Abel na Kaini (kizazi cha Adamu na Hawa); Je, wake zao ni kizazi cha nani?

Abel na Kaini (kizazi cha Adamu na Hawa); Je, wake zao ni kizazi cha nani?

Abel nadhani hakuoa!!
Ila hili swali najiuliza mara nyingi sana na hata kuuliza watu wengine ikowamo viongozi wa dini!
Sorry ulipowauliza viongozi wa dini walikujibu nini labda mwenzetu unaweza kuwa ulijiwa jibu angalau la kulidhisha
 
mchina muafrika mzungu mwarabu mjapani walikuaje na asili tofauti na adam na hawa? na kama asili ya mwanadamu ni pale eden, wamarekani wabrazil waargentina wametokea wapi? sababu wapo bara tofauti na bara waliloumbiwa adam na hawa.
Maswali magumu sana haya nadhani majibu hayawez kupatikana na tumuache mungu aitwe mungu
 
Abel alimuoa pacha wa Kaini na Kaini alitakiwa amuoe pacha wa Abel ndipo Kaini akakataa kwani pacha wake alikuwa mzuri sana kuliko pacha wa Abel.Baada ya mzozo Adam akapewa maelekezo na Mwenyezi Mungu waandae sadaka na yayule itakayochukuliwa atakuwa imekubaliwa.Sadaka ya Abel ilikubaliwa na Kaini alikasirishwa sana na kuahidi lazima atamwangamiza Abel.Kaini alipewa mbinu na Shetani ya kumuua Abel na akamuua.Abeli akawa ndiyo mtu wa kwanza kuuwawa na Kaini akawa mtu wa kwanza kua.
Duu kumbe asanten mnatufunza vitu hapa leo mambo mengine ni magumu hata kuyafikiria
 
Swali jepesi sana.iko hivi
Adam na hawa hawakuwa watu halisi kama tulivyo mimi na wewe bali yalikuwa ni majina ambayo yalitumika kuwakilisha makundi ya watu.so Adam alikuwa anawakilisha wanaume na hawa alikuwa anawakilisha wanawake.lengo la kitabu cha mwanzo ni kuonyesha historia ya binadamu so isingewezekana kuzungumziwa namna kila mtu alivyopatikana so yakachaguliwa majina mawili ili yawe vielelezo au kuwakilisha makundi hayo ya watu.ukisoma vizuri kitabu chenyewe kinajieleza mfano habari ya nyoka kuongea unaona kabisa kwamba No kitu ambacho hakileti maana.so mwandishi wa kitabu kile alitumia majina ya adamu na hawa kwa maana hizo.mfano mzuri ni hadithi za sungura na fisi ambazo hutumia majina hayo kuwakilisha watu halisi.
hizo sasa ndo rafsiri zililopondukia hata mwandish wa biblia hajui hayo usemayo
 
Sorry ulipowauliza viongozi wa dini walikujibu nini labda mwenzetu unaweza kuwa ulijiwa jibu angalau la kulidhisha
Kuna aliyeniambia kuwa Kaini alioa ndugu yake, wa kuzaliwa tumbo moja kwani wazawa wa kike waliozaliwa hawakuandikwa!
Lakini katika maandiko yanaeleza kuwa Kaini alikimbilia nchi ya Nodi na kuoa huko mkewe!
 
Adam aliishi miaka 930.Biblia inasema alizaa wana na binti wengi.Kaini na Habili walioa miongoni mwa hao binti.Mpango wa Mungu ulikuwa ni kuzaa na kuongezeka na kuijaza nchi.wote tu wazao wa adam na hawa.
 
Kuna aliyeniambia kuwa Kaini alioa ndugu yake, wa kuzaliwa tumbo moja kwani wazawa wa kike waliozaliwa hawakuandikwa!
Lakini katika maandiko yanaeleza kuwa Kaini alikimbilia nchi ya Nodi na kuoa huko mkewe!
Hivyo inaonesha kuwa kumbe kulikuwa na watu wengi tuu ila hawakuandikwa katika bibilia
 
Kaini na Abeli walioa dada zao ambao walikuwa watoto wa adam na hawa pia. Katika kipindi cha zamani kuoana ndugu lilikuwa jambo la kawaida kabisa na ukizingatia wakati wa Adamu na Hawa kulikuwa hakuna uzao mwingine zaidi ya huo.

Hivyo Kaini na Abeli walioa dada zao.
 
Kwahiyo huu ujinga ndio mnaomezeshwa?

Una ushahidi gan kwamba Allah ndiye aliyetuumba?

Una ushahidi gani wa kuwepo kwa Allah?

Umesema kila mtu na Dada yake wa kuzaa nae, majina yao ni yepi?

Kama Mungu anafanya atakavyo yeye bila kushirikisha wanadamu, ina maana yeye ni dictator?
Na we we una ushahidi gani kuwa hatukuumbwa na Mungu weka na evidence ya udictator wake ili tujue coz huamini uwepo wake then unataka ushahidi gani??
 
