JamiiCheck - Tanzania

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

JF Prefixes:

Baada ya jana Klabu ya Simba kutoa taarifa kuwa mlinda mlango wao, Aishi Manula alishindwa kusafiri kuelekea Algeria baada ya kupata hitilafu ya kiafya dakika chache kabla ya kuondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Haya ndio majibu ya Tanzania One "Siumwi chochote, ila wao ndio wanajua nini kinaendelea. Siwezi kuzungumza chochote, naacha wasimamizi wangu wazungumze." — Aishi Manula
Wanawake wajawazito hupewa tahadhari au hata hukatazwa kabisa kufanya baadhi ya mambo kwa lengo la kuwaepushia madhara yanayoweza kuhatarisha afya zao, pamoja na mtoto aliyeko tumboni. Miongoni mwa mambo yaliyodumu kwa muda mrefu kwenye jamii zetu ni kuzuia wanawake wajawazito kutumia mayai ili kuwalinda watoto wasizaliwe wakiwa na vichwa vikubwa, au wakiwa hawana nywele. Kisayansi, jambo hili lina ukweli kiasi gani?
Nimekutana na taarifa zinadai kuwa Baltasar Ebang Engonga ameachiwa huru na kurudi mtaani baada ya kukutwa hana hatia kwani Wanawake wale aliokuwa akifanya nao ngono kwenye zile video zaidi ya 400 ni watu wazima na walionekana kuwa wameridhia kufanya na kurekodiwa. Aidha vipimo vilionesha hana ugonjwa wowote wa zinaa na hivyo kuwa huru kwani hajasababisha madhara yoyote kwa jamii. Je, ni kweli au watu wanatupiga huku mtaani wakuu?
Wakuu nimekutana na barua mtandaoni inasambaa inaonekana kuwa ya LHRC ina kichwa cha habari, uimarishwaji wa demokrasia uchaguzi wa serikali za mitaa 2024, barua hiyo inaeleza kuwa Tanzania imeonesha hatua kubwa katika kuimarisha demokrasia kutokana na uchaguzi wa serikali za mitaa. wakuu hapa uhalisia ni upi imetolewa na LHRC kweli?
JamiiCheck imefuatilia hotuba iliyotolewa na Stephen Wasira akiwa kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa mkoani Mwanza tarehe 26-11-2024 ambapo mbali na mambo mengine alisema kuwa Serikali katika awamu hii sita ilinunua magari ya wagonjwa 528, lakini pia CHADEMA ilijipanga kusimamisha wagombea kwa 85% mijini na 60% vijijini.
Back
Top Bottom