Statesmann
JF-Expert Member
- Jul 16, 2019
- 2,344
- 3,472
Cc wazee wa kula tunda kimasiharaNatoka Tanga naludi Dar nimenunua biskuti namkaribisha mdada jirani niliekaa nae kafakamia mwanzo mpaka mwisho mpaka mimi mwenyewe nkaogopa...nasema huyu dada kaniamini nini aisee!!!
Yani inashangaza halafu ni afisa wa elimu,Hivi unapewa kitu kwenye basi na wewe unakula tu
Ahaaaa oky kumbeeeeNamaanisha abiria mmoja kampa abiria mwengine hizo biskuti hazijagaiwa na wahudumu wa gari.
Sasa waliwashusha kwenye gari baada ya kupoteza fahamu au waliwaibia wakiwa ndani ya basi? na kama ni ndani ya basi, abiria wengine hawakuwaona?
Lindi. Abiria wawili waliokuwa wakisafiri na basi la Buti la Zungu kutoka Dar es Salaam kwenda Mtwara nchini Tanzania wamenusurika kifo baada kula biskuti zinazodaiwa kuwa na dawa za kulevya wakiwa ndani ya basi hilo.
Abiria hao ni Dadi Rashid (49) ambaye ni ofisa elimu taaluma Utete wilaya ya Rufiji mkoa wa Pwani na Omary Burian (27) mfanyakazi wa bodi ya korosho Dar es Salaam.
Akizungumzia tukio hilo leo Jumatano Novemba 27, 2019, Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya Sokoine mkoani Lindi, Idrisa Chande amethibitisha kuwapokea wagonjwa hao jana usiku Jumanne wakiwa hawajitambui na kwamba wanaendelea na matibabu hospitalini hapo.
Kamanda wa polisi mkoa wa Lindi, Poudence Proteus amesema amepokea taarifa hiyo na atalizungumzia baada ya uchunguzi kukamilika leo Jumatano.
Chanzo: Mwananchi
======
UPDATES:
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi Pudenciana Protas amesema tayari wameshawakamata Vijana watatu wanaodaiwa kuwapa Biskuti zinazoaminika kuwa na Dawa za kulevya abiria wawili waliosafiri nao kwenye basi la Buti la Zungu kutoka DSM kuelekea Mtwara na kisha kuwaibia vitu mbalimbali.
Vijana hao wamekamatwa wakiwa kwenye Gesti moja Lindi Mjini na tayari wapo mikononi mwa Polisi wakiendelea kuhojiwa.
"Tumewakuta na Laptop, simu walizoiba kwa abiria, mabegi, nguo za wale abiria, kadi za Bank, vyeti mbalimbali, vitabu na mbaya zaidi waliwavua viatu wale abiria tumewakuta navyo, tumewakuta pia na zile Biskuti zinazoaminika kuwa na Dawa za kulevya" -RPC LIndi
Abiria hao ni Dadi Mohamedi (49) na Omary Burian (27), wote wawili wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi 'Sokoine' kwa matibabu zaidi.
Saizi watakuwa wanaona aibu sanaBiscuit tu zimewatoa udenda. Sijui hali ingekuwa vipi kama wangeringishiwa nyama ya swala!
hao waliopewa ni wadada? au basi tu utamke wadada/wanawake?Wadada wanatumiwa sana siku hizi kwenye hii issue,hapo lazima hao jamaa wamepigwa simu na pesa.
I'm responsible for only what I write not what you understand!!hao waliopewa ni wadada? au basi tu utamke wadada/wanawake?
Hiii chai boss
Wewe huwezi hata kujiongeza sasa kama walikuwepo wawili tu hizo biskuti wamepewa na kondakta? Pia hao waliokula biskuti ni mafala kila siku tunapigiwa kelele usile kitu cha usiyemjua wao wamekula, Mimi kwenye basi huwa napokea salamu tuHilo basi lilikuwa na abiri wawili tu???
Hao wamepewa na abiria wenzaoHizo huduma hua zinatolewa kwa gari zima ni maji, soda, biscuit na pipi.
Iweje wapewe wa 2 tu?
Kashaliwa huyoHuu ulaji ulaji wa ovyo na kupewa vitu na mtu usiyemjua siyo mzuri hata kidogo.
Mwaka juzi nilikuwa natoka songea naja dar..gari niliyopanda iliyokuwa inapitia mtwara..gari haikujaa Sana ilikuwa inachukua na abiria wa njiani.
Tukafika tunduru Kuna binti alipanda kwa muonekano tu hakuonyesha kuwa mwenyeji wa dar..alivyopanda akakaa kwenye siti ambayo kulikuwa na mwanaume wa makamo.
Yule mwanaume alikuwa na biscut akampa yule dada..kila atakachonunua anampa yule dada. Kilichonishangaza yule binti hakuwa mtu wa kukataa ..nikawa najiuliza anajiamini vipi yule kaka Kama ni mtu mwenye nia mbaya je!..
Nilichoka baada ya kuona yule kaka anampapasa yule dada Mara amminye titi kwa kuibia..Mara amlalie begani.
Sikujua kilichozidi kuendelea huko mbeleni maana Mimi sikufika hadi ubungo na sidhani Kama yule binti alifika alipokuwa anaelekea.
Zile nasikia wanatia sumu kwenye bomba LA sindano zen wanachome kwenye kopo LA juice c unajua sindano jinsi ilivyo nyembamba,,kuna bodaboda aliibiwa kwa mtindo huo.Kuna jamaa yangu alipewa juice ya kopo tena sealed, maana alifungua mwenyewe kwa madai yake, akanipigia simu akiwa magomeni kwenye daladala la kkoo ubungo.
"nimekunywa juice lkn sielewi elewi" nikamuuliza uko wapi? Hakujibu na baadae simu haikupatikana hadi nilipopata taarifa yupo hospitali amelazwa hajitambui.
Kwakweli..maana ile mipapaso ya garini khaaa! Kuna muda nilijikuta nacheka peke yangu..Kashaliwa huyo
sikutaka kureply lakini nimeshindwa kuvumilia. ukidhania yeye anakula na wewe ndo ule huo ni ujinga. wao wanaanza kwa kumeza disinfectant kwa hiyo hata akila hapati madhala. Kuna jamaa aliibiwa pikipiki yangu . jamaa alipuliza kemikali chumbani akaingia na yule dereva boda boda amlipe akamwambia kaa kidogo kuna kitu nafanya hapa twende sehemu nyingine dereva akalala usingizi yeye akatoka akachukua pikipiki kamuacha guest house jamaa anaamshwa na mhudumu asubuhi anataka malipo ya chumbaMimi hata unipe nini, sili. Unless kama tunatumia wote na lazima kiwe kitu cha maana. (Mfano wale wa nyama choma) ukinikaribisha nakuangalia kwanza unakula weeeeee ukitikia ¾ ndio naanza kula kidogokidogo, na hapo ujue njaa imenikaba kwelikweli