Abiria wa Pugu anafuata nini kwenye SGR kama sio upigaji

Abiria wa Pugu anafuata nini kwenye SGR kama sio upigaji

Naskia SGR wanapakia abiria hadi wa buku alafu wanapitiliza hadi dodoma

Juzi hapa kulikuwa na malalamiko abiria wa Doodma wale original na wa moro wanakosa tiketi wanaona online treni imejaa kumbe mmewapa nafasi watu wa pugu na abira wa karibu kwa bei kitonga na hao kitonga ni wahuni wanaopitiliza hadi Morogoro, Dodoma kwa elfu moj hivi hamuoni aibu?

Huu mradi msipikuwa makini mtauuwa mapema tu maana naona hii ni michezo ya wafanyakazi

Ukienda abood pale hakuna nauli ya mlandizi wala nauli ya Chalinze ukipanda gari ya mro kama nuali ni sh 13000 utalipia hiyp hiyo 13000 hakuna masihara

Ukipanda tilisho,kilimanjaro,bm za arusha kama unashukia Tanga au himo wao haiwahusu utalipa 45000 ile ile ya Arusha wanafanya hivyo kuepuka upigaji wa wafanyakazi na abiria wasio waaminifu sasa nyie sgr hamjifunzi kwa wenzenu?

Abiria wa pugu si apande daladala za gongo la mboto pugu kwenye sgr anafuata nini
BONGO
BONGO
BONGO
 
Wewe unafikiri behewa ni kama gari la mabox? Sio haraka hivyo, sema wasitishe huduma kwa vituo vya karibu mpaka hapo baadae watakapopata behewa nyingi zaidi.
Sasa hapa umetoa hoja gani zaidi ya Utopolo. Kwa hiyo Wasisafiri?
Nimeanza kusafiri na treni kabla ya Baba yako hajabalehe.
 
nikupotezeana muda tu, tuache siasa kwenye uchumi treni ya dom kituo cha kwanza kiwe moro then dom. nauli mbili tu moro na dom, lakini naona kuna shida kwenye ticketing system, iweje mtu akate ticket ya pugu na apate seat hadi moro?
Kwa utaratibu huo pia kunauwezekano mtu akakata tiketi ya moro akaenda hadi Dodoma. Mliotumia hiyo tiketi huko nyumbani Tanzania hali ipoje?
 
Kuna wakati utaratibu mdogo unaweza kuondoa tatizo kubwa
Uongozi uweke sheria ya kukagua tiketi kila baada ya umbali fulani kama wanavyofanya kwenye mabasi ya abiria,watagundua tu kuwa kuna mtu anasafiri umbali ambao hakustahili kwa gharama ambayo haistahili,ila hili la abiria wa Pugu kwenda Dodoma ni uzembe wa management umefanyika, wao ndio waulizwe,wakati hilo linatokea wao walikuwa wanafanya nini.
 
Ngoja tusafiri na hii treni ya abiria SGR kwa kupitia video hii kupata ukweli wa safari ya Express vs Simama kila kituo ktk kipande cha reli Dar es Salaam hadi Dodoma na kurudi inakuwa vipi kiuhalisia yaani upatikanaji tiketi, foleni kufika dirishani, huduma ndani ya treni, upishanaji wa treni zinazotoka sehemu tofauti n.k


View: https://m.youtube.com/watch?v=TqryCZcJAO0
 
Wanashindwa kuwa wabunifu. Watengeneza mabehewa ya Abiria wa njiani.

Na kwa treni inayoanzia Dar na kituo cha kwanza kiwe Ruvu siyo Pugu.

Shida tumejaza watu wasiofikira katika hizi Taasisi.
Sahihi kabisa
Na lisiwe na milango ya kuunganisha na mabehewa mengine
Hilo behewa likifika mpaka Moro, likaguliwe upya, na mpaka Dodoma linatakiwa kuwa tupu, watakaokutwa humo watajieleza
 
Wa pugu, soga, ruvu, ngerengere waruhusiwe tu, ila nauli iwe flat rate 13 elfu ya moro ku discourage upigaji
Umeongea la maana sawa. Waweke nauli flat kwa wanaoishia Morogoro hii itaondoa hiyo shida
 
Kuzuia mtu kushuka njiani utakua Ni uonevu maana sometimes watu hupata dharula na kuishia njiani kurudi walipotoka

Solution waweke nauli ambayo ni flat. Kama Dar to Moro ni 13k basi iwe hiyo hiyo atayeshuka njiani hiyo inakua hiari yake, atayelipa 13k ili ashukie pugu hiyo ni hiari yake
Kama pugu Kuna umuhimu Basi waongeze mabehewa ya kuishia PUGU kuwasaidia abiria wa PUGU ""kuwasaidia""
 
Back
Top Bottom