2025 uchaguzi ukiwa huru na haki, Rais Samia hawezi kushinda uchaguzi

Shauri nini kifanyike kukabiliana na hali ngumu ya kiuchumi, hayo ya uchaguzi bado mbali sana.
Shaurianene uko bungeni,, Mambo ya ushauri wa kiuchumi non of my business
 
Unaropoka tuu kama unajamba huna hata Takwimu,Samia kaajiri zaidi ya ajira rasmi 12,000 na kapandisha madaraja zaidi ya 190,000.

Ongea kingine wewe kenge mwenye chuki.

Yanini kuandikia mate? Si uchaguzi ukafanyike chini ya katiba mpya?
 
Afu Samia kapanic mapema yaani kila tukio analeta kampeni, kwenye Mpira, TV, events zote Ni Samia,lakini still watu hawamuelewi[emoji1]

Umemdadavua vyema karata yake pekee ni wizi wa uchaguzi.

Ukweli huu kuwekwa wazi ni habari mbaya mno kwa wale vijana wake wa propaganda mitandaoni.

Hao kula yao inategemea kuonyesha mafanikio ya propaganda hizo per day per day.
 
Hata jpm hakushinda. Alituzimia internet.

Haijawahi tokea ktk bara la afrika.
 
Katiba mpya 😬😬😬😬.

Mtaishia kutoa excuses hadi mnazeeka.

Katiba mpya inakuudhi? 😁😁

Kuzeeka tu? Hiyo agenda mbona itaishi mno hata kama sisi tukiwa makaburini jana, leo au kesho?

Kwani kina Ben Sanane, Lijenje, Mawazo wako wapi?

Udhwalimu haukuwahi kushinda mjomba.
 
Umemdadavua vyema karata yake pekee ni wizi wa uchaguzi.

Ukweli huu kuwekwa wazi ni habari mbaya mno kwa wale vijana wake wa propaganda mitandaoni.

Hao kula yao inategemea kuonyesha mafanikio ya propaganda hizo per day per day.
Ndio maana yuko bize na Kikosi kazi cha kina Zitto
 
Katiba mpya inakuudhi? 😁😁

Kuzeeka tu? Hiyo agenda mbona itaishi mno hata kama sisi tukiwa makaburini jana, leo au kesho?

Kwani kina Ben Sanane, Lijenje, Mawazo wako wapi?

Udhwalimu haukuwahi mjomba.
Katiba mpya haileti ugali mezani.
 
Mkuu, hakuna siku mgombea wa CCM atashindwa uchaguzi wa Urais hata kama atakuwa kichaa.

Kwa katiba hii, tutasubiri mno NEK ikipitisha jina imetoka hyo, hata kama hatutapiga kura.
 
Kumpigia kura huyu mama labda niwe nimelogwa .Bora nipigie kura tofali
Upo sahihi sana mkuu. Ila CCM itashinda nakuhakikishia na SSH atarudi tena ikulu. Sababu kuu tatu ni hizi;

1. Watanzania wengi bado wana mwamko mdogo kuhusu uchaguzi. Hawajui thamani ya kura yao. Hivyo wengi wanaotaka mabadiliko ya kweli huwa hawajitokezi kupiga kura. CCM hutumia mwanya huo kuhamasisha wanachama wake hai takribani milioni 8 nchi nzima kujitokeza kumpigia kura mgombea wao hata kama ni bogus.

2. Wakati wa uchaguzi ukifika wapinzani huwaleti mgombea wa maana zaidi ya kuleta watu kama TAL au ZZK ambao hawakubaliki wala hakuna anayewajua huko kijijini ambapo ndio kuna wapiga kura wengi mtaji wa CCM. Hao niliowataja muda mwingi wanatumia kufanya harakati ambazo ni watu wenye elimu na uelewa kama mimi naweza kung'amua propaganda na mambo ya msingi kwa maslahi ya taifa. Kijijini kwetu Butiama hakuna anayewaelewa hata kidogo.

3. CCM wakati wa uchaguzi wanakuwa wamoja, focused, determined na well organized kuliko kipindi chochote hutumia mtaji wa watu, fedha na hata nguvu kuhakikisha wanachukua dola. Watanzania wengi ni waoga husubiria haki iwafuate hawana uwezo wa kupigania haki kwa maandamano wala chochote.

Kiufupi watanzania tumeridhika tunajua malalamiko tu na kufuatilia umbea, vibonzo na mpira wa Simba na Yanga nchi imeachiwa CCM tena kundi dogo tu
 
2025 kwenye siasa ni mbali sana ku project jambo kama hilo. Kuna kufariki, kubadilika sheria na sera, hamahama ya wanasiasa, vyama vya upinzani vutakavyo behave, hali ya uchumi itakavyokuwa, matokeo ya uchaguzi ndani ya CCM 2022/3 na consequence zake _ Kumbuka ya Lowassa 2015, hali ya uchumi na siasa za nje huko duniani zitakavyotuathiri nk nk.

Siasa ndani ya wiki moja hubadili mustakabali mzima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…