Abel na Kaini (kizazi cha Adamu na Hawa); Je, wake zao ni kizazi cha nani?

Abel nadhani hakuoa!!
Ila hili swali najiuliza mara nyingi sana na hata kuuliza watu wengine ikowamo viongozi wa dini!
Sorry ulipowauliza viongozi wa dini walikujibu nini labda mwenzetu unaweza kuwa ulijiwa jibu angalau la kulidhisha
 
mchina muafrika mzungu mwarabu mjapani walikuaje na asili tofauti na adam na hawa? na kama asili ya mwanadamu ni pale eden, wamarekani wabrazil waargentina wametokea wapi? sababu wapo bara tofauti na bara waliloumbiwa adam na hawa.
Maswali magumu sana haya nadhani majibu hayawez kupatikana na tumuache mungu aitwe mungu
 
Duu kumbe asanten mnatufunza vitu hapa leo mambo mengine ni magumu hata kuyafikiria
 
hizo sasa ndo rafsiri zililopondukia hata mwandish wa biblia hajui hayo usemayo
 
Sorry ulipowauliza viongozi wa dini walikujibu nini labda mwenzetu unaweza kuwa ulijiwa jibu angalau la kulidhisha
Kuna aliyeniambia kuwa Kaini alioa ndugu yake, wa kuzaliwa tumbo moja kwani wazawa wa kike waliozaliwa hawakuandikwa!
Lakini katika maandiko yanaeleza kuwa Kaini alikimbilia nchi ya Nodi na kuoa huko mkewe!
 
Adam aliishi miaka 930.Biblia inasema alizaa wana na binti wengi.Kaini na Habili walioa miongoni mwa hao binti.Mpango wa Mungu ulikuwa ni kuzaa na kuongezeka na kuijaza nchi.wote tu wazao wa adam na hawa.
 
Hivyo inaonesha kuwa kumbe kulikuwa na watu wengi tuu ila hawakuandikwa katika bibilia
 
Kaini na Abeli walioa dada zao ambao walikuwa watoto wa adam na hawa pia. Katika kipindi cha zamani kuoana ndugu lilikuwa jambo la kawaida kabisa na ukizingatia wakati wa Adamu na Hawa kulikuwa hakuna uzao mwingine zaidi ya huo.

Hivyo Kaini na Abeli walioa dada zao.
 
Na we we una ushahidi gani kuwa hatukuumbwa na Mungu weka na evidence ya udictator wake ili tujue coz huamini uwepo wake then unataka ushahidi gani??
 
Mkuu hivi vitabu vya dini vinaacha maswali mengi sana mpaka tunatilia shaka uhalali wake.
Mkuu kwani umelazimishwa kuamini mbona kuna vtabu vingi utaweza kuvisoma na kuamini. Hyo ni imani ka wewe unavotilia mashaka na wengine hivo hivo
 
Adam aliishi miaka 930.Biblia inasema alizaa wana na binti wengi.Kaini na Habili walioa miongoni mwa hao binti.Mpango wa Mungu ulikuwa ni kuzaa na kuongezeka na kuijaza nchi.wote tu wazao wa adam na hawa.
Wewe ebu kuwa serious kidogo, Abel alikuwa na mke? alizaa watoto? hao watoto waliitwa nani?....Abel si aliuwawa mapema sana?
 
Na we we una ushahidi gani kuwa hatukuumbwa na Mungu weka na evidence ya udictator wake ili tujue coz huamini uwepo wake then unataka ushahidi gani??
Tunaambiwa kuwa Mungu ni mkamilifu na anafanya kitu kwa ukamilifu.

Ila uumbaji una mapungufu mengi sana ambayo kama ni Mungu aliyeumba basi anajiharibia CV.Hatukuumbwa na Mungu kwa sababu tumezaliwa na wazazi wetu.

Maandiko yanayodai uwepo wa Mungu yamemchora kama Dude lenye ukatili, wivu, hasira na chuki sana.Ndio maana ameagiza mauwaji na uvamizi wa nchi za watu wengine.
 
Mkuu kwani umelazimishwa kuamini mbona kuna vtabu vingi utaweza kuvisoma na kuamini. Hyo ni imani ka wewe unavotilia mashaka na wengine hivo hivo
tuachane na habari za dini kwanza huwa navutiwa na wew naomba nije pm kukusabahi.
 
Zaman ilkuwa kawaida kuona ndugu kwa ndugu,ila baada ya binadam kuwa weng ikasitishwa,ila hz n hadithi za kutungwa
 
Hahahahahaha, walikuwa wanazaa asubuh na jion, jaman hizi fiction nyingne tujiongeze wenyewe kutafakari tuu. Wamekuwa kuku wa mayai
 
Naona wengi tunasoma Biblia kwa mistari michache na kufanya conclusions ambazo hazitusaidii kujibu maswali muhimu. Kwanza tuelewe stori ya Adam na Hawa imewekwa kwa kusudio la kumwelewesha mwanadamu na mahusiano yake na Mungu, na mtiririko wa maisha ya binadamu toka wakati huo hadi sasa. Adam na Hawa walikuwa wanadamu pekee ambao waliishi bustani ya Eden ikimaanisha kuwa wanadamu wengineo waliishi sehemu nyingine mbali mbali.
Ukisoma Mwanzo 1:26-29 wanadamu waliumbwa wengi tu na walikuwepo kila kona ya dunia kabla ya Adam na Hawa.
 
Bado hujajibu swali.tufanye walioa na miaka mia nane sasa kijiji kilitokana na kinanani?itakuwa walioana kaka na Dada maana hakukua na shangazi wala mjomba ni baba mama na watoto tu na hapo kwenye miaka zamani hawakuhesabu kama leo ilivyo siku zilikuwa chache tu na dunia ilikuwa ni sehemu wanazojua wao tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…