ACT Wazalendo wataka Zanzibar ipewe mamlaka kamili

ACT Wazalendo wataka Zanzibar ipewe mamlaka kamili

Unadhani kutakuwa na faida gani kwa Tanganyika nchi kwenda kwenye federation badala ya nchi moja?

Kwa sasa nani ni mnufaika wa Muungano katika ya Zanzibar na Tanzania bara ?
Kwa mujibu wao anayefaidika ni Tanganyika maana yeye ni both Tanganyika na pia ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Na Zanzibar haikui maana haiwezi jitegemea kiuchumi kisa kubanwa na Tanganyika kujiamulia masuala kma gesi na mafuta, Kodi, bandari huru, benki kuu, kitu UN, kushiriki michezo kimataifa n.k.

Yes mwingine atasema Zenji ananufaika ila wao wanapiga hesabu kwamba bila muungano wangekua kama Seychelles au Taiwan.

So hatuwezi fahamu haya yote mpaka wote tuwe na mamlaka kamili
 
Hawa ACT ni oppurtunist na zitto ndio oppurtunist mkubwa. Hana itikadi anayoiamini ila chochote kinachokuja mradi mkono uende kinywani. Watu mnaoperate katika katiba ya taifa moja halafu unakuta chama kimoja kinataka kuvunjwa katiba hiyo. Ukiwapa zanzibar madaraka kamili maana yake nini? Ukisikia yale wanzanzibari hao wa ACT zamani wakiwa CUF kitu wanataka utashangaa. Wanakuambia wanataka muungano ila wawe na madaraka kamili ikiwa ni kua na kiti umoja wa mataifa, kua na mabalozi nje, kua na passport yao. Hapo ndio mtu unashangaa wanataka muungano kweli au wanafanya mzaha.
 
Tanganyika ina mamlaka kamili yapi wakati haipo hata katika ramani ya dunia? Ikibalika kuwa na serikali tatu(though kwa mtazamo wangu either iwe serikali moja au muungano uvunjwe, one the two) ndipo utabaini jinsi Tanganyika ilivyomezwa kijinga na hilo la eti Tanganyika ina mamlaka kamili chini ya koti la muungano hata zuzu ajafahamu ya kuwa that shit doesn't exist.
Yaani JMT inashughulika na mambo ya muungano na yasiyo ya muungano ya upande wa Tanganyika. Ila serikali ya Zanzibar inashughulika na mambo yasiyo ya muungano kwa upande wa zenji.

So mpaka hapo serikali ya Tanganyika ndio hiyo hiyo ya JMT so unaweza ona imevaa koti la muungano hivyo zenji ni kama mualikwa tu au kawilaya tu.

Ndio wao wanasema Tanganyika ibaki na mamlaka kamili na wao wawe na mamlaka kamili ILA mambo ya muungano pekee ndio yabaki JMT.

Hopefully umeelewa hoja Yao!! Hawataki nchi mpya au kujitawala ila wanataka MAMBO YASIYO YA MUUNGANO yaamuliwe na ZANZIBAR kuliko Sasa wanafungwa na JMT ambayo ndio hiyo hiyo Tanganyika!!
 
Huu muungano either uvunjwe or uwe wa serikali 3 ili Tanganyika nayo itambulike na sio kuendelea na huu muuondo wa kipumbavu wa serikali 2 unaoibeba Zanzibar
Vipi serikali moja, nayo huipendi? Tatu za kufanyia kitu gani?
 
Yaani JMT inashughulika na mambo ya muungano na yasiyo ya muungano ya upande wa Tanganyika. Ila serikali ya Zanzibar inashughulika na mambo yasiyo ya muungano kwa upande wa zenji.

So mpaka hapo serikali ya Tanganyika ndio hiyo hiyo ya JMT so unaweza ona imevaa koti la muungano hivyo zenji ni kama mualikwa tu au kawilaya tu.

Ndio wao wanasema Tanganyika ibaki na mamlaka kamili na wao wawe na mamlaka kamili ILA mambo ya muungano pekee ndio yabaki JMT.

Hopefully umeelewa hoja Yao!! Hawataki nchi mpya au kujitawala ila wanataka MAMBO YASIYO YA MUUNGANO yaamuliwe na ZANZIBAR kuliko Sasa wanafungwa na JMT ambayo ndio hiyo hiyo Tanganyika!!
Kama kawaida yako mkuu 'zitto junior', umejitahidi vizuri sana kueleza jambo husika kwa ufasaha kabisa lakini bado ni shida kueleweka.

Kuwa na "mamlaka Kamili" itawezekana vipi wakati kuna baadhi ya mambo yanabaki kuwa nje ya mamlaka?
Huoni hapa kuwa kuna kujichanganya kiaina, tena nadhani kwa maksudi tu kwa hao wanaoimba "mamlaka kamili".
 
Yapi hayo yanabaki ya nje ya mamlaka? Kwanini yabaki nje ya mamlaka ya Zanzibar ila Tanganyika Bado Ina "mamlaka" yake!!
 
Yapi hayo yanabaki ya nje ya mamlaka? Kwanini yabaki nje ya mamlaka ya Zanzibar ila Tanganyika Bado Ina "mamlaka" yake!!
Sasa kuna ugumu gani kurahisisha tu lugha, kwamba kila nchi ijitegemee kivyake,; kwa mambo yake yote?
 