Mkuu hivi vitabu vya dini vinaacha maswali mengi sana mpaka tunatilia shaka uhalali wake.
Mkuu kwani umelazimishwa kuamini mbona kuna vtabu vingi utaweza kuvisoma na kuamini. Hyo ni imani ka wewe unavotilia mashaka na wengine hivo hivo
 
Adam aliishi miaka 930.Biblia inasema alizaa wana na binti wengi.Kaini na Habili walioa miongoni mwa hao binti.Mpango wa Mungu ulikuwa ni kuzaa na kuongezeka na kuijaza nchi.wote tu wazao wa adam na hawa.
Wewe ebu kuwa serious kidogo, Abel alikuwa na mke? alizaa watoto? hao watoto waliitwa nani?....Abel si aliuwawa mapema sana?
 
Na we we una ushahidi gani kuwa hatukuumbwa na Mungu weka na evidence ya udictator wake ili tujue coz huamini uwepo wake then unataka ushahidi gani??
Tunaambiwa kuwa Mungu ni mkamilifu na anafanya kitu kwa ukamilifu.

Ila uumbaji una mapungufu mengi sana ambayo kama ni Mungu aliyeumba basi anajiharibia CV.Hatukuumbwa na Mungu kwa sababu tumezaliwa na wazazi wetu.

Maandiko yanayodai uwepo wa Mungu yamemchora kama Dude lenye ukatili, wivu, hasira na chuki sana.Ndio maana ameagiza mauwaji na uvamizi wa nchi za watu wengine.
 
Mkuu kwani umelazimishwa kuamini mbona kuna vtabu vingi utaweza kuvisoma na kuamini. Hyo ni imani ka wewe unavotilia mashaka na wengine hivo hivo
tuachane na habari za dini kwanza huwa navutiwa na wew naomba nije pm kukusabahi.
 
Zaman ilkuwa kawaida kuona ndugu kwa ndugu,ila baada ya binadam kuwa weng ikasitishwa,ila hz n hadithi za kutungwa
 
Jibu ni kwamba baada Mungu Kumuumba Adam ,na kuwambia malaika wammsujudie yaani wammpe heshima,m malaika wowote walisujudu isipokuwa huyu Iblis ambayo asili yake alikuwa ni jinni.kumbuka huyu huyu Iblis au ababil au abaa sijda alilelewa mbinguni na mpk akawa kiongozi wa malaika wote.ni kiumbe anajua mambo mengi sana mbingun.Kwa kukataa huko Mungu alimpa laana na kumshusha duniani.

Adam na hawa waliishi peponi walishushwa duniani baada ya kuasi maagizo ya Mungu . Baada ya Adam na hawa Kuletwa duniani Mungu aliweka utaratibu wa wao kuzaa na walizaa kila siku ASUBUHI na jioni -elewa mwanzo wa dunia siku moja haikuwa kama ya Leo ambapo masaa yalikuwa hayakimbii saana kama maisha ya Leo.

so hapo Sheria ya kuoa ilikuwa tofauti na za miaka hii.baada ya kuja mitume na manabii KULETA taratibu za dini.na mambo kama hayo ya kuoa. So ilikuwa hivi .mtoto aliyezaliwa jioni alikuwa ANAOLEWA na MTU aliyezaliwa ASUBUHI.walitoka tumbo moja lkn utaratibu ulikuwa hivyo. Naa kwani watoto walikuwa wanakuwa haraka haraka kuliko maisha yetu.

haya.ya Leo.sasa hao akina kabil walioa ndugu zao wa tumbo moja kilichotenganisha ni Muda tu.Nasisitiza wa ASUBUHI alioa /kuolewa na wa jioni.asante
Hahahahahaha, walikuwa wanazaa asubuh na jion, jaman hizi fiction nyingne tujiongeze wenyewe kutafakari tuu. Wamekuwa kuku wa mayai
 
b55aee8c5956b34290e83734ce61925e.jpg
 
Naona wengi tunasoma Biblia kwa mistari michache na kufanya conclusions ambazo hazitusaidii kujibu maswali muhimu. Kwanza tuelewe stori ya Adam na Hawa imewekwa kwa kusudio la kumwelewesha mwanadamu na mahusiano yake na Mungu, na mtiririko wa maisha ya binadamu toka wakati huo hadi sasa. Adam na Hawa walikuwa wanadamu pekee ambao waliishi bustani ya Eden ikimaanisha kuwa wanadamu wengineo waliishi sehemu nyingine mbali mbali.
Ukisoma Mwanzo 1:26-29 wanadamu waliumbwa wengi tu na walikuwepo kila kona ya dunia kabla ya Adam na Hawa.
 
Adam na eva waliishi mia zaidi ya mia tisa.



Ukituliza kichwa vizuri utajua kaini na abel walioa nani.


Ungeuliza kain na abel walioa wakiwa na umri gani ingekuwa hoja nzito.

What if walioa wakiwa na miaka mia saba.
Miaka mia saba sikijiji kabsaa.
Bado hujajibu swali.tufanye walioa na miaka mia nane sasa kijiji kilitokana na kinanani?itakuwa walioana kaka na Dada maana hakukua na shangazi wala mjomba ni baba mama na watoto tu na hapo kwenye miaka zamani hawakuhesabu kama leo ilivyo siku zilikuwa chache tu na dunia ilikuwa ni sehemu wanazojua wao tu.
 
Back
Top Bottom