Abiria wanusurika kifo baada ya kulishwa biskuti zenye dawa za kulevya

Abiria wanusurika kifo baada ya kulishwa biskuti zenye dawa za kulevya

Natoka Tanga naludi Dar nimenunua biskuti namkaribisha mdada jirani niliekaa nae kafakamia mwanzo mpaka mwisho mpaka mimi mwenyewe nkaogopa...nasema huyu dada kaniamini nini aisee!!!
Cc wazee wa kula tunda kimasihara
[emoji2]
 
Mwanaume wa mkoan analewa biscut tu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] hv anaweza kweli kuimili mziki wa balimi
 
95628f2c8fb2c1a0b6effa976b518120

Lindi. Abiria wawili waliokuwa wakisafiri na basi la Buti la Zungu kutoka Dar es Salaam kwenda Mtwara nchini Tanzania wamenusurika kifo baada kula biskuti zinazodaiwa kuwa na dawa za kulevya wakiwa ndani ya basi hilo.

Abiria hao ni Dadi Rashid (49) ambaye ni ofisa elimu taaluma Utete wilaya ya Rufiji mkoa wa Pwani na Omary Burian (27) mfanyakazi wa bodi ya korosho Dar es Salaam.

Akizungumzia tukio hilo leo Jumatano Novemba 27, 2019, Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya Sokoine mkoani Lindi, Idrisa Chande amethibitisha kuwapokea wagonjwa hao jana usiku Jumanne wakiwa hawajitambui na kwamba wanaendelea na matibabu hospitalini hapo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Lindi, Poudence Proteus amesema amepokea taarifa hiyo na atalizungumzia baada ya uchunguzi kukamilika leo Jumatano.

Chanzo: Mwananchi

======


UPDATES:


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi Pudenciana Protas amesema tayari wameshawakamata Vijana watatu wanaodaiwa kuwapa Biskuti zinazoaminika kuwa na Dawa za kulevya abiria wawili waliosafiri nao kwenye basi la Buti la Zungu kutoka DSM kuelekea Mtwara na kisha kuwaibia vitu mbalimbali.

Vijana hao wamekamatwa wakiwa kwenye Gesti moja Lindi Mjini na tayari wapo mikononi mwa Polisi wakiendelea kuhojiwa.

"Tumewakuta na Laptop, simu walizoiba kwa abiria, mabegi, nguo za wale abiria, kadi za Bank, vyeti mbalimbali, vitabu na mbaya zaidi waliwavua viatu wale abiria tumewakuta navyo, tumewakuta pia na zile Biskuti zinazoaminika kuwa na Dawa za kulevya" -RPC LIndi

Abiria hao ni Dadi Mohamedi (49) na Omary Burian (27), wote wawili wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi 'Sokoine' kwa matibabu zaidi.
Sasa waliwashusha kwenye gari baada ya kupoteza fahamu au waliwaibia wakiwa ndani ya basi? na kama ni ndani ya basi, abiria wengine hawakuwaona?
 
😁😁😁😁😁 abiria mkarimu anakupa biscuit unapokea moyoni unawaza "dah watanzania ni wakarimu sana huwez kufa na njaa"
 
Wana bahati hawakutaturiwa marinda,tuwapongeze hao mapolice kwa kuwakamata waharifu ndani ya muda mfupi bila kurushiana risasi
 
Lakn pia Kuna watu wanapenda kushobokea mtu kwenye gari. Kuna siku nasafiri ile nimeingia tu kwenye gari saa 11 ivi. Mtu anaanza kuniuliza unaenda wap mwenzangu. Nikamjibu. Sijakaa vizur Mara unatetemeka umekuja na bodaboda Nini. Khaaa nikajifunika kanga usoni hakuona sura yangu mpaka tunaambiwa break time
 
hao waliopewa ni wadada? au basi tu utamke wadada/wanawake?
I'm responsible for only what I write not what you understand!!

Wakurupukaji na wajinga mmekuwa wengi sana humu na muda wa kupoteza kuelewesha sina.
 
