Pre GE2025 2025 kuna uwezekano Paul Makonda akachukua fomu ya Urais. Ndipo Rais Samia ataijua vizuri rangi ya Paul Makonda

Pre GE2025 2025 kuna uwezekano Paul Makonda akachukua fomu ya Urais. Ndipo Rais Samia ataijua vizuri rangi ya Paul Makonda

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Atachukuaje fomu wakati rais samia hajamaliza mihula miwili kwa mujibu wa katiba ya chama chao?
 
Labda achukue fomu ya ubunge, ya urais ni mpaka 2030 na atachuana na vigogo wengine wazito akina madelu na yule jamaa wa kipara
 
Katiba inataka mgombea Urais angalau awe na degree moja.

Nikumbushe Makonda ana degree ya kutoka chuo gani?
Katiba ipi? Kama mnadai Katiba mpya hata ya Sasa hamuelewi Huwa mnalalamika nini?
 
Nimekaa pale nawazoom Watanzania mimi mlinzi msomi na mwenye vinasaba vya kinabii.

Hizi sifa anazozichukua huko mitaani kwenye ziara zake huyu Mheshimiwa zitamfanya 2030 aione iko mbali.

Maana kwa sasa target yake kubwa ni Urais na si cheo chochote. Aliamini 2025 angeachiwa kijiti na Magufuli lakini dili likagoma mapema tangu tu alipopigwa chini kwenye kura za maoni jimboni (Kigamboni).

Sasa baada ya kuukwaa uenezi anaitazama 2030 lakini kwa sifa anazopata mtaani hatoweza kusubiri 2030.

Mwakani 2025 anajilipua rasmi liwalo na liwe. Kama akilljilipua kuna uwezekano akaungwa mkono na wanakamati wengi hapo ndipo Watanzania wataona kasheshe.

Mimi simpendi Makonda, hata nyuzi zangu zinaonyesha hilo kwa uwazi kabisa lakini akigombea Urais nitamuunga mkono.

Kwa jinsi alivyo yule kijana ataleta maendeleo makubwa hapa nchini, naamini makandokando yake atayaacha.

Suala la Rais aliyeko madarani kupiti bila kupingwa kwenye kura za maoni huko CCM usilitafakari sana kwenye uchaguzi wao wa ndani 2025. Lolote linaweza kutokea.
Makonda hata akigombea na Samia kama mgombea binafsi anamtoa asubuhi tuu.
 
Wacha kupiga ramli zisizokuwa na kichwa wala miguu.Inaelekea Makonda anakunyima usingizi.Mtapigwa spana mpaka mkome.
 
Back
Top Bottom