Absalom Kibanda: Kilichobaki ni Kuandika kitabu cha Maovu yako Samwel Sitta!

naunga mkono hoja yako siasa ni mchezo wa ajabu sana,chadema kuna kitu wanavizia hapo haiwezekani kibanda apate ujasiri wa kumsafisha lowasa mbowe asimuite na kumkanya, kuna kitu.
 
Mkuu kula tano,
Tatizo watu hawawaelewi wanafiki hawa, walikuwa wanatumia hoja ya ufisadi kama mtaji wa kisiasa.
Ilipokuwa inatakiwa kufanya maamuzi muhimu kuumaliza huo ufisadi ndani ya bunge kama chombo cha kutunga na kusimamia sheria, wali side na hao mafisadi. Wakija majukwaani kwa wajinga wao, wanatoa mapovu kujidai wanaumizwa na wanauchungu na nchi,sio yeye aliyetukana wapinzani wakati wa uchaguzi au mmesahau?
 
Kwanini alizima sakata la Richmond kihuni? Wacha achambuliwe kama karanga. Yeye na EL,RA,AC na wengine ni janga la kitaifa, hata ikibidi kuuwawa wauawe tu hawana faida yoyote kwa nchi yetu.

Kuhusu hili la kuuzima moto wa richmond ambao kiukweli bado tulikua na kazi nao aliwakera wengi mpaka reginald mengi ambae pia alikua nyuma yake alikasirika sana na nasikia mpaka akawaagiza wahariri wake wasimpe tena sitta coverage kwenye vyombo vyake vya habari,na hata sijui kama uswahiba wao umerejea katika hali ya kawaida,mengi alichukia sana inasemekana.Lakini kama mnavyojua shinikizo lilikua kubwa sana ndani ya ccm kipindi kile ambamo mafisadi walikua na nguvu kubwa mno wakati ule,na kama si jitihada na busara za wajumbe wawili wa kamati kuu bwana ABDULRAHMAN KINANA na BERNARD MEMBE,Sam six ilikua avuliwe uanachama,lakini wawili hao na hasa kinana ambae alionekana kama hana upande alisimama kidete kumtetea spika na kuwaeleza wazi wazi wajumbe wa kamati kuu akiwemo mwenyekiti kwamba spika hana matatizo yeyote anafanya kazi yake na kiukweli anakisaidia chama ambacho kimechafuka..ndio akaponea kwenye tundu la sindano na kupewa masharti ya kuuzima huo mjadala bungeni kwa kuwa unakichafua chama na serikali yake,hapa ndipo alipokosea mzee wangu huyu,hakutakiwa kuyumba kwani tayari alikua na base kubwa ya wabunge na sisi wananchi kiujumla,lakini akaufyata mkia ndani ya ccm lakini bado alikua na uchungu ndio maana mkawa mnasikia habari za CCJ zikipamba moto kwa kasi,ni kweli sitta na wenzake walipanga kujionadoa kwenye chama kama udhibiti dhidi yao kama wapambanaji wa ufisadi utaendelea na hasa kama jk atamrudisha Ngonyani Lowassa serikalini (mpango ambao alikua nao kweli),lakini lowassa hajarudi serikalini mpaka leo na wao nadhani baadae wakaona hakuna haja ya kujitoa badala yake wapambane na mafisadi goi goi wakiwa humo humo ili kama ikibidi mafisadi ndio waondoke...matokeo yake ndio hii issue ya kujivua magamba japo inaonekana kukwama kutokana na udhaifu wa mwenyekiti na pia hujuma za mafisadi.Lakini habari ya ccj ama kujiunga na chadema vyote vilikuwepo na vikao vya kina sitta na viongozi wa chadema na ccj vilishika hatamu sana kipindi hicho,mh.mboe kama anaingia na kusoma haya atakua anaelewa nazungumzia nini,sitts ndio alikua awe mgombea urais wa chadema badala ya slaa kwa msiojua,na hasira za chadema kwa sitta na huu wimbo wa usaliti wa sitta unaoimbwa hapa ni kutokana na tukio la sitta kuwatosa chadema dakika za mwisho,ikabidi wamtafute mgombea wa fasta bwana slaa,ambae hata hivyo kwa muda ule uliobaki alifanya vizuri,nampongeza kiukweli kwa kuwa alitokeo from no where na kutikisa,kama angekua sitta angemshinda jk kwa wakati ule,alikua juu mno.
 

