Acheni kupotosha alichokuwa amesema Tundu Lissu kuhusu Acacia na MIGA


..kweli.

..lakini kwa ccm wako radhi nchi iingie hasara kuliko kuchukua wazo zuri toka kwa mTz aliye nje ya chama chao.

..TL alianza kupinga madudu tangu miaka ya 90 wakati serikali inataka kuingia mkataba wa mgodi wa Bulyankulu.

..miaka yote walikuwa wakimpinga TL.

..Walipoona haiwezekani tena kupinga hoja zake,na inabidi wakabiliane na makampuni ya madini,wakaanza kumchafua binafsi.

..Juhudi za kumchafua zilipoanza kugonga mwamba, kutokana na jinsi TL alivyokuwa
anajibu mapigo na kuonekana kuwa na credibility zaidi ktk kutetea rasilimali zetu ndipo likatokea shambulio la kinyama.
 
Basi mara moja moja uwe unapitapita pale mitaa ya Mnazi mmoja.
Hahaha sawa, lakini naogopa kesi za uzururaji kutoka kwa mgambo wa jiji.
Nilipoteza kitambulisho cha machinga, na kile hakirudi, maana hakina Jina langu.
 
Mbona ktk maelezo yako kama gazeti yasiyo kuwa na kichwa wa miguu inaonyesha wewe ndio unajitekenye mwenyewe halafu unacheka mwenyewe.
 
True... ila kwenye makanikia alikuwa anawatetea wazungu na alimudu sana.

UCHUNGUZI HURU UMEBAINI KWAMBA LISSU THE GREAT NDIYE MWANASHERIA BORA KABISA KUWAHI KUWEPO KWENYE ENEO LA MAZIWA MAKUU TANGU KUUMBWA KWA MBINGU NA ARDHI .
 
Mnaanza kujikosha eeehh!
 
Mimi nimekuelewa ila kuna watu hii hoja yako wataiweka katika muktadha wa siasa hawatakuelewa na watakuponda.
 
Kwa hiyo tumenyolewa kwa chupa kama alivyokuwa anasema huyo jamaa?
 
Leo nimeona hii Barrick to Restart Gold Mining in Tanzania
Huko wallstreet journal, tuwekee kwenye lugha ya SADC mkuu. Imeelezea yoote ya nyuma kwa kizungu, sasa sisi huku SADC tunaweza kupitwa na huondo motomoto wa leo.
Mimi kinachonitia hofu sio kinachoripotiwa na media bali kinachosemwa na wenyewe Barrick! Kwa mfano, ukisoma Ripoti Rasmi kutoka Barrick Gold, kuna sehemu wanamnukuu Mark Bristow, ambae ndie President & CEO wa Barrick kwa sasa! Bristow anasema:- Kauli hiyo ya CEO wa Barrick ni ya kuiogpa kama ukoma kwa sababu inaonesha wazi kwamba anawaandaa kisaikolojia Wafanya Maamuzi!

Hapo serikali wasipokuwa makini, ile 16% lazima Barrick waifanyie figisu figisu kwa sababu, mapato ya 16% yetu yatatokana na Gawio/Dividends!

Na ni utaratibu wa kawaida kwa kampuni yoyote ile kwamba, kampuni italipa dividends pale tu kampuni inapotengeneza faida! Lakini kutengeneza faida haitoshi, bali kampuni pia iwe imesimama vizuri!

Kampuni iliyopata 3 years value destruction kama ambavyo Barrick wanataka kutuaminisha ni kampuni inayotakiwa ku-recover kutoka kwenye hiyo destruction!!

Kampuni inayojaribu ku-recover itakuwa na uwezekano mdogo sana wa kutengeneza faida, na kwahiyo pia ina uwezekano mdogo sana wa kulipa dividends... hivi ndivyo Barrick wanachojaribu kutueleza!!

Lakini katika ku-recover, hata kama unapata faida si busara kutumia faida hiyo bali busara ya kibishara ni kutumia faida hiyo kufanya re-investment ili kampuni isimame sawasawa!!

