ACT Wazalendo: Iwapo Nchimbi hataonekana hadharani ndani ya wiki moja tutaiburuza Serikali mahakamani

Upuuzi huu jamani hadi naona aibu Wapinzani mnakwama wapi ?

Ni kwamba mnafurahia baadhi ya mambo yakitokea ili mpate agenda

Nchimbi amekuaje mtu wenu gafla mpka mmekua na uchungu mkali kiasi hiki?

Siasa za Tanzania sometimes ni takataka 🚮
Hapa mbona umewaza kwa hisia zaidi, kiongozi.
Ila ukiwa objective huwezi kuwa na mtazamo huo.
 

Weww furahia kisa unapiga buku 7 au uko kwenye system, nakuambia yana mwisho haya, hata hao nchimbi na Pole pole hawakutegemea yatawakuta haya
 
Kama bado kuna namna anatumia kodi za wananchi, umma una haki ya kujua yuko wapi. Serikali itusaide kujua mara ya mwisho alipotakiwa kukabidhi vitendea kazi vya serikali baada ya kufukuzwa alikua wapi.
 
Wewe umefanya lipi la tofauti la kuifanya Ccm itoke madarakani?
kuelimisha watu kila ninapopata nafasi kwamba hatua ya kwanza ni sisi kuweza kudai madai yeyote yale ambayo serikali ina wajibu kwa kutumia njia rasmi.

na kimsingi lengo kuu wala haitakiwi kuitoa ccm madarakani, ccm inapaswa kushurutishwa kufanya wajibu wake
 
Mkuu, Wasilisho lako la awali limekosa mashiko kwa sababu limejengwa kwenye msingi wa hisia.
Wewe ndio umetumia hisia
Kuchambua wasilisho langu hilo sio tatizo langu ni tatizo lako
Sina namna ya kukusaidia
Kama hutojali ungefanya rephrasing ili ujenge hoja inayohitaji kupingwa kwa hoja.
Nimejenga hoja mbona
Wewe tu umekosa hoja ya kupingana na wasilisho langu

Kama ukipata hoja karibu nipoo na muda ninao
 
Kama huwezi kuwalaumu walio rusha risasi huja haja ya kulaumu chadema

Kwani maandamano ni jinai
Mpaka useme chadema walipaswa kukemea
nikikuuliza watu walienda wapi dec 9 utaona kama nataka kudhihaki wananchi,

mimi sio mwanachama wa chama chochote, hivyo kwenye mgogoro uliotukuta napima ccm walifanya nini?, chadema walifanya nini?

yawezekana hatuwezi kuelewana kwa muda mfupi, ila nakuacha na mtizamo huu wa kutafakari

chadema waliona hatari ya maandamano siku ya uchaguzi? , kama ndivyo walifanya nini kuwasaidia potential victims wa kadhia hiyo ?

kama hawakuona hatari basi ni masikitiko sana , na kama waliona na wakakaa kimya basi ni msiba mkubwa zaidi wao na ccm hawana tofauti.
 
nikikuuliza watu walienda wapi dec 9 utaona kama nataka kudhihaki wananchi
wewe kua open unaogopa nini ?
,

mimi sio mwanachama wa chama chochote, hivyo kwenye mgogoro uliotukuta napima ccm walifanya nini?, chadema walifanya nini?
Mie pia ukifatilia mijadala yangu utaona sina chama wala sina haja na chama

Mara zote nasema shida sio CCM
Kama hii nchi isiposimikwa misingi mipya na imara iliyo bora hata chadema au wengine wakipewa nchi wembe utakua ule ule
yawezekana hatuwezi kuelewana kwa muda mfupi, ila nakuacha na mtizamo huu wa kutafakari

chadema waliona hatari ya maandamano siku ya uchaguzi? , kama ndivyo walifanya nini kuwasaidia potential victims wa kadhia hiyo ?
Swali langu linarudi pale pale
Kwanini unalaumu chadema na sio CCM Chauma au ACT ?
kama hawakuona hatari basi ni masikitiko sana , na kama waliona na wakakaa kimya basi ni msiba mkubwa zaidi wao na ccm hawana tofauti.
Natamani mimi na wewe tupate muda wa kutosha niambie kama una muda ni kutag sehemu
 
Kimsingi ACT wapo sahihi kuhoji the whereabouts ya raia namba mbili Tanzania, aliyekuwa makamu wa raisi sio kwa kuwakilisha chama chake, lakini taifa. Aliyepigiwa kura na 98% ya wapiga kura(?), huyu mtu ameachia madaraka kwa barua, hakuna mahali tuliona akifanya press na waandishi wa habari, huyu mtu yuko wapi?

Angekuwa ameachia nafasi kwenye chama chake, hayo yangekuwa mambo ndani ya chama, lakini huyu ni raia namba mbili na taifa(regardless of political differences) linapaswa kujua alipo, maana hakuna mahali aliongea.

Hii ni national issue, sio swala la chama fulani. Utashangaa mwaka unapita na jamaa haonekani, familia yenye woga inakaa kimya maana tupo kwenye taifa la kutekana na kuuana.
 
Mie pia ukifatilia mijadala yangu utaona sina chama wala sina haja na chama

Mara zote nasema shida sio CCM
Kama hii nchi isiposimikwa misingi mipya na imara iliyo bora hata chadema au wengine wakipewa nchi wembe utakua ule ule
hapa nakuunga mkono , na kama kweli unamaanisha basi tumeshafika muafaka.

Swali langu linarudi pale pale
Kwanini unalaumu chadema na sio CCM Chauma au ACT ?
kutokuilamu ccm haimaanishi ccm haina makosa miaka yote hii ccm inafanya makosa, nachosema mimi kwenye janga lile hivyo vyama viwili vikubwa wote wameonesha incompetence , mkombozi anayetegemewa na wengi cdm imeonesha udhaifu mkubwa sana.

Natamani mimi na wewe tupate muda wa kutosha niambie kama una muda ni kutag sehemu
mimi nipo karibu kila siku mkuu
 
Kweli huko ni kuweka siasa kwenye kila jambo. Ina maana ACT wameshindwa kutuma muwakilishi kwenda nyumbani kwa Balozi Nchimbi kumuulizia kama yupo au hayupo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…