Mto Songwe
JF-Expert Member
- Jul 17, 2023
- 6,683
- 14,060
Taifa Stars ndio inawachezaji wenye umri mdogo zaidi (Average)Uchambuzi wangu kwa Taifa stars
1. Samata soka limeanza kushuka nafikiri umri nao unachangia
2. Himid mao, huyu jamaa Pasi anapoteza tu na wala hajali, anakaba hovyo na kusababisha faulo za ovyo katka maeneo yasiyo na hatari yoyote mpka anapata kadi.....
Ni mzito sana soka la sasaivi linahitaji vijana wenye mbio, kwa staili yake ya uchezaji hata Timu ya wanawake ya Hispania hapati namba.
3. Manula nafikiri kukaa nje muda mrefu imeshusha sana kiwango chake ingekuwa busara ajinoe kwanza vizuri lasivyo Mzimu wa Goli tano siku moja utamludia tena.
4. Mwamnyeto, huyu beki ni vile tu Taifa stars hatuna kikosi kipana ila hapaswi hata kuwa mchezaji wa reserve maan ni mzito mno na hana maamuzi ya haraka hajui kujiposition timu ikiwa haina mpira....
Huwa Akikutana na straika wasumbufu anakuwa kama mtu aliyeweuka asiyejua afanye nini mwshoni huishia kupitwa au kukata hovyo.
5. Mohamed hussein (Tshabalala), kwa huyu sina maelezo mengi ila Huyu mtu hapaswi kuwa Mchezaji mpira.
6. Bacca, huyu ni beki mzuri sana ila huwa anakosa sapoti hivyo inamlazimu kuingilia namba za wenzake ili kuclear makosa yao(Tshabalala na mwamnyeto) hivyo kupelekea nafasi yake muda mwingine kubaki wazi na kupelekea Goli.
7. Haji mnoga, huyu jamaa ni full back Tapeli namuita Full back tapeli maana hata Kupunguza mtu mmoja tu kasheshe anaishia kujigonga gonga na kutoa pasi za nyuma.
8. MSUVA, huyu saizi yeye ndo alitakiwa awe kocha wa Taifa stars, kama kuna ndugu yake humu amshauri tu.
9.Kocha, kiukweli tu kocha hana mbinu wala ubunifu wowote katika mshindano ya mechi tatu wew unaenda kupaki basi ? Ameacha nje vijana ameweka wazee wakina Himid mao, kaweka watu wavivu yule mzungu hajui hata kujiposition.
Mwisho, Taifa stars wiki ijayo inarejea Tanzania.... Ni wakati sasa wa kuanzisha academy na kutengeneza kikosi chenye ushindani... Sio kikosi hichi ambacho watu wana umri mkubwa karbia wamfikie kocha wao,
kwa haraka haraka tu ukimtazama Mtu kama Himid mao ni aibu kwake kusakata soka mpka saivi....yule na Msuva saivi ndo walifaa wawe wanashindana kuhonga huko TFF mahela ili kupata kazi ya Kuifundisha Taifa stars.
Sitanii ndugu zangu hebu fikirieni wew ni mgeni na Umekutana na Taifa stars(huku kocha akiwa katoka mara moja) kati ya Timu nzima ile hivi kwa haraka harak tu si utadhania Himid mao ndo kocha wao. Ila kituko ni kwamba huyu ni First eleven player,
Hii ni aibu.
Sasa hao fitness coach wa kigeni wanafanya kazi gani....tuwafukuze tuuTaifa stars 75% ya wachezaji fitness Yao ni zero na hii ndiyo itatugharimu ikiwemo umri mkubwa n.k .
Angalia Mozambique , Cape Verde , Namibia au Angola mataifa Madogo kisoka wana fitness nzuri wanakimbiza Mpira .
Bongozozo amejisafirisha mwenyewe na watu wake .Tulikuwa tunachangisha Pesa za nini? Maana nimeangalia kwenye jukwaa mashabiki wa Taifa stars walikuwa ni Bongozozo na Ally Mayai pekee na watu kadhaa wakiwa wamevaa suti. Nikiona nchi nyingine wamepeleka mashabiki waluwalu kama akina Mzee wa utopolo wenye uwezo wa kujichafua mwili mzima na makorokocho yenye rangi za Taifa. Naamini kama garama za wachezaji caf wanalipa. Nilitarajia harambee zingewasafirisha mashabiki halisi wa mpira tunaowafahamu kutoka kwenye timu zetu
Washukuru Tanesco maana wamekuzuia kuona machungu yanayojirudia .Kmmmk Tanesco nimekosa game zote za jana huu ujinga sasa. Ila pongezi kwa chama langu Morocco kwa kukipiga vizuri kichwa cha mwendawazimu ili kipate ufahamu.View attachment 2875103
Tunasubiria kukamilisha mzunguko🤠Daah! Sidhani kama tuna chetu huku Rafiki.
Japo ngoja tuone mechi zijazo nazo.
Sasa mama atawapa nani feza ya kila goli?Congo 1-1 Zamb
Mdogo pale ni Feisal na Haji mnoga, ila kuanzia Samata, msuva, Himid, Tshabalala, mwamnyeto wote wamedanganya miaka tu hata nyuso zao zinaakisi hilo.Taifa Stars ndio inawachezaji wenye umri mdogo zaidi (Average)
ipo kati ya guinea ya ikweta vs guinea bissauWakuu leo saa 11 kuna mechi?
Kule Asia Japan asipo beba ndoo itakuwa sio poa. Japan wapo vizuri sana. Pia kura yangu inaenda kwa Korea Kusini [emoji2406]yaha mashindano ya AFCON yanayoendelea yalipaswa kufanyika mwaka jana ila kutokana na hali mbaya ya hewa nchini ivory coast yakasogezwa mbele nakufanyika 2024 ndio maana yanaitwa AFCON 2023 kitu ambacho kitapelekea kuwa na mashindano mawili ya AFCON yanayofatana kwakua AFCON inayofata nimwakani tu hapo 2025 nchini morroco kabla ya nchi za tanzania,kenya na uganda kwa pamoja hawajaandaa AFCON nyingine 2027, kwakua hii AFCON 2023 imegongana kinyakati na mashindano ya ASIAN CUP 2024 yanayoendelea pia mda huu, ni mashindano gani yamekuwa na msisimko sana!? binafsi sijafatilia hata mchezo mmoja katika mashindano ya ASIAN CUP 2024 na nimejiuliza kwa mda leo swali hilo bila kupata majibu kwakua sina access ya kufatilia mashindano hayo. timu za taifa kama australia, japan na korea kusini zimekuwa na wachezaji baadhi maarufu wanaokipiga ulaya , mnaofatilia pia hayo mashindano ya ASIAN CUP 2024 mnijibu hapa! Japo sijaridhiswa na mahudhulio kwenye mechi nyingi za AFCON