Kwa mara nyingine,ni kama Barrick wanajaribu kutueleza kwamba, kampuni inayofanya re-investment ya faida yake na yenyewe ni ngumu sana kulipa dividends!!!

Sasa serikali wasipokuwa makini na hiyo timu yao ya wawakilishi kwenye kampuni ya Twiga, basi watarajie mwisho wa mwaka balance sheet ya Twiga Company itakuwa inasoma mapato ni madogo sana kuweza kulipa dividends, na kama yapo basi imeonekana ni busara ku-reinvest ili mnyama Twiga asimame sawasawa!!!!

Na hapa tukumbushane hili suala la Free-carried share linawasumbua nchi nyingi tu walio-adapt hii kitu! Anglophone countries kwa mfano, wao wanaita Free-Carried Interest (FCI), na wengi wanakumbana na figisu figisu za kutolipwa hiyo FCI.
 

..tunachopaswa kuangalia hapa ni hiyo migodi ita-last muda gani kuanzia sasa hivi.

..kuna mgodi kama Nzega muwekezaji alishaondoka katuachia mashimo.

..migodi itakayokuwa chini ya hii arrangement mpya ina muda mrefu kwenda mbele, au tumeishia kugawana " mkia " nyama yote imeshaliwa?
 
Kwa taarifa yako mapato ya ndani hayatoshi. Tra inakusanya wastani wa trillion 1.3 kwa mwezi hivyo kwa mwaka ni zaidi trillion ya 15. Bajeti ya serikali kwa mwaka ni zaidi ya trillion 30 hivyo kuna nakisi ya zaidi ya trillion 15.

Ili kupata fedha za bajeti zinazopelea serikali hupata misaada ambayo hailipwi na pia kukopa kutoka nchi marafiki na mabenki ya ndani na nje.
 
Nakuelewa lakini kwanini tusiwape muda tukaona hiki kipya kabda kinaweza kuwa na value, tofauti na ilivyokuwa hapo mwanzo. Na labda, wmeweka room ya ku revisit mikataba na kuona wai nani anaumia ba nani anamumiza mwenzake. Maelezo ya kabudi, kwenye mkataba mpya kuna kipengee cha ku revisit maraba kila baada ta miajka mitano.
Siping kuwa extra careful,lakini kwanini tusiwape muda kwa hiki cha sasa tukaona na ukashauri baadaye kwa kukosoa waliyoyasifia sasa, kama hayataonyesha mafanikio then.
I understand your position, a naona ni mapema kuanza ku doubt kabla hata plan haijawa excuted.
Leo wallstreet journal wanasema 16% share na watagawana benefits huoni wamekaba kote, licha ya wewe kuoa holes mapema?!
Wape muda.
 
Hivyo unasema misaada hatupati?! Au uliposema misaada hailipwi ulimaanisha mikopo?! Hii misaada zinatolewa lini, na ziatumika wapi sasa?!
Wakati wa mkapa alikuwa akisema tulitoka kutegemea budget ya wafadhil 80% hadi yukawa na budget yetu ya 80% wafadhili 20%, wakati huo mikanda ilibanwa, TRA ikaundwa.
Wakati wa kikwete, mambo yalikuwa, bomba wanavyosema, sasa ni lini uchumi umeharibika maana sasa ndio tunaambiwa tuko vizuri tunakaribua kuwa dona contre, lini tumeanza kuyumba?! Misaada inaenda eneogani tusilotumia pato la ndani?!
 
Nimezungumza kwa kuweka tahadhali si tu kwa sababu hata kwa wenzetu suala la Free Carried Interest limejaa figisu figisu, hata hapa kwetu suala la kampuni za madini ku-declare loss sio jambo la ajabu!!