Kibanda kaka wabongo wa leo sio wa zamani,kuna watu wanakufuatilia nyendo zako kila unapotia mguu kwenye ofisi au vikao haramu vya mafisadi,simu mnazopigiana na Rostam na Lowassa and everything,we are watching u brother,kwani nani asiejua ukaribu wako wewe na Rostam?!!siku ile Rostama alipochemka(ingawa sasa inaonekana alikua right)kumponda yule babu wa loliondo na tiba zake jukwaani Igunga ni nani alie,pigia simu Rostam kumshtua kwamba amechemka kwa kauli ile kwani itamharibia wa wananchi na kumshauri awaagize kina Bashe na genge lake pale habari cooperation waipake rangi ile kauli ya bwana mkubwa ni nani???????????????
 

Eeeeh! eeeeh eeeh mkuu pande hizo na mimi unihusishe,hawa wahariri wengi kwenye angle hiyo ni mafisadi papa,ntatoa mchango wangu wa kile ninachokijua tena kwa ushahidi,namstahi tu mkubwa mwenzangu huyu lakini likipatikana jukwaa la kumuweka hadharani na mimi ntalipanda!
 

"hakuna hata mmoja mwenye ubavu wa kumnyoshea mwenzake kidole". WADAU MNAIKUMBUKA HII KAULI?NADHANI SI MALA YA KWANZA KUISIKIA KUTOKA KWA KAMANDA KIBANDA,KAULI HII HII ALIITUMIA NGONYANI LOWASSA SIKU ALIPOAMBIWA NA DK.MWAKYEMBE "APIME"

Kiufupi bwana kibanda hata kama sitta alikua kwenye hilo kundi,ilikua ni kwa malengo ya kuleta maisha bora kwa kila mtanzania,lakini badae akaona wenzake wamebadilisha kimya kimya hiyo kauli mbiu na wengi wakawa wanajishughulisha na maisha bora kwa kila mwanafamilia wao,hapa ntawagonga ridhiwani na swahiba wako bwana kibanda,kaka Fred Lowassa,nadhani ndio maana sitta akaamua kuwa muasi kwa ajili yetu tupate maisha bora,hii unasemaje?
 

...Duh kwahiyo ugomvi wako na Sitta ni kwa sababu tu Sitta ameamua sasa kupambana na ufisadi wa akina Lowassa na Rostam?naona bila chenga unazidi kudhibitisha ukweli wa maneno ya Sitta, .....Umesha-Chuka-Chako-Mapemaaa.

Lakini siku zote ukumbuke kuwa heshima ya kalamu ni umakini na uadilifu, ukishazipoteza hizo sifa tegemea kuishi kipambepambe maisha yako yoote utakayokuwa kwenye hii fani, mie nilishaacha kitambo kusoma makala zako, kadri unavyozidi kuuza ufahamu wako na makala zako zinatoka kwenye uchambuzi na kuelekea kwenye udaku, kalaghabao...
 
Mpayukaji siujui ufisadi wa Sitta sasa sijui nitauandikaje? Kusudi langu ni kuandika tafsiri yangu ya mapambano ya ufisadi ya akina Sitta na wanafiki wengine CCM wanaojiita wapambanani ilhali wakiwa na malengo mengine

Sasa kama wao ni wanafiki, wewe sijui tukuweke kwenye kundi gani?labda mganga njaa litakuwa sahihi zaidi.
 

