2024 Africa Cup Of Nations (AFCON) | Special Thread. Mechi ya fainali, FT: Nigeria 1 - 2 Ivory Coast. Ivory coast abeba ubingwa. 11.02. 2024

Pia mimi sijaelewa maana beki alikuwa kwenye mstari wa goli
Kinachoaangaliwa ni mtu wa mwisho bila kujali alikuwa beki au goal keeper. Pale Beki alienda kusimama golini keeper akiwa ametoka. Mchezaji anapokuwa offside ni pale anapowazidi wachezaji wa timu pinzani isipokuwa mtu mmoja tu.
Aliyefunga goli aliwazidi wote isipokuwa mtu mmoja tu ambaye ni beki aliyekuwa golini maana keeper alitoka.
 
Cameroon hii ni uchafu kuitazama…

Yaani miaka ile uanaangalia Cameroon mpaka una-enjoy unakutana na akina Rigobert Song kitasa cha maana, akina Raymond Kalla, DjembaDjemba, Ndiefi, Etoo, Mboma na wengineooo

Leo hii akina Joel Matip wanagoma hadi kuchezea timu ya taifa, wanaokubali kuja kucheza ni mabishoo hawana uchungu na timu yao🚮🚮🚮
 
Ninachojiuliza offside inaangalia tu position ya kipa? Mbona kuna beki alikuwa nyuma ya kipa?
Unatakiwa uwe nyuma ya wachezaji angalau wawili wa timu pinzani kabla ya kufunga goli jamaa aliyefunga goli alikuwa nyuma ya mchezaji mmoja tu wa Cameroon ambaye alikuwa ni beki aliyekuwa golini wachezaji wengine wote 10 wa Cameroon ikiwemo kipa wao walikuwa nyuma ya mfungaji hiyo ni Offside
 
Yan imekua team ya ovyo sana.

Hawa Giants wengi wanaanguka sana vby.
 
Hii timu ni aibu kuishabikia kwakweli inacheza mpira wa ovyo mno bora wangeishia tu makundi
 
Relax dogo. Nimesema mtazamo wangu juu ya uchezaji wake. Heshimu mawazo ya wengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…