ACT Wazalendo wataka Zanzibar ipewe mamlaka kamili

ACT Wazalendo wataka Zanzibar ipewe mamlaka kamili

Yapi hayo yanabaki ya nje ya mamlaka? Kwanini yabaki nje ya mamlaka ya Zanzibar ila Tanganyika Bado Ina "mamlaka" yake!!
Tanganyika haipo as a state kama wao walivyo.

Kuna ajira ngapi ambazo wazanzibar wanazipata kupitia Muungano?

Bila shaka tukienda wanakotaka waathirika wakuu ni wao wenyewe maana Tanzania bara hakuna inachonufaika na Muungano kiuchumi zaidi ya kisiasa tu
 
Kama ni hivyo kwanini serikali ya tanzania bara na viongozi wake wasi iachie zanzibar ?
Acha kuongea usilolijua mzee. Ngoja nifumbe mdomo wangu. Endelea kuongea kwa mihemko.
Sasa ukifumba mdomo tutajuaje kama una hoja ya msingi au lah?
 
Hivi suala la serkali moja kwanini wengi hawalipigii chapuo! Kwangu naona zanzibar iwe tu mikoa. Serkali moja. Bunge 1. Mahakama 1.
Haiwezekan tumeshafikia maono ya Africa Mashariki kuelekea sarafu 1.
Africa 1.
Alafu bado Tanzania tunajikata vipandepande
ACT wanafanya siasa hadaa, ambazo walistahili kuifanya enzi ya zama kupambana na ukoloni siyo sasa.
 
Kwani lazima wapinzani wote wafanane mawazo?
Hamuwezi kufanya siasa bila kushambulia wengine?..
Au upinzani ni Chadema peke yake?
Wengine lazima wapigwe vita??
Mkuu mimi sina chama chochote. Ni raia tu wa kawaida. Ila kitendo cha ACT Wazalendo kuipigania Zanzibar pekee kuwa na mamlaka kamili huku wenye akili tukiona kwamba ni Tanganyika pekee ndio iliyokuwa inahitaji haya mamlaka kamili kinashangaza sana.
Zanzibar tayari ina raisi wake, ina serikali yake, ina bendera yake, katiba yake, wimbo wa taifa wake na mengine mengi, huku Tanganyika ikiwa haipo na haina hata kimoja.

So kwanini tusihoji? ACT Wazalendo ni chama kilichoundwa kwa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sio katiba ya Zanzibar kwahiyo kingejikita zaidi kwenye mambo yanayohusu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sio kujikita kwenye kuipigania Zanzibar pekee yake.
 
Mfano wako wa Gambia hauendani na wa Zanzibar kwa sababu Gambia ni nchi kwa mujibu wa sheria za kimataifa
Ulisema kwamba Zanzibar haiwezi kuwa na muungano kisa Ina watu wachache. Ndio nkasema nchi kuwa na watu wachache sio issue hata The Gambia ni nchi ndogo kispace na population ila iliwahi kuwa na muungano na Senegal huko nyuma licha ya disparity hiyo.

Na nmesema hata UN The Gambia Ina kura 1 kama ambayo India yenye raia billion 1 Ina kura Moja pekee.
 
Sasa Zanzibar haiwezi kuwa na mamlaka kamili kinchi kama zilivyo nchi zingine huru halafu kuwe na Muungano
EU wamewezaje? Yaani Zanzibar inatakiwa iwe na mamlaka kamili alafu Tanganyika iwe na mamlaka kamili kupitia koti la Muungano. Kwa hiyo nchi mbili ila Zina muungano kwa baadhi ya mambo kma Fedha, jeshi n.k mbona simple tu.

Kama tu Wales na England nchi Zina mamlaka kamili ila zinashirikiana vitu Fulani ambavyo ni vya muungano.

So Zenji ingekua WHO, FAO, n.k na Tanganyika (ambayo imevaa koti la Tanzania) nayo iwe member.

Tuwe na mfumo kama wa EU, au Common market tu, Integration fulani Ili Kila nchi iwe na uhuru kwenye mambo yasiyo ya muungano
 
Tanganyika haipo as a state kama wao walivyo.
Tanganyika ipo mkuu, mfano wizara ya michezo sio jambo la muungano hivyo Yule waziri ni wa Tanganyika maana Zanzibar Wana waziri wao wa michezo!

So serikali ya Tanzania ni Tanganyika Ile ile sema imeongezewa duties za Zanzibar kwenye eneo mfano fedha na uchumi n.k.

Ilihali state ya Zanzibar imeporwa vitu kma FAO, WHO n.k
 
Wapewe inchi yao, na Tanganyika wapewe ya kwao, watakaokataa kumuachia mwenzake hao ndio wakorofi
Najua tu upo upande hautaki kuachia ila unajidai kama unataka, fix tu
Wapewe nchi yao kina nani? Maana tayari Zanzibar wana nchi yao, lkn hakuna nchi inayoitwa Tanganyika.
 
