Kiranga alishawauliza kama mungu yupo kweli je iweje mtu anazaliwa bila kumjuwa?
na ili amjuwe basi ni lazima akatandikwe viboko madrasa au mafundisho kanisani?
but wakaingia chini ya meza na hawakurudi na jibu...
Nataka kukyonyesha jinsi ulivyo mvivu wa kutafakari.
Mambo ya tech yameanzia na yanaendelezwa na hao hao ambao walianza kuamini Mungu ambaye kwako unauliza kwa njnj iwe far east tu.
Niambie kiluchoanzia Africa ukiacha ebora , kipindupindu na maradhi mengine.
Twende kazi...
Vinathibitisha kwa kuwa vyenyewe sio infinity kwa kuwa sio inglfinity Ina maana kuna kilichosababisha viwepo
Aliyesababisha viwepo ni Mungu aliyeumba ulimwengu na vilivyomo na ambaye ndiye chanzo cha Uhai.
Namba 2. Waarabu walifanya utumwa East Africa tu, na watumwa wao wengi waliuzwa Uarabuni na Ulaya tu. Kule Afrika Magharibi (Ghana, Senegal, Mali, Nigeria, n.k) ambako ndiko utumwa wa kutisha ulifanyika biashara hiyo ilifanywa na wazungu hasa wareno na wahispania na watumwa wao walipelekwa Amerika zaidi. Hivyo biashara ya utumwa afrika haikufanywa na waarabu tu. Pili, biashara ya utumwa ni biashara ya kale sana wazungu na waarabu walianza kufanyiana biasha hii kabla hawajakuja kuifanya Afrika, hata bibilia na misahafu inaitaja biashara hii kuwa ni halali. Tatu, watawala wetu wa Kiafrika ndo waliokuwa wanauza watu wao kwa wageni kama watumwa na kupewa nguo, shanga, vioo, bunduki, visu, vikombe, n.k.
Namba 4. Mitume iko kila sehemu na ilikuwa ikitumika kufanikisha mambo ndani ya jamii husika ila mitume yetu iliitwa ya kishenzi na watawala wa kigeni. Yesu na Mohamed SAW ni watu maarufu kwa wakati wao waliotumika kutatua matatizo fulani ndani ya jamii sawa na wale waliotatua shida ya usafiri, umeme, mawasiliano, n.k. Wao walitatua shida ya ukosefu wa amani ndani ya jamii na wengine walitatua shida za maji, usafiri, mwanga, joto, umeme, n.k. Hivyo MUNGU ni kweli yupo bila kumung'unya maneno na akina Yesu, Mohamed, Mussa, Yakob, Ibrahim ni baba wa Amani duniani wanaopaswa kuheshimiwa pia sawa na akina Galileo, Estens, Boys, Archemedes, n,k
Umenikumbusha Mkuu,jamaa yangu mmoja wa Kibongo alitembelewa na rafiki yake kijana wa kizungu maskani akamkuta jamaa anasoma Bible.Hakika yule mzungu alishangaa sana kuona jamaa yupo bize na bible ambayo yeye mzungu anaiita novel
Newton, Galileo ,Kepler to mention but a few ni moja ya watu wajinga kadri ya mpum.bavu wewe
Ivi mkuu ulitaka niseme biblia na quran zipo sahihi kwa pamoja? Nilichokiona mchanganyiko wa ukweli, uongo and many unreasonable teachings.
Kitabu cha Mungu kitasemaje uongo?
Ikiwa unaamini hao ndio walioleta/walioanzisha hayo mambo ya tech, kwanini Mungu amepiga lana ya vita visivyoisha na kuahidi mateso, mashaka na tabu kwa kila uzao? (there generations)
Sasa je huo ndio uthibisho? If yes, hembu niambie tu nini maana ya kuthibitisha?
Basing on underline 1.Hiyo ni Lugha yenye maana pana. Kaa Muda Mrefu na Bibilia utaelewa. Wote waliompokea Mungu kwa Imani wanafananishwa na uzao wa ibrahimu ambao kupitia izrael ujumbe ulipangwa kuwafikia watu wote. Hiyo ni mipango ya Mungu. Lakini baada ya Yesu, hakuna cha muisrael wala myunini, wala yoyote. Injili ni kwa watu wote.
Uhusiano: Baada ya Mwanadamu kutenda dhambi edeni na kifo kikatangazwa kwa mara ya kwanza. Lakini Mungu aliandaa mpango wa kuwakomboa wanadamu wote watakao kubali ili Turudie katika hali ya zamani kabla ya dhambi na kumuangamiza shetani kabisa. Njia aliyoamua ni kuwa kupitia israel Mwokozi wa ulimwengu azaliwe, Ili kila atakayemuamini apate uzima ule wa milele. Ndio maana Kwa Mungu sasa hakuna cha Muisrael wana msukuma wala nani, bali ni wanaomwamini Mwokozi wa ulimwengu na waliokataa. Hata waisrael waliomkataa wataangamia wote. Muda sio mrefu huyu mwokozi atakuja na kila jicho litamuona kuwapa wote sawasawa na uchaguzi waliuchagua. kama ni uzima wa milele au upotee milele. Hakuna tukio la kiulimwengu lililobakia kutokea hadi sasa ni kuja kwa yesu tu ndio kunasubiriwa dalili zote tayari.
Kuchagua kujiunga na imani hii ya kumsubiri yesu na Kumuamini yesu ndio uchaguzi wa thamani kuliko zote ktk muda huu tunaoishi ktk ukingo wa historia ya dunia.
Acha kupoteza Muda, Mungu yupo (finite mind cannot understand fully the Infinity GOd). ukiimarika katika majibu ya mashaka yako mkuu imarisha na watu wote wanaokuzunguka.
watu wengi wanoamini dini ni wajinga na waoga wa kifo.
Newton, Galileo ,Kepler to mention but a few ni moja ya watu wajinga kadri ya mpum.bavu wewe
Unajua kutofautisha kati ya wengi na wote .. wewe ni mmoja ya wajinga ninao ongelea.
Mkuu tatizo ni research yako mie ningeomba uchambuzi wa kina juu ya research yako. Aina ya maswali uliyouliza yanaonesha utata wa kwenye research.
Nimeweka kukuonyesha ulivyo mvivu wa kutafakari, na hoja yako ni matokeo ya uvivu wa kutafakari.
Bado unahoja kuhusu Waliokuletea tech ndo hao hao walioleta dini kwa wenzio ?
Habari ya vita na mengineyo bado ni hoja zilizojengwa kwenye msingi wa sinker na sio thinker
Mtoa mada kama huamini kuwepo kwa Mungu, je unaamini kuwepo kwa shetani??. Na unadhani wewe umetoka wapi?
Mkuu Shetani ni nani? ni kiumbe? Embu nipe maana ya shetani ili nikujibu, may be im one of them according to your perspective.
Mkuu hatuelewani kabisa. Embu tafuta mtu, mpe mawazo na hoja unayotaka kusema then mwambie aandike yeye ili wewe uitume tu.
Mungu sio wa kumfanyia masikhara, mtoa mada "take care"
Mkuu nahisi ungeorodhesha hayo maswali niliyouliza na ambayo yanakupa mashaka na ufanywaji wa research.
Or
Ungeanza na kuulizia finding moja moja kati ya hizo tisa, then tuone hofu yako iko wapi.
Hata nikitofautisha Kati ya wengi na wote bado hao wasomi nguri ni sehemu ya hao wengi labda uweke exception.
Kwani kufikiri mnaogopa ?