Light Saber Imetosha Sasa
JF-Expert Member
- Nov 3, 2017
- 5,182
- 9,586
Tanga: Mji wa "Linga"
Kuna mgeni mmoja alifika Tanga, akamkuta binti mmoja mstaarabu amekaa mlangoni. Mgeni: "Samahani dada, hapa ndio Tanga?" Binti (kwa sauti ya upole na madaha): "Hapa hapa kaka yangu, karibu ukanyage ardhi ya mahaba. Unataka nini? Maji ya baridi? Tunda? Au unataka nikupulize kwanza upepo wa bahari ndio useme shida yako?" Mgeni: "Dah, mimi nilikuwa natafuta duka tu nianze safari." Binti: "Safari haina haraka kaka, duka halikimbii... karibu unywe kwanza kikombe cha kahawa, huko unakoenda utafika tu majaliwa ya Mungu." (Mgeni hadi leo hajarudi kwao!)