This is Non sense!!! ufisadi wa ndoa unatuhusu nini waTz. Tunajadili mambo yenye maslahi kwa taifa wewe unaleta mambo ya magazeti ya udaku?
Nenda kampelekee Shigongo, sio kuleta upuuzi hapa jamvini.
 

Mkuu mi nadhani sasa usijibu tena. tunaumizana bure kwa maneno na kitabu chenyewe hakijatoka. tusubiri utoe kitabu ndipo tujadiliane objectively. wasiwasi na hisia za zetu sote zitathibitika kama ni kweli au ni uongo.
 

Hakika nimepata picha kuwa kama kitabu hicho kitamhusu SITA hata kwa kutaja jina lake ndani ya kitabu hicho NI DHAHILI UTAKUWA UMETUMWA N A HAO AMBAO WATU WATU WENGI HUMU NDANI WAMEKUWA WAKIPIGA KELELE KUKUSULUBU, NIKAJIKITA KUKUPA NAFASI KUKUTETEA NA NIKAKINGA KUSEMA UNA HAKI YAKO KUITUMIA KUSEMA YALE UNAYOYAJUA KUHUSU SAKATA LA RICHMOND NA DADA YAKE DOWANS.

Ulipojitokeza nimefuatilia mazungumzo yako nimegundua kuwa UNASTAHIKI KUHUKUMIWA HATA KABLA UJATEKELEZA DHAMILA AU ADHIMA YAKO KWA KUWA TAYARI UMEDHIHILI KUWA UMETUMWA TENA MBAYA UMETUMWA NA MAFISADI.

Nilitegemea kuwa wewe ni Muungwana sana kupitia kanusho lako la awari, ajabu umegeuka ghafla na kufanya madudu, ambayo sikutegemea uyafanye kama mtu mwenye ufahamu mkubwa kama wako wa mhariri wa chombo cha habari,kwa kuwa ni mwandishi ambae unafahamu ubaya na uwezo wa kauri kutoa maana au kupotosha maana kwenye jamii.

Wenye akili zao wamejaribu kukuprovoke na kweli wamefanikiwa kujua msimamo wako,unajua kuwa mchezo uliochezwa na NTAMBASWALA Umefumua UKWELI HATA KABLA WINO WA KWANZA WA KITABU CHAKO AUJAFANYA KAZI,Naungana lasmi na wengineo kuwa UMETUMWA HIVYO MIMI BINAFSI UMEDHIHILISHA KUWA UMESHINDWA HATA KABLA UJAANZA [IT END BEFORE IT START] yaani imeisha hata kabla aijaanza.

ULIPODHIHIRISHA KUWA UMETUMWA ni baada ya kauri ya huyu jamaa Ntambaswala Na wewe Kibanda pasipo busara umefanya kosa la Msingi [Technical Mistake] umejisahau kiasi kuwa umejibu kana kwamba UNAJUA KWA USAHIHI PERSONAL LIFE YA SITA LAKINI AWALI UMEKENUSHA KUZUNGUMZIA PERSONAL LIFE YA SITA KWENYE KITABU.Tizama ulivyojikaanga kwenye Red kuonyesha upofu wako kuwa umejisahau kiasi kuwa UMEMSHAMBULIA DHAHILI HATA KABLA UJASHIKA KALAMU YAKO KUANZA KUTUNGA KITABU HICHO.