Inabidi kwanza wafafanue mamlaka kamili unahusu nini. Je unahusu kusimamia uchumi wao kikamilifu? Kama ni hivyo ina maana wawe na Benki Kuu yao wenyewe na fedha zao wenyewe. Aidha, itabidi vile vile wawe na wizara yao ya Fedha itakayosimamia ukusanyaji wa kodi zao na usimamizi wa sera zao za mambo ya fedha.

Je inahusu uwakilishi katika taasisi za kimataifa kama Umoja wa Mataifa na Fifa? Kama ni hivyo ina maana watahitaji kuwa na wizara ya Mambo ya Nje yao wenyewe ambayo itasimamia uwakilishi wao huko Umoja wa Mataifa, AU na kwengine.

Je inahusu uwezo wao wa kuamua kuingia katika vita? Kama ni hivyo watahitaji kuwa na jeshi lao wenyewe ambalo litawajibika kwa Rais wa Zanzibar.

Je inahusu usimamizi wa masuala ya uhamiaji yao ili waweze kuamua kikamilifu nani ana haki ya kuishi Zanzibar na kutambulika Kama mzanzibari? Hii si ina maana wawe na wizara yao ya Mambo ya Ndani ambayo itakuwa pia na mamlaka ya kutoa Pasi za kusafiria kwa raia wa Zanzibar?

Wakiwa na vyote hivi, serikali ya Muungano itakuwa inafanya nini? Ukweli ni kuwa hakuna Muungano wa nchi yeyote ambao kila nchi iliyoungana ina mamlaka kamili. Namna pekee ya kuwa na mamlaka kamili ni kuwa nchi ambazo hazijaungana. Kwa mantik hii ingekuwa vyema kama ACT-WAZALENDO wangesema wazi kuwa hawautaki Muungano na kuwa wakishika dola watahakikisha kuwa unavunjika.

Amandla...
 
Yaani muungano wa Sasa Kuna masuala ya muungano, masuala yasiyo ya muungano bara, na masuala yasiyo ya muungano Zanzibar.

Sasa katiba inasema serikali ya muungano ni both masuala ya muungano na masuala yasiyo ya muungano ya bara.

Na Zanzibar inasimamia masuala yasiyo ya muungano kwa upande wake.

ILA

Tanganyika (Ambayo ndio hiyo hiyo muungano) inawaamulia mambo yasiyo ya muungano.

So wanachotaka mfano michezo sio suala la muungano why hawawezi kushiriki Olympic au AFCON!! n.k so wao wanataka hicho tu Cha kujiamulia wenyewe mambo yasiyo ya muungano kama afya, elimu n.k

Cc Mohamed Said
Hawawezi kushiriki katika Olympics au World Cup kwa sababu vyombo hivyo vinatambua nchi zenye mamlaka kamili peke yake ( isipokuwa tu kwa Umoja wa Kifalme kwa sababu msingi wa mpira ulikuwa ni ushindani kati ya England, Scotland na Wales). Njia pekee ya Zanzibar kushiriki kama Zanzibar ni kutoka kwenye Muungano.

Amandla...
 
EU wamewezaje? Yaani Zanzibar inatakiwa iwe na mamlaka kamili alafu Tanganyika iwe na mamlaka kamili kupitia koti la Muungano. Kwa hiyo nchi mbili ila Zina muungano kwa baadhi ya mambo kma Fedha, jeshi n.k mbona simple tu.

Kama tu Wales na England nchi Zina mamlaka kamili ila zinashirikiana vitu Fulani ambavyo ni vya muungano.

So Zenji ingekua WHO, FAO, n.k na Tanganyika (ambayo imevaa koti la Tanzania) nayo iwe member.

Tuwe na mfumo kama wa EU, au Common market tu, Integration fulani Ili Kila nchi iwe na uhuru kwenye mambo yasiyo ya muungano
European Union sio nchi bali ni ushirika wa nchi kama ilivyo EU. England, Wales, Northern Ireland na Scotland hazina mamlaka kamili. Scotland, Wales na Northern Ireland zina mabunge na serikali zao kama ilivyo Zanzibar lakini maamuzi makubwa yanayohusu UK yanafanywa Westminster.
Hatuwezi kuwa tumeungana Kama kila mmoja wetu atakuwa na mamlaka ya kujifanyia anavyotaka. Hata katika ndoa, wanandoa wanakubaliana kila mmoja kupoteza sehemu ya uhuru wake na kuishi katika misingi ambayo wanakubaliana. Tofauti na hivyo sio ndoa.

Amandla...
 
Marais tunawachagulia huku Dodoma,
Sheria tunawatungia huku Dodoma,
Hiyo haiwatoshi? Waambie wakae kwa kutulia.
 
Back
Top Bottom