2025 CHADEMA twende na nani kati ya Lissu au Mbowe?

2025 CHADEMA twende na nani kati ya Lissu au Mbowe?

Kinachombeba Mbowe kumlinganisha na mgombea wa ccm ni kesi aliyonayo?

It's true huenda kweli amesingiziwa lakini sababu hiyo pekee haimfanyi awe mgombea bora!

Labda utuambie amekupa sera zipi ili tuzipime!
 
Kisiasa mpaka sasa FAM, LISSU wote wapo juu ,ni swala la kukubaliana tunapanda na nani na wao kukubaliana tu

Hata ivyo umesema ukweli, mgombea wa ccm akiwa SSH, ni mgombea weak hata Mie nikisimamishwa na CHAMA saa 7 mchana nimemaliza biashara,

Ikumbukwe uchaguzi 2025 sio uchaguzi na CCm ,bali uchaguzi kati ya dhuluma na ukandamizaji, lazima CCM waondoke ,ZAMBIA NDANI YA TZ inakuja 2025
Mpaka sasa tuna upinzani dhaifu kuliko wakati wowote katika historia ya upinzani na vyama vya upinzani hapa Tz. Hakuna chama hata kimoja chenye mtu ambaye anakubalika na watanzania wengi kama mgombea wa kiti cha urais kutoka upinzani. Wapinzani wamekuwa so weak kiasi kwamba wamebaki tu kimya hawakemei waziwazi mambo mabovu yanayofnywa na serikali kwa kuogopa kushambuliwa au hata kuuwawa.

Kama wapigania uhuru wa mataifa haya ya kiafrika wangekuwa waoga kama walivyoviongozi wengi wa vyama vya upinzani hapa Tz naamnini mpaka leo nchi nyingi za kiafrika zingekuwa bado zinatawaliwa. HAKUNA TENA UZALENDO BALI NI MASLAHI TU.
 
SSH anweza akawa weak candidate lakini CCM bado sio chama dhaifu...

Kwa wapinzani kushinda uchaguzi mkuu inahitaji kukidhoofisha Chama cha Mapinduzi kwa sababu bila hivyo CCM hata wakiweka jiwe wanaweza kushinda...

CCM wana fitna, wana watu, wana mifumo...
Kuidhoofisha ccm ni kuiondolea nguvu za dola, yahani kumuweka samaki nje ya maji.
 
Sio hivyo tu siasa za kwenye majukwaa pia haziwezi ,Upako wa kisiasa kwake upo chini, sio kwamba Rais lakin tuliomfatilia kampeni za 2020 Kama mgombea mwenza ukubalikaji wake ujengaji wa hoja aliachwa mbali na mgombea mwenza wa CHADEMA,

Sasa nafasi ya urais si ndo itakua balaa, Sana ataeleza ujenzi wa madarasa, nalo jibu litakua MOJA kwamba ni pesa za uviko

Atasema miladi imemalizika,sijui reli, Bwawa,n.k jibu litakua ni MOJA tu TOZO ZETU,
Akija na mpango wa kuboresha maisha ,ataambiwa Tumeisha shutuka hakuna mitano tena

Hoja zinakua zimekwisha
Speech zake nyepesi hatari, kuhutubia hamna kitu, Hana Strong hold ATA moja uku bara,,
 
Kuidhoofisha ccm ni kuiondolea nguvu za dola, yahani kumuweka samaki nje ya maji.

Na hapo ndipo kilipo kitendawili, ambacho kwa kiasi Mwl Nyerere alikitolea dokezo la jawabu lake, kwamba ili kuidhoofisha CCM ni hadi pale kutapotokea mpasuko ndani yake na upinzani kuanzia ndani...
 
Na hapo ndipo kilipo kitendawili, ambacho kwa kiasi Mwl Nyerere alikitolea dokezo la jawabu lake, kwamba ili kuidhoofisha CCM ni hadi pale kutapotokea mpasuko ndani yake na upinzani kuanzia ndani...
Na dokezo hilo la marehemu Mzee JKN sioni likitokea kwa utaratibu na Sheria zilizopo, upande wa raisi ndo washindi.
 
Ccm hawakubali uchaguzi ufanyike ktk nchi hii na wao ndio wa kwanza kusema upinzani ni dhaifu huku wakiwaogopa kwenye sanduku la kura.

Wanalazimisha waendelee kutumia tume yao ya uchaguzi kwa sababu wanafahamu wananchi hawako nao kwani eti wao wako na polisi, Tiss na tume yao ya uchaguzi.

Kama hali itabaki kama ilivyo basi hamna kabisa haja ya kushiriki huo uchaguzi feki wa 2025 kwani itakuwa ni kuhalalisha uhuni wa ccm na vikaragosi vyake.
 
Mpaka sasa tuna upinzani dhaifu kuliko wakati wowote katika historia ya upinzani na vyama vya upinzani hapa Tz. Hakuna chama hata kimoja chenye mtu ambaye anakubalika na watanzania wengi kama mgombea wa kiti cha urais kutoka upinzani. Wapinzani wamekuwa so weak kiasi kwamba wamebaki tu kimya hawakemei waziwazi mambo mabovu yanayofnywa na serikali kwa kuogopa kushambuliwa au hata kuuwawa.

Kama wapigania uhuru wa mataifa haya ya kiafrika wangekuwa waoga kama walivyoviongozi wengi wa vyama vya upinzani hapa Tz naamnini mpaka leo nchi nyingi za kiafrika zingekuwa bado zinatawaliwa. HAKUNA TENA UZALENDO BALI NI MASLAHI TU.
Sawa bwana , mawazo binafsi ni haki yako
 
Back
Top Bottom