Weka maswali yako hapa unibiwe
Lakini kitu kingine ambacho wavivu wa kufikiri Kama wewe hukitumia ni viroja zaidi kuliko hoja, Mimi ninafahamu msemo wa kiswahili usemao ukimuona Kobe juu ya mti ujue kawekwa, hiyo Ina maanisha chochote ukionacho chenye mwanzo na ukomo ujue kimefanywa kuwa kilivyo.
Sasa basi maswali yenye mashiko ukiacha sijui mkanganyiko kwenye vitabu sijui ni nini na nini vile hayo waachie watoto wa Shule za awali wewe panda kidogo onyesha ukomavu kifikra kwa kujiuliza maswali kuhusu ;
Nini chanzo cha uhai duniani, nani/nini aliyefanya dunia iwe hivi ilivyo na kwa nini ?
Nini sababu ya binadamu kuwepo hapa duniani ?
Lakini GT kuruka maswali hayo na kija JF au mtaani na viswali vya hapa panasema watu 10 na hapa panasema watu 100 ni utoto.
Haya jibu maswali ya msingi niliyoweka nawe weka maswali yako ya chekechea usaidiwe.
Hakika hutahitaji mjadala wa kukuuumbuwa kwa viswali vya chekechea utakuwa umejua ujuha wako hapa hapa.
Haya twende kazi.
Ndugu yangu kweli upotayari kujibu maswali yangu!!? Ok naomba basi unijibu tu maswali machache tu ambayo siyaelewi yapo ndani ya biblia:
1. Je asili ya mungu ni nini?
2. Baada ya Kaini kumuua Abel alijitenga na uso wa mungu, Je alipata wapi mke na matokeo yake kukawa na wanefili?
Genesis (4:16-18)
3.Naomba unitafsirie maana ya maandiko haya kwenye Genesisi 6:
1.And it came to pass, when men began to multiply on the face of the earth, and daughters were born unto them,
2That the sons of God saw the daughters of men that they were fair; and they took them wives of all which they chose.
Naomba tuanze na maswali hayo kwanza tutaendelea.
Halafu:-
Isaya 53:
1 Ni nani aliyesadiki habari tuliyoileta?
Na mkono wa BWANA amefunuliwa nani?
2 Maana alikua mbele zake kama mche mwororo,
Na kama mzizi katika nchi kavu;
Yeye hana umbo wala uzuri;
Na tumwonapo hana uzuri hata tumtamani.
3 Alidharauliwa na kukataliwa na watu;
Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko;
Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao,
Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu.