t like him"- ikimaanisha kuwa ni jambo linaweza kuoneka dogo, ila yeye (Elon Musk) hampendi tu Donald Trump.
Picha (screenshot) hiyo inayodaiwa kutoka ukurasa wa gazeti maarufu la Marekani, New York Times, imekuwa ikizunguka kwenye mitandao ya...