A
Anonymous
Guest
Ndugu wana JF,
Kuna jambo linazidi kuwa kero kwa wasafiri wengi wa mabasi ya mikoani. Ni hii tabia ya makampuni ya bus kusimamisha safari kwenye vituo maalum vya chakula ambavyo bei zake ziko juu kupita kiasi. Abiria tunashushwa hapo kana kwamba hatuna chaguo lingine, wakati ukweli ni kwamba wengi wetu hatuna uwezo wa kumudu hizo bei.
Swali la msingi ni hili: kwa nini wamiliki wa vituo hivi wanapandisha bei kiholela ilhali wanajua kabisa hali halisi ya maisha ya Mtanzania wa kawaida? Je, huu si ni unyonyaji wa wazi kwa abiria. Mf sahani ya wali nyama Tsh 8,000/=
Mbaya zaidi, kuna mazingira yanayotengeneza kama ulazima dereva anasimama sehemu moja tu, muda wa kusimama ni mfupi, na hakuna mbadala. Hii inawanyima baadhi ya watu haki yao ya msingi ya kupata chakula kwa bei nafuu na inayofikika.
Je, mamlaka husika zinaona hili? Au kuna mahusiano ya kimaslahi kati ya makampuni ya mabasi na wamiliki wa hizi sehemu za chakula?
Natoa wito:

- Mamlaka zifuatilie na kudhibiti bei kwenye vituo hivi
- Makampuni ya mabasi yatoe uhuru wa chaguo kwa abiria
- Bei ziwe rafiki kulingana na hali ya uchumi wa nchi