Acheni kumlaumu Rais Samia. Mafuta yamepanda bei katika soko la Dunia, ulizeni bei za mafuta Kenya, Uganda, Rwanda zipoje

Acheni kumlaumu Rais Samia. Mafuta yamepanda bei katika soko la Dunia, ulizeni bei za mafuta Kenya, Uganda, Rwanda zipoje

Ahlan wa Sahlan

Habari zenu wana JF:

Kumekuwa na tabia ya upotoshaji inayoendelea hapa nchini kwa watu kumlaumu rais kwa hali ya kupanda kwa gharama za maisha inavyoendelea kila kukicha, kubwa ni hili la kupanda kwa gharama za mafuta ya petroleum, diesel na mafuta ya taa.

Bei ya mafuta kwa nchi zisizozalisha mafuta zimepanda kwa kiasi kikubwa duniani kote. Pigieni simu watu wa Nairobi, Mombasa, Kisumu, Kampala , Lusaka, Kigali n.k muwaulize bei za mafuta zipoje.

Tembeleeni hii tovuti mjionee bei za mafuta duniani.

Upo sahihi, ni dunia nzima kama ambavyo ilivyokuwa korona! Kila nchi sasa hivi inaonja makali!
 
Ahlan wa Sahlan

Habari zenu wana JF:

Kumekuwa na tabia ya upotoshaji inayoendelea hapa nchini kwa watu kumlaumu rais kwa hali ya kupanda kwa gharama za maisha inavyoendelea kila kukicha, kubwa ni hili la kupanda kwa gharama za mafuta ya petroleum, diesel na mafuta ya taa.

Bei ya mafuta kwa nchi zisizozalisha mafuta zimepanda kwa kiasi kikubwa duniani kote. Pigieni simu watu wa Nairobi, Mombasa, Kisumu, Kampala , Lusaka, Kigali n.k muwaulize bei za mafuta zipoje.

Tembeleeni hii tovuti mjionee bei za mafuta duniani.

Halaumiwi kama unavyosema...Anaupiga mwingi. Umemwagika. Kwanini tuseme wakati anaupiga mwingi, unapomwagika tukae kimya?
Tusikope tu kununua mafuta
 
Ule unafiki tuliokuwa tuna uweka tuweke Sasa pia mwendazake kala sana hii inchi
 
FidQ alisema hielewe mitaa hapo ndo utajua ni nzeji ndo alitolea chupa langoma
 
Usihangaike nao hao fala achana nao ,mbona wasilete mafuta yao wayauze bei ya Chini?

Eti wanataka Serikali ifute Kodi kwenye mafuta Ili ijiendeshaje? Ili isijenge barabara?

Hakuna pimbi atafanya hili.
Nishati ni moja ya visababishi vya inflation kwenye bidhaa hapa panahitaji umakini sio matusi vinginevyo panaweza pakaleta shida.

Ni vema serikali ingeangalia sehemu nyingine ikahamishia huu mzigo wa kodi inayotoza kwenye mafuta huko ili kupunguza ukali wa maisha.

Hili jambo linamadhara makubwa kama lisipodhibitiwa.Tumezoea kwa umbali wa kawaida bodaboda ni 1000 lakini tunapoelekea bodaboda kianzio kitakuwa 2000,ni wangapi watamudu haya malipo?vipi hesabu ya bosi kwa bodaboda itapatikana?Usalama wa hii ajira ya bodaboda ambayo imeajiri kundi kubwa la vijana ukoje?
Mifano ni mengi ya madhara ya kupanda kwa bei ya nishati kwenye mnyororo wa usafirishaji.

kimsingi usifananishe madhara ya kupanda kwa mafuta ya kupikia na madhara yatokanayo na kupanda kwa dizeli na petroli ni vitu viwili tofauti.

Mnaweza waona watanzania ni watu waoga lakini usicheze na ugumu wa maisha,ni rahisi watu wakaingia barabarani kuandamana kushinikiza mabadiliko ya uongozi.
 
Watanganyika tusipokua makini tutafanywa mafukara na awamu hii.
Teh teh,ni awamu ipi tangu tupate uhuru watanzania wamekuwa wakila
Pipi...
Awamu zote ni malalamiko tu
Mwimbo unaopigwa ni huo huo

Mzee nchi hii wanaokula na kufaidika
Ni wachache....
Nchi hii kutesa kwa zamu

Ova
 
Zitto Kabwe ametowa ushauri mzuri na unatekelezeka kama kuna utashi.

Serikali ibebe huu msalaba kwa kuondowa sh 500 za tozo kwa kila litter ili wananchi wapumuwe.
Mama anawashauri wake ambao nahisi hawamshauri vizuri, hii mbona ni rahisi tu, kwa kipindi hiki Serikali ikubali isichukue tozo yoyote kwenye mafuta, mbona tozo zipo nyingi ambazo huingizia mapato Serikali?

Huyu Mama akiendelea kushauriwa na hao Walamba asali, ategemee upinzani mkubwa sana 2025, Mimi itakuwa mara yangu ya Kwanza kupiga kura ya Rais kwenda upinzani, Miaka ya nyuma Wapinzani nilikuwa nawapa kura ya Ubunge au Udiwani tu.
 
Usihangaike nao hao fala achana nao ,mbona wasilete mafuta yao wayauze bei ya Chini?

Eti wanataka Serikali ifute Kodi kwenye mafuta Ili ijiendeshaje? Ili isijenge barabara?

Hakuna pimbi atafanya hili.
Acha kuwa mpuuzi Zanzibar hapo tu petrol ni 2600 wao wako na visima??.

Kazi ya serikali sio kumnyonya raia Bali ni kumrahisishia vitu viwe himilivu!!. Huwa mnakunywa pombe gani za hovyoo hizi?.
 
Acha kuwa mpuuzi Zanzibar hapo tu petrol ni 2600 wao wako na visima??.

Kazi ya serikali sio kumnyonya raia Bali ni kumrahisishia vitu viwe himilivu!!. Huwa mnakunywa pombe gani za hovyoo hizi?.
Kalete mafuta yako uuze bei ya 2600
 
Mafuta yamepanda sababu ya wingi wa kodi. Apunguze utitiri wa kodi kwenye mafuta
 
Mafuta yamepanda sababu ya wingi wa kodi. Apunguze utitiri wa kodi kwenye mafuta
Samia ndio aliziweka hizo Kodi?

Na huko kwingine kuna utitiri wa Kodi?👇

20220507_122014.jpg
 
Ili na miradi iende likizo kusudi wewe ununue mafuta bei ya chini sio?

Unajua Kodi za kwenye mafuta zinafanya Kazi gani?
Dhibiti ufisadi na upigaji kwa hatua kali za mfano fisadi akamsimulie mama yake,bila kudhibiti ufisadi kukusanya kodi kutakuwa bure.
Kodi inapokuwa chini uchochea ukuaji wa uchumi kwa maana utakusanya zaidi.
Soda ikiwa bei chini watu wataigeuza maji watamudu wengi kununua utapata kodi zaidi.Kadri bei inavyokuwa juu zaidi ndivyo wanunuzi upungua na makusanyo ya kodi upungua pia.
 
Ufisadi upo ila haifiki hata 10% ya makusanyo which is insignificant ..

Hapo kwenye kukusanya Kodi kuna uzembe mkubwa,pesa nyingi inapotea kwa kutokusanywa na kutoingiza vyanzo vipya vya mapato.
 
Back
Top Bottom