2025 CHADEMA twende na nani kati ya Lissu au Mbowe?

Kinachombeba Mbowe kumlinganisha na mgombea wa ccm ni kesi aliyonayo?

It's true huenda kweli amesingiziwa lakini sababu hiyo pekee haimfanyi awe mgombea bora!

Labda utuambie amekupa sera zipi ili tuzipime!
Na wewe pewa kesi
 
Upinzani dhaifu Ila unawatoa kamasi watawala
 
Kabisa CCM wanawaogopa wapinzani wao hatari,,,Ila kwenye keyboard wanasema ni dhaifu
 
Wazee wakupiga kampeni huku ndege inajikoki airport, hata matokeo hayaja tangazwa washatimukia ughaibuni. WAKUMPA KURA NI SSH TU. syo hao madalali.
We mpe ni haki yako
 
Mwaka 2020 ulikuwa uchaguzi mwepesi sana kwa CCM...

1995 na 2015 hii ndio miaka ambayo ulimi uliwatoka CCM kwa kupelekeshwa na upinzani...
Uchaguzi mwepesi kwa ccm ilikuwa 2000 na 2005 kuanzia hapo ccm haijawahi kuwa na uchaguzi mwepesi.

CCM ilishazidiwa kwa hoja na vyama vya upinzani tangu 2010 mpaka hapo haijawahi kuwa na hoja shawishi kwa wapiga kura.

2015 ccm ilitumia mbinu kushinda uchaguzi na ilifanikiwa probably ilisoma udhaifu wa upinzani walielekeza nguvu kubwa kushinda urais na siyo bunge ccm wakaelekeza nguvu kwenye kuretain majority bungeni na wakatumia mbinu kuretain urais walifanikiwa wakiamini watajipanga upya kihoja lakini walikosa hoja.

2020 CCM haikuwa na mbinu za kushinda uchaguzi ila ilitumia nguvu kushinda uchaguzi ndiyo maana ni uchaguzi pekee ulioacha makovu na michirizi ya damu Tanzania bara na visiwani kwa mara ya kwanza.

Sasa wameshatumia mbinu kushinda uchaguzi 2015, wametumia nguvu kushinda uchaguzi 2020. 2025 watatumia nini ???

Moja ya jambo ambalo ccm wanalifurahia kwa sasa ni CHADEMA kuendelea kususia chaguzi na ACT kuendelea kuanzisha harakati ndogo katikati ya harakati kuu hii inaipa ahueni ccm na kibaya zaidi response ya wananchi nayo ni ya tabia za jongoo kama ilivyo tabia ya jongoo kwa chama kikuu cha upinzani.
 
Kinachombeba Mbowe kumlinganisha na mgombea wa ccm ni kesi aliyonayo?

It's true huenda kweli amesingiziwa lakini sababu hiyo pekee haimfanyi awe mgombea bora!

Labda utuambie amekupa sera zipi ili tuzipime!
Mbowe has been a quality candidate from day one probably kinachomwangusha ni trust issues kwenye jamii anayotoka.
 
Kwanza siyo kweli kwamba wapinzani ni waoga.
Wamepiga vita for 20 years ambayo inafanya wastahili pongezi.

Kinachokufanya uone upinzani ni dhaifu ni dola kuwanyima jukwaa tu, wakipewa jukwaa ndiyo utajua wanauwezo kiasi gani.

Magufuli aliwafungia kufanya siasa for five years lakini alipowafungulia ilimlazimu kukodi mpaka watu wakumpiga mawe mgombea wa upinzani pale chato.

CCM imepata ahueni sana upande wa Zanzibar kwa sasa kuliko kipindi chochote kwa matukio matatu yaliyofuatana.
1. Kusambaratika kwa CUF
2. Kifo cha Maalim Seif
3. Wafuasi wa CUF kujiunga ACT Wazalendo badala ya CHADEMA.
 
Bila Nek,policcm,Tissccm na masoja,kwa hali waliyonayo wananchi,mgombea yo yote wa Chadema anaweza kushinda uchaguzi 2025 hata kama anatoka kijijini kusikosikika hata Redio!
 
Sisiemu hata iwe na mgombea dhaifu itashinda tena kihalali sababu upinzani hawana mtu sahihi... ni majizo ma magaidi na watetezi wa mabeberu tu ndio wako huko... huyu mama binafsi simkubali ila atashinda saa tatu asubuhi...
 
Mbowe 2005 alipata kura laki tano.

Lisu 2020 akajizolea kura milioni moja.

Sasa hao ndio unasema ni mwiba kwa CCM??
Hizo chaguzi za kihuni ziliandaliwa na kutangazwa matokeo yake na nani.

Yaani Yanga wanacheza na Simba halafu eti refa anatakiwa kuwa Mshindo Msola au Murtaza Mangungu, kuna mechi hapo kweli, wewe hata akili hutumii ili ufahamu kwamba Tanzania hakuna uchaguzi ila ni uhuni tu.
 
2025 Chadema tunaenda na Katiba Mpya
 
Sisiemu hata iwe na mgombea dhaifu itashinda tena kihalali sababu upinzani hawana mtu sahihi... ni majizo ma magaidi na watetezi wa mabeberu tu ndio wako huko... huyu mama binafsi simkubali ila atashinda saa tatu asubuhi...
Akili ndogo wewe, kwa nini hao wanaoweza kushinda wanaogopa tume huru ya uchaguzi na badala yake wamekomalia tume yao. Jibu hilo swali kwanza.
 
Mbona Lowasa alipata milioni sita 2015 na Magu akapata milioni 8??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…