Abiria wa Pugu anafuata nini kwenye SGR kama sio upigaji

BONGO
BONGO
BONGO
 
Wewe unafikiri behewa ni kama gari la mabox? Sio haraka hivyo, sema wasitishe huduma kwa vituo vya karibu mpaka hapo baadae watakapopata behewa nyingi zaidi.
Sasa hapa umetoa hoja gani zaidi ya Utopolo. Kwa hiyo Wasisafiri?
Nimeanza kusafiri na treni kabla ya Baba yako hajabalehe.
 
nikupotezeana muda tu, tuache siasa kwenye uchumi treni ya dom kituo cha kwanza kiwe moro then dom. nauli mbili tu moro na dom, lakini naona kuna shida kwenye ticketing system, iweje mtu akate ticket ya pugu na apate seat hadi moro?
Kwa utaratibu huo pia kunauwezekano mtu akakata tiketi ya moro akaenda hadi Dodoma. Mliotumia hiyo tiketi huko nyumbani Tanzania hali ipoje?
 
Kuna wakati utaratibu mdogo unaweza kuondoa tatizo kubwa
Uongozi uweke sheria ya kukagua tiketi kila baada ya umbali fulani kama wanavyofanya kwenye mabasi ya abiria,watagundua tu kuwa kuna mtu anasafiri umbali ambao hakustahili kwa gharama ambayo haistahili,ila hili la abiria wa Pugu kwenda Dodoma ni uzembe wa management umefanyika, wao ndio waulizwe,wakati hilo linatokea wao walikuwa wanafanya nini.
 
Ngoja tusafiri na hii treni ya abiria SGR kwa kupitia video hii kupata ukweli wa safari ya Express vs Simama kila kituo ktk kipande cha reli Dar es Salaam hadi Dodoma na kurudi inakuwa vipi kiuhalisia yaani upatikanaji tiketi, foleni kufika dirishani, huduma ndani ya treni, upishanaji wa treni zinazotoka sehemu tofauti n.k


View: https://m.youtube.com/watch?v=TqryCZcJAO0
 
Wanashindwa kuwa wabunifu. Watengeneza mabehewa ya Abiria wa njiani.

Na kwa treni inayoanzia Dar na kituo cha kwanza kiwe Ruvu siyo Pugu.

Shida tumejaza watu wasiofikira katika hizi Taasisi.
Sahihi kabisa
Na lisiwe na milango ya kuunganisha na mabehewa mengine
Hilo behewa likifika mpaka Moro, likaguliwe upya, na mpaka Dodoma linatakiwa kuwa tupu, watakaokutwa humo watajieleza
 
Wa pugu, soga, ruvu, ngerengere waruhusiwe tu, ila nauli iwe flat rate 13 elfu ya moro ku discourage upigaji
Umeongea la maana sawa. Waweke nauli flat kwa wanaoishia Morogoro hii itaondoa hiyo shida
 
Kama pugu Kuna umuhimu Basi waongeze mabehewa ya kuishia PUGU kuwasaidia abiria wa PUGU ""kuwasaidia""
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…