Wewe
Hilo basi lilikuwa na abiri wawili tu???
Wewe huwezi hata kujiongeza sasa kama walikuwepo wawili tu hizo biskuti wamepewa na kondakta? Pia hao waliokula biskuti ni mafala kila siku tunapigiwa kelele usile kitu cha usiyemjua wao wamekula, Mimi kwenye basi huwa napokea salamu tu
 
Huu ulaji ulaji wa ovyo na kupewa vitu na mtu usiyemjua siyo mzuri hata kidogo.

Mwaka juzi nilikuwa natoka songea naja dar..gari niliyopanda iliyokuwa inapitia mtwara..gari haikujaa Sana ilikuwa inachukua na abiria wa njiani.

Tukafika tunduru Kuna binti alipanda kwa muonekano tu hakuonyesha kuwa mwenyeji wa dar..alivyopanda akakaa kwenye siti ambayo kulikuwa na mwanaume wa makamo.

Yule mwanaume alikuwa na biscut akampa yule dada..kila atakachonunua anampa yule dada. Kilichonishangaza yule binti hakuwa mtu wa kukataa ..nikawa najiuliza anajiamini vipi yule kaka Kama ni mtu mwenye nia mbaya je!..

Nilichoka baada ya kuona yule kaka anampapasa yule dada Mara amminye titi kwa kuibia..Mara amlalie begani.

Sikujua kilichozidi kuendelea huko mbeleni maana Mimi sikufika hadi ubungo na sidhani Kama yule binti alifika alipokuwa anaelekea.
 
Huu ulaji ulaji wa ovyo na kupewa vitu na mtu usiyemjua siyo mzuri hata kidogo.

Mwaka juzi nilikuwa natoka songea naja dar..gari niliyopanda iliyokuwa inapitia mtwara..gari haikujaa Sana ilikuwa inachukua na abiria wa njiani.

Tukafika tunduru Kuna binti alipanda kwa muonekano tu hakuonyesha kuwa mwenyeji wa dar..alivyopanda akakaa kwenye siti ambayo kulikuwa na mwanaume wa makamo.

Yule mwanaume alikuwa na biscut akampa yule dada..kila atakachonunua anampa yule dada. Kilichonishangaza yule binti hakuwa mtu wa kukataa ..nikawa najiuliza anajiamini vipi yule kaka Kama ni mtu mwenye nia mbaya je!..

Nilichoka baada ya kuona yule kaka anampapasa yule dada Mara amminye titi kwa kuibia..Mara amlalie begani.

Sikujua kilichozidi kuendelea huko mbeleni maana Mimi sikufika hadi ubungo na sidhani Kama yule binti alifika alipokuwa anaelekea.
Kashaliwa huyo
 
Kuna jamaa yangu alipewa juice ya kopo tena sealed, maana alifungua mwenyewe kwa madai yake, akanipigia simu akiwa magomeni kwenye daladala la kkoo ubungo.

"nimekunywa juice lkn sielewi elewi" nikamuuliza uko wapi? Hakujibu na baadae simu haikupatikana hadi nilipopata taarifa yupo hospitali amelazwa hajitambui.
Zile nasikia wanatia sumu kwenye bomba LA sindano zen wanachome kwenye kopo LA juice c unajua sindano jinsi ilivyo nyembamba,,kuna bodaboda aliibiwa kwa mtindo huo.
 
Mimi hata unipe nini, sili. Unless kama tunatumia wote na lazima kiwe kitu cha maana. (Mfano wale wa nyama choma) ukinikaribisha nakuangalia kwanza unakula weeeeee ukitikia ¾ ndio naanza kula kidogokidogo, na hapo ujue njaa imenikaba kwelikweli
sikutaka kureply lakini nimeshindwa kuvumilia. ukidhania yeye anakula na wewe ndo ule huo ni ujinga. wao wanaanza kwa kumeza disinfectant kwa hiyo hata akila hapati madhala. Kuna jamaa aliibiwa pikipiki yangu . jamaa alipuliza kemikali chumbani akaingia na yule dereva boda boda amlipe akamwambia kaa kidogo kuna kitu nafanya hapa twende sehemu nyingine dereva akalala usingizi yeye akatoka akachukua pikipiki kamuacha guest house jamaa anaamshwa na mhudumu asubuhi anataka malipo ya chumba
 
Back
Top Bottom