Sasa CEO anaposema kulikuwa na destruction kwa kampuni na kwahiyo panahitajika kazi ya ziada, hiyo kwangu ni Red Flag kwa serikali isije kesho na kesho kutwa Barrick waka-claim ili kuifanya Twiga isimame, basi mapato yanayopatikana in a given year yawe re-invested ili hatimae wasilipe hiyo 16%!

Mbaya zaidi, hoja ya reinvestment inaweza kuonekana ni rational bila kujua what's behind that reinvestment! Man, 16% si pesa ndogo kwahiyo usitarajie Barrick watakuwa wanaitoa kirahisi rahisi tu!! Kama patakuwa na upenyo wa kutoilipa, trust me, watautumia huo upenyo!!

Kwamba ni mapema kuwa-doubt; HELL NO... don't trust these people!!! Hawa unatakiwa kukaba hadi penalti, na wajue kwamba unajua hawawezi kukudanganya!!!

Na kama nilivyowahi kusema hapo kabla, this's an old wine in a new bottle... Barrick na Acacia ni wale wale, na kabla Acacia hawajaitwa Acacia walikuwa wanaitwa African Barrick Gold (ABG).

In 2014 baada ya kuandamwa sana na scandals, ndipo wakabadili jina kutoka African Barrick Gold na kuwa Acacia, na enzi hizo ABG ilikuwa inaendeshwa moja kwa moja na hawa hawa Barrick Gold, ambao hivi sasa watakuwa wanaendesha Twiga!!

Kwahiyo, manufaa kwa serikali wala hayatatokana na Barrick kuwa malaika kwa sababu hawana huo umalaika bali yatatokana na serikali wenyewe kuwakazia... na muhimu zaidi, wawakilishi wake ndani ya Twiga wanatakiwa kuwa watu waadilifu kweli kweli na wenye weledi wa kutosha!!

Kuhusu ku-revisit mikataba... binafsi nimepitia ile mabadiliko ya sheria ya madini ya mwaka 2017! Inawezekana sikuwa makini lakini sikuona kipengele cha ku-revisit mikataba!! Hata hivyo, ni Sheria ya Madini ya mwaka 2010 ndiyo ina kipengele cha ku-revisit Sheria ya Madini (sio mikataba) kila baada ya miaka 5!

Ni hiyo sheria ndiyo ilimpa Magu nguvu kupitia upya sheria ya madini mwaka 2017 kwa sababu hiyo sheria ya madini ya 2010 ilianza kufanya kazi 2012, na 5 years later, ndiyo 2017 ambayo Magu nae akaitumia! Na hapo ndipo akapata nafasi ya kupandisha mrabaha kutoka 4% & 5% to 6%, kufuta TMAA, introduction of 1% Clearance Fee, na mabadiliko mengine.
 
Nakuelewa sana, na hawa Barrick Gold Mine waliwahi kudhulumiwa sana, hata na serikali yetu huko nyuma kwa uharibifu wa mazingira. Lakini mengine sikumbuki ila nina jarida la African Science reserch journal limewataja nilisoma zamani kidogo ila walikuwa wakilalamikiwa.
Na kuhusu revisit ya mikataba ni moja ya vitu kabudi alikuwa akitamba wamevifanikisha wao, ingawa umeshalitolea maelezo.
Serikali inaamini watakuwa vizuri, na niwao tu wenye mamlaja na hili, sio bunge wala yeyoteawaye bali wao, hivyo sioni wakifanya tofauti na ilivyo sasa, unachokisema kina make sense, basi nakushauri jivue u anonymous uwe verified user, kisha upeleke mchango wako kwao. Wakikataa basi, lakini utakuwa umejaribu.
Au upeleke mchango wako sasa live kwa Kabudi who seemed to be the key person on all new contracts despite his role as a minister of foreign affairs. Muongee, what you think na labda ata ku enlight what is inside the contracts yote.
Huwa sioni shida why, mawazo yakataliwe unaweza kutoa faida kwa taifa zima kama sio, kwako binafsi kulipwa kwa mawazo yako.
Jaribu, kisha utuletee mrejesho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…