Kuna Taarifa zilizosambaa kwenye Mitandao ya Kijamii, zinazodai Tarehe 31 Januari 2023 wakati Tundu Lissu akifanya Mahojiano ya channel ya YouTube ya Jambo TV, kwamba alimpongeza Rais Samia kwa kuunda Tume mpya ya Kuchunguza Haki Jinai. Taarifa hizo ni Uzushi.
Uzushi huo ulidai kuwa Tundu Antipas Lissu alisifia kuundwa kwa Tume ya Haki Jinai, hata hivyo, kwa mujibu wa video iliyorekodiwa wakati wa mahojiano hayo Lissu hakupongeza kuundwa kwa tume ya haki jinai wala hakuzungumzia kundwa kwa tume ya haki jinai bali alizungumzia mfumo wa haki jinai kwa kukosoa mfumo huo.
Tarehe 31 Januari 2023 Rais Samia alizindua Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuimarisha Taasisi za Haki Jinai. Rais Samia alisema Tume hiyo imeundwa kutokana na kuvurugika...