Acheni kupotosha alichokuwa amesema Tundu Lissu kuhusu Acacia na MIGA

Huwa nashangaa sana watu wanaoiona ACACIA kuwa ni tofauti na BARRICK GOLD. ni Barrick walioanzisha kampuni tanzu ya ACACIA ikiwa ni namna ya kushughulika na nchi zetu za kimagumashi, na viongozi magumashi. Nyerere mwenye akili aliwaambia kabisa mapema kwamba subirini kwanza, tujipange kama nchi. uroho wa Mkapa ukatuingiza kichwa kichwa. PAPARA ZA MAGUFULI NAZO ZIKATUTOA MATAKO MATAKO.
Barrick anaonesha kidole kwa ACACIA kwamba ndiyo mtoto mkorofi, wakati yeye ni msikivu na mtiifu!!! Barrick ni wazoefu sana wa kupora mali kama hizi kwa miaka nenda miaka rudi.
Hata hii habari ya kampuni ya pamoja na hisa 16%, subiri kwanza uone je tutapata kitu? nina mashaka sana tutaambulia propaganda tu.
 
Kuna mahali niliposema Lissu alisema serikali itishie kujitoa?! Halafu acheni porojo za kwamba eti serikali ilikuwa na lengo fulani ndo maana ikakubali kuchukua USD 300M.... hizo ni POROJO! In short, serikali ilichemka, na hawakuwa na namna zaidi ya kuchukua hizo 300M!
 
Rubbish
 
Lakini tukijitoa huko MIGA siyo kwamba ndo tunawafukuza hao wawekezaji....


Ni nani yuko tayari kupeleka mtaji wake sehemu ambayo hata uhakika wa kuuchukua haupo...!

Tatizo la msingi katika nchi yetu sio ubovu wa wawekezaji bali ubovu wetu watanzania kwa kutanguliza maslahi binafsi dhidi ya taifa, Harvard hata sisi tumepeleka watu wetu lakini mbona hawafanyi makubwa, jibu wanarudi wanafikia kwenye mikono michafu ya wanasiasa matokeo yake wanageuka mazimwi manyonya damu .
 
Yaani hilo la kwamba Acacia zamani ilikuwa inaitwa African Barrick Gold... baadae wakabadili jina ndo wakaitwa Acacia lakini ni wale wale tu... nishasema sana hapa!! Ajabu, kuna watu wanaamini Acacia ni shetani na Barrick ni malaika!!
 


Ngoja nikwambie kitu mkuu,
Unajua kwamba mtu anaweza akawa anazo HOJA za msingi kabisa katika jambo fulani lakini tatizo kubwa likawa ni jinsi gani huyo mtu anawasilisha hizo hoja zake kwa wahusika?

Ni sawa tu na mtu anayo story nzuri yenye mafunzo mengi/vichekesho vingi,lakini tatizo lake hajui jinsi ya kuiwasilisha kwa ufasaha hiyo story mbele ya hadhira yake ili watu wajifunze kweli/wacheke kweli kweli kama alivyotaka yeye.


Utaona kwamba jamaa alishindwa hapo hata kama alikuwa nazo kweli hoja zilizokuja kufanyiwa kazi mbeleni,
Mtu mwerevu anajua jinsi ya kuwasilisha hoja zake smartly na lengo lake kutimia bila kuleta mambo ya sijui rubbish na majigambo mengine ya kijinga tu,ambayo yatawafanya wengine wakuone mpuuzi tu hata kama kweli unazo hoja za msingi.
 
Watu wanapeleka mitaji maeneo ya vita, ije kuwa nchi ambayo imejitoa MIGA! Na haya mambo muhimu kwa wawekezaji sio hii mikataba ya MIGA bali uongozi uliopo madarakani!!

Nchi inaweza isiwe mwanachama wa MIGA sio kwa sababu ya kutaka ukorofi dhidi ya wawekezaji bali kwa kuona mkataba hauna maslahi kwake! Na pasipo na MIGA, taifa husika linaweza kuwa na mifumo yake yenyewe ya uwazi na huru; na hivyo kutokuwa tishio kwa wawekezaji!!!

But on top of that, hata kama ingekuwa kujitoa, Tanzania isingekuwa ya kwanza! Back 2007, Bolivia baada ya kuona wanaibiwa sana kwenye mafuta yao, hiki ndicho kilifuata:-

Mwaka 2012 nao, Venezuela nao wakachomoa betri!

Kisha soma hapa:-
All in all, hiyo sio hoja. Hoja ni upotoshaji wa kile alichosema TL. Akina Mataga wanaacha maelezo ya awali ya TL na kuchukua kipengelea kwamba "TL alisema serikali ikiwabughudhi Acacia basi watatupeleka mahakamani"

Na kimsingi sio alisema Tz ijitoe, bali kama serikali haijaanza kupambana na hawa akina Acacia, ijitoe kwanza ili kuwanyima pumzi Acacia!!
 
Hahaha nilitaka kuelewa, mikopo ndiyo inaitwa misaada au ni vitu viwili tofauti?!
Maana serikali inatumia mapato ya ndani, na mnasema tunapata misaada, yenyewe inatumika wapi na lini na nani anaitoa?!
Je, huwa tunakopa lini ikiwa inaonekaka pesa za ndani zinatosha na mnasema misaada tuna pata?!
Nani anatumia misaada hii, au inatumika wapi, lini na kwanini?!
 
TL aliwasilisha hoja yake vizuri tu bali watu walipotosha! Waliacha yoooooooooooooote aliyoongea waka-exaggerate kipengele kimoja wapo na kudai alisema "...serikali ikiwasumbua Acacia basi Acacia itatupeleka mahakamani!" Hicho sicho alichosema TL
 
Leo nimeona hii Barrick to Restart Gold Mining in Tanzania
Huko wallstreet journal, tuwekee kwenye lugha ya SADC mkuu. Imeelezea yoote ya nyuma kwa kizungu, sasa sisi huku SADC tunaweza kupitwa na huondo motomoto wa leo.
 
CCM ni wasanii hatari, leo wanataka kujitoa kwamba eti hawakushiriki ku sign hii mikataba ya kilaghai ya madini na maliasili nyingine nyingi...yaani wanatakiwa wawaombe radhi watanzania... tumeibiwa mno sababu ya CCM.

Leo hii wanataka kuwageuzia kibao watetezi wa mali asili zetu miaka nenda rudi kama kina Lissu na wengineo kwamba si wazalendo bali eti ni watetezi wa mabeberu.

CCM hebu muogopeni Muumba mbingu na nchi.....anawaona mnayoyafanya...!!
 
huwezi ukawa msaliti alafu uendelee kuishi, kama kuna mwingine anataka yampate ya kumpata bas afanye usaliti kwa nchi. wamesomeshwa kwa pesa za serikali wazazi wao walikua masikini wa kutupwa, wakulima waliochoka 'strong and tired peasants' leo wanakashifu na kuisaliti nchi kwa kitu so called democracy. endeleeni kuzusha ila sio usaliti... you will kiss your @ss
 
Yaani ni mchezo unachezwa ili kufuta uzalendo wa Tundu Lissu toka enzi na enzi, pale alipokuwa akipambana na ULOFA wa Mkapa na kuwatetea wananchi mamia walioswekwa ndani kwa kesi za kubambikiza. Leo CCM wale wale wamebadili ngozi toka mbwa mwitu kuwa kondoo, wakijifanya watetezi. Kumbe ni kambi ya majizi watupu. hebu waulize ule mgao wa pesa za Escrow zile za kigeni, kuna hata mmoja amewajibishwa???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…