Watu wanapokosa hoja ........ Pengine fisadi kinara wa ndoa ni huyo mnayejaribu kumtetea hapa hata kufikia hatua ya kunisingizia kwamba nataka kumuandikia kitabu. Dhamira yangu....................i
.Nimevaa viatu vya Ntambaswala,nikajiona wewe unavyonishambulia mimi, ambae ni raia wa kawaida nisie fahamina na SITA,na kuwa niko ndani ya jamiiforum ama kushabikia upande wa Mafisadi, au kushabikia Upande wa Wapinga Mafisadi au Kusimia Ukweli unaojisimamia wenyewe pasipo kujali kundi, kisha wewe Kibanda unanipa jibu tajwa hapo juu.Hakika kibanda IMEKULA KWAKO POLE SANA KWA KUWA KWA AINA YA SISI WATAFUTA UKWELI UMENIAIBISHA SANA, UMENISIKITISHA SANA, UMENIFEDHEHESHA SANA NAKUCHUKUA FULSA HII KUMUOMBA MSAMAHA MKUU LINCOLNTZ.Samahani Mkuu LincornTz hakika sijaona utumbo ndani ya JF kama huu,manake uliniambia hapo chini nami nikakuplease nikitumainia huyu jamaa ni Mhariri hivyo ni mtu mwelewe na mwenye mwanga wa kujua matatizo mazito tuliyonayo ndani ya Taifa,kumbe ni wale Rais Jakaya Kikwete aliwabatiza jina la Makanjanja [bogas].

 
itakua ngumu kutushikia chini. Huwezi kumchafua yule mzee mbona itakua ngumu.
 
 

ROMANTIC, ru a male or female?! Kama ni male, plz isije ikawa ni kisasi cha kulipiza kuchukuliwa demu wako; na kama ni female isije ikawa jamaa alikopa ndo unataka kulipiza hapa....malizianeni huko huko bana! LOL!
 

KWANGU mimi, Samwel Sitta, Mwakyembe, Mengi na Kibanda wote ni wanafiki wa kutupwa! Hata hivyo, lazima nikiri kwamba unafiki wa Kibanda ndo nimeugundua sasa! I will explain:
1. Sitta na Mwakyembe; hawa ni political opprtunists tu hakuna lolote zaidi ya kujifanya wanapigana vita dhidi ya ufisadi lakini kimsingi ni kwa malengo yao binfsi hususani kwa huyu Sitta. Ni ngumu sana kuwaelewa watu hawa, labda nitoe hadithi moja iliyo kwenye imani ya waislamu( waniwie radhi wale wasio waislamu).
Kulikuwa na mwanazuoni mmoja (wa kiislamu) ambae alikuwa ni mtu wa ibada sana. Na ilikuwa kila anaposali, alikuwa anamlaani shetani mara 1000; hii manake ni kwamba, minimum alikuwa anamlaani shetani mara 5000 kwa siku (sala 5). Siku moja mwanazuoni huyu akawa anasafiri na kama tujuavyo, zamani hapakuwa na usafiri huu wa sasa. Baada ya kutembea umbali mrefu porini, akawa amechoka sana hivyo akaamua kujiegemeza kwenye mti mmoja na hapohapo akapitiwa na usingizi. Akiwa katikati ya usingizi, mara akaja mtu mmoja na kumwamsha na kumwambia afanye haraka kutoka kwani mti ulikuwa unaanguka. Na kweli, ile kutoka tu ule mti ukadondokea upande ule ule aliokua amelala yule mwanazuoni. Kuona hivyo, yule mwanazuoni akamshukuru sana yule na kuanza kumwombea dua kadhaa wa kadhaa kwa mwenyezi mungu! Baada ya kumwombea dua zile na kumtakia heri kwa mwenyezi mungu; ndipo yule mwanazuoni akamwuliza yule "mwokozi wake ni nani". Yule mwokozi akajibu, mimi ni yule shetani ambae kila unapofanya ibada kwa mungu wako huwa unanilaani mara 1000! Yule mwanazuoni akashangaa, na akataka kufahamu ni kwanini ameamua kumnusuru na kifo wakati anajua yeye ni adui yake! Shetani akajibu "Nimelazimika kukuokoa kabla ya kifo kwavile nimechelea ungekufa ukiwa shahidi!! Huyo ndie Samwel Sitta na Mwakyembe wake!!!!

