DOKEZO Achana na kunguni, UDOM ina vyoo vichafu sijawahi kuona

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Dokta tulia amekuambia utulie kijana swala la vyoo hata yeye wakati anafundisha alikuwa analijua
 
Basi hapo tatizo sio wanafunzi tatizo hapo ni UONGOZI wa Chuo, JamiiForums emu na hii habari iende viral yule mama ajibu na hili
 
Hilo suala sio la watanzania, ushaelewa hilo suala ni la uongozi wa Chuo wameajiri watu wa kufanya usafi wa vyoo kwanini vyoo vinakua vichafu, unasemaje watanzania kufanyaje?
Naifahamu UDOM ya miaka ile, sijui ya sasa.

Nilishaishi pale kwa miaka mitatu, zaidi ya miaka kumi iliyopita.

Kulikuwa na wafanya usafi wa kampuni iliyopewa mkataba wa kutoa huduma ya usafi. Pamoja na kuwa walikuwa wanafanya usafi kila siku, bado vyoo bilikuwa vikichafuliwa.

Tatizo lipo kwa "Watanzania"

Hivi unafikiri wangeondolewa Watanzania wote na Waafrika wote hapo UDOM, halafu wakawekwa Wazungu badala yake, unafikiri tatizo la uchafu lingeendelea kuwepo?
 
Lichuo likubwa lenye eneo kubwa hivyo na vyoo vingi wanashindwa kuvihudumia na si ajabu havitumiki sana maana ni vingi ila ni uchafu tu.

Vyuo vidogo kama IFM(dar) na TIA(dar) vyoo vyao wanajitahidi mno. Pamoja na ule udogo wa chuo, wingi wa wanafunzi zaidi ya eneo lakini vyoo mda mwingi ni visafi na maji yapo vyooni 24/7.
 
Mwanzo umejibu vizuri Sasa hivi unajibu ovyo nimekwambia tembea tembea tembea kuna vyuo ukipelekwa chooni utaduwaa choo kilivyopendeza Sanitizer zimejaa ukimaliza unaosha mikono shwaa unaenda, umesema wa huko youdom inabidi watembezwe vyuo vingine wajifunze hapa ndio ukisema la maana, Mimi nasemaje uongozi ndio una shida, kuna Chuo kimoja nilianzisha varangati suala la maji nikaanza kuchunguzwa Mimi ni nani mboni nataka kumletea msala mkuu wa Chuo
 
Maji kisimani wanashindwa kuweka tank kubwa juu wanafunga motor wakasupply maji vyooni, nilitoa hili wazo Chuo fulani wakalifanyia kazi Mambo yakawa mazuri ingawa nilikosana na mkuu wa Chuo, weka tank juu kwenye kila sehemu ya choo vuta mipira ya maji kutoka kwenye kisima funga motor pandisha maji kwenye matank mboni vyuo vingine wanafanya hivi Youdom wanashindwa nini?

Jibu swali Youdom wanashindwa nini kupandisha maji kwenye matank na kufunga motor za kusupply kwani wanafunzi si wanalipa Ada au wanasoma bure?
 
Dah,vyoo mchafue wenyewe,halafu lawama muipe serikali!maajabu
 
Dah,vyoo mchafue wenyewe,halafu lawama muipe serikali!maajabu
Wewe unaonekana hata Chuo hujafika, hujui unachokisema

Pesa za ada wanazolipa kuna fungu linakatwa kwa ajili ya usafi moja ya usafi ni usafi wa vyoo na vyoo haviwezi kua safi km miundombinu ya maji ni mibovu maji ya shida wanachota kwenye visima mtu anahangaika na kindoo Cha maji akakate gogo wakati somewhere kuna wenzao maji yapo bafuni na vyooni ni suala la kubinyeza koki tu, kwa hio lazima wahoji usiwe zuzu
 
Dah,vyoo mchafue wenyewe,halafu lawama muipe serikali!maajabu
Nenda NIT hapo ukifika waambie wakuelekeze Chooni ukashangae kidogo vyoo vilivyo visafi km wanafunzi hawaingii chooni maana hamuelewi mpaka muone
 
Nenda NIT hapo ukifika waambie wakuelekeze Chooni ukashangae kidogo vyoo vilivyo visafi km wanafunzi hawaingii chooni maana hamuelewi mpaka muone
Aaah mi nikakague vyoo vya kazi gani?huko UDOM mjitafakari,mara kunguni mara vyoo vichafu
 
Basi hapo tatizo sio wanafunzi tatizo hapo ni UONGOZI wa Chuo, JamiiForums emu na hii habari iende viral yule mama ajibu na hili
Simply waweke maji
Na pia wanafunzi waache upumbavu wa kuchafua vyoo,, kukosa maji isiwe kisingizio Cha kuchafua hovyo.

Ni kweli kuvuta maji kisimani ni kazi inayokera ila ndio hivyo,, Kwa ajili ya Afya yako lazima ukavute tu.


Maji vyooni hayapo, na semester nzima naweza kuisha, maji hayajawahi toka bombani.. hili lipo wazi.
 
Aaah mi nikakague vyoo vya kazi gani?huko UDOM mjitafakari,mara kunguni mara vyoo vichafu
Nimekwambia hauelewi mpaka uone, usiseme wanalaumu Ila waone wajifunze mboni vyuo vingine kuna vyoo visafi na wanafunzi hawalalamikii?
 
Youdom ipo wapi Somalia au Sudan? Mboni vyuo vingine vina vyoo visafi?
Kwa sababu kuna maji

Udom maji hakuna,, hadi ukasombelee kisimani.

Lakini kwani kusombelea maji kisimani ndio kunampa mtu authority ya kushusha limzigo lake Bila maji?
Ni ujasiri wa hali ya juu sana.
 
Uko sahihi hata vingi vya public ni vichafu ustaarabu na ushamba pia
Vyoo vya wanawake ndo mtihani ukiwa unasafiri ptuuuuuuu...
 
Uko sahihi hata vingi vya public ni vichafu ustaarabu na ushamba pia
Vyoo vya wanawake ndo mtihani ukiwa unasafiri ptuuuuuuu...
 
Sio baadhi ni majority wachafu mbwa.
 
Unachoongea sio masihara,nilienda Kondoa Mmang'ati katoka chooni naingia nakuta zigo hinhaa...we nkapiga kelele ,mwenye gesti alikua karibu akaja fastaaaa....akaniambia "shhhhhhhhh Hawa hawajui vyoo vya sink kaa kimya nshawazoea Hawa wateja Wangu wa maporini Huko"akanielekeza choo kingine kile akaenda safisha mwenyewe
Ni mfano ila mmekuelewa na uko sahihi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…