2. Reginald Mengi nae ni miongoni mwa wanafiki wengine walio kwenye vita dhidi ya ufiisadi. Kwenye grand/political corruptions, two sides za corrupt people lazima zihusike. Hizi sides ni Business People in one side and Politicians/gvt executives in other side. Huyu babu (R. Mengi), kila linapokuja suala la ufisadi, yeye kila siku anataja one side(business people) na kuacha kutaja upande wa wanasiasa. Kwangu mimi, huu ni unafiki ninaoona ni vita vya kibiashara zaidi kuliko za kifisadi hata kama anachozungumzia ni ufisadi. hana tofauti yoyote na shetani aliyemnusuru kifo mwanazuoni ambae ingekuwa rahisi kuzani kamnusuru kumbe hakutaka kufa akiwa shahidi. Nitaanza kum-support huyu mzee atakapoanza kuwafanyizia na corrupts politicians na sio kuishia kwa akina Manji na Rostam pekee.

3. Kibanda: Huyu nae kwa sasa namuona ni mnafiki mwingine sawa na akina Sitta na Mzee Mengi. Ina maana unafiki wa Sitta ameuona sasa wakati watu wadogo kama sisi tu tulishauona tangu kitambo? WHY now? Kwavile amewageuka CHADEMA?! Sio Siri, hivi sasa Sitta ananuka kwa wana magwanda wote kwavile hivi sasa haongei lugha ya CHADEMA. Kumwandika Sitta, yeye binafsi au kambi yake ni unafiki uliovuka mipaka ikiwa uandikaji huo unatokana na hivi sasa Sitta kutoongea lugha mnayoipenda. By the way, kwa respected journalist kama Kibanda kuandika in favor of politicians ni jambo la aibu na kutia kinyaa kama sio kuichafua tasnia ya habari. Awe ametumwa na akina Lowassa, au Mbowe; yote ni matusi na kejeli kwa tasnia inayoheshimika kama tasnia ya habari. Kuna kila dalili kwamba, uandishi wa kitabu hicho(dhidi ya akina Sitta) hautokani na dhamira ya mwandishi mwenyewe-- na kama ni dhamira ya mwandishi mwenyewe basi ina lengo la kumfurahisha Mbowe ambae amegeukwa na Sitta.
 

Kwani hapa kisichoeleweka ni nini? Kwanini mnataka Kibanda aandike kuhusu watu mnaowataka nyie? Yeye kaamua kuandika kitabu kuhusu Sitta labda ndiye anamfahamu vizuri na weakness zake, si tusubiri aandike tuone ushahidi alionao juu ya tuhuma za Sitta? uzuri wa maandishi hayafutiki. Wengine wataandika kuhusu hao wengine kadri walivyokusanya data zao. Lakini ugomvi wa Sitta na Kibanda mnaujua au mnarukia tu mada? Nyie tulieni baada ya mechi mtatoa comment zenu.
 

Sisi wengine tutasoma kitabu hicho! Go Kibanda...go Kibanda dont give up! We need to know the true colours of this man!
 
Hata kama Sitta ni mchafu lakini bado hajaanza kunuka. Lowassa na RA ni wachafu kiasi cha sabuni nazo kuogopa kuwasafisha kwa kuogopa kuchafuka.

Hivi nyie vijana mnamjua Sitta au mmeanza tu kumsikia hapa majuzi akiwa Spika ! Sisi tuliomfahamu toka akiwa Waziri, akiwa CDA hadi kuongoza kituo cha Uwekezaji...mmh, ngoja tunyamaze. Hawa ndio wanafiki wenyewe ndani ya serikali dhalimu ya CCM wanaotumiwa katika kuuma na kupuliza. Of all the people Sitta ! Come on give me a break !
 
ROMANTIC, ru a male or female?! Kama ni male, plz isije ikawa ni kisasi cha kulipiza kuchukuliwa demu wako; na kama ni female isije ikawa jamaa alikopa ndo unataka kulipiza hapa....malizianeni huko huko bana! LOL!

Hata,kila kitu hapa hapa jukwaani tu si unajua mimi siwezi kupanda lile jukwaa lao wahariri ambalo jama ni boss kule,mi tutakutana hapa hapa kwenye jukwaa huru,mambo hadharani tufiche nini na sie watu wazima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…