Hawa ACT ni oppurtunist na zitto ndio oppurtunist mkubwa. Hana itikadi anayoiamini ila chochote kinachokuja mradi mkono uende kinywani. Watu mnaoperate katika katiba ya taifa moja halafu unakuta chama kimoja kinataka kuvunjwa katiba hiyo. Ukiwapa zanzibar madaraka kamili maana yake nini? Ukisikia yale wanzanzibari hao wa ACT zamani wakiwa CUF kitu wanataka utashangaa. Wanakuambia wanataka muungano ila wawe na madaraka kamili ikiwa ni kua na kiti umoja wa mataifa, kua na mabalozi nje, kua na passport yao. Hapo ndio mtu unashangaa wanataka muungano kweli au wanafanya mzaha.
Kwa vile CCM imetawala nchi hii ya Zanzibar na Tanzania takriban Miaka 60 iliyopita, 30 bila ya vyama vingi, na 30 ndani ya vyama vingi. ACT Wazalendo chama DUME kina kila sababu kama chama cha upinzani kuyasemea yale yaliyokwenda kombo ili kuiwajibisha CCM kwa makosa ya kiutendaji au kisera , fikra, mipango au mifumo yake ya kiutawala ambayo imeshindwa kuondoa kero za wananchi ambazo ni (Umasikini,Maradhi, na Ajira)
 
Ukitaka kujua kuwa CCM imeshindwa Huku Zanzibar na Tanzania Kwa Ujumla watazame pale wanapovutana Kuhusu Madai ya SMZ katika Muungano .
Wenyewe hawakubaliani na wanashindwa kutatua changamoto za Muungano.
Huku ni kushindwa.
M<F
  1. Kushindwa kuweka udhibiti wa Ardhi
  2. Kushindwa Kuendeleza uchumi wa Bahari .
  3. Kushindwa kuboresha Muundo wa Muungano wetu na hatimae ule wa Afrika.
  4. Kushindwa kuendeleza uchimbaji wa mafuta na Gesi Zanzibar
 
Sasa kuna ugumu gani kurahisisha tu lugha, kwamba kila nchi ijitegemee kivyake,; kwa mambo yake yote?
Mbona EU ni shirikisho ila Kila nchi Ina bendera, jeshi n.k ila sarafu, biashara, sheria za kazi n.k Wana share!!

Ndio wao wanataka hivyo kwamba mambo yasiyo ya muungano basi yaamuliwe na wanachama wenyewe kama tu EU inavyo operate. Why masuala ya elimu na afya sio ya muungano ila Bado yanakua dictated na Tanganyika iliyovaa koti la muungano
 
  1. Kushindwa kuweka udhibiti wa Ardhi
CCM kila siku wanakuja na mipango mipya isiyo ondowa matatizo.
Tembelea Zanzibar miaka 60 iliyopita ikiwa na population ya watu laki mbili na nusu hivi.
Mji uliisha Darajani kwengine kulikuwa Ngambo nyumba za Vibanda bila Plan wa la Miundo mbinu ya Kisasa.
Miaka 60 baadae Mji umeishia Tunguu, Mfenesini na Kisauni
tazama watu walivyi jenga Ni squarter mbele kwa mbele . Hakuna Plan wala master plan ya Nchi
Ikiwa Visiwa vyenye ukubwa wa wilaya ya Ilala tuu wameshindwa kuwa na Master plan, Hivi wanaweza nini hawa?
Kwanini wasilaumiwe,?
Ukiwauliza utaskia Hatuna mam;laka ya kuendeleza Nchi hii ya Zanzibar.
 
Kwa vile CCM imetawala nchi hii ya Zanzibar na Tanzania takriban Miaka 60 iliyopita, 30 bila ya vyama vingi, na 30 ndani ya vyama vingi. ACT Wazalendo chama DUME kina kila sababu kama chama cha upinzani kuyasemea yale yaliyokwenda kombo ili kuiwajibisha CCM kwa makosa ya kiutendaji au kisera , fikra, mipango au mifumo yake ya kiutawala ambayo imeshindwa kuondoa kero za wananchi ambazo ni (Umasikini,Maradhi, na Ajira)
Duniani kote vyama huungana na kuwa na itikadi moja na kuunda Serikali, Kama sio swala la Tumbo maana yake ACT inakubaliana na Sera za CCM ndio maana wakaungana, tafuati na hapo wadanganyeni wajinga
 
  1. Kushindwa kuboresha Muundo wa Muungano wetu na hatimae ule wa Afrika.
    • Walipounganisha Tanganyika na Zanzibar walidai lengo nikuunganisha AFRIKA.
    • Ukitazama katiba haioneshi ruhusa ya kuongeza nchi nyingine kwenye muungano huu.
    • Wanapo vutana kuhusu Mfumo wa Muungano kurekebishwa ,wanafukuzana kwenye chama.
    • Aboud jumbe kafukzwa,
    • Maalim Seif kafukuzwa,Mzee Hassan Nassor Moyo kafukuzwa
    • Mansour Yusuf Himid Mtoto wa Mwana Mapnduzi kafukuzwa
    • Chupuchupu Amani Karume kufukzwa.
    • Sasa unajiuliza Huu muungani ni kwa maslahi ya Nanai, Mbona Hauendelezwi, Kwa nini Uwe unalindwa Kwa mitutu ya Bunduki na Kulishana Viapo vya Kuulinda?
    • Kulikoni?
    • Au ndio Vile tena aina ya Ukoloni.?
    • LET US BE HONEST
 
Yaani hatua kubwa ya kufikia serikali moja tuliyopiga turudi kwenye shirikisho tena ?

Muungano wa Tanzania hauwezi kabisa kufit kwenye mfumo EU.

Hata katika logic ya kawaida huwezi kutengeneza equal share of responsibility na rights kwenye nchi mbili moja ina 58 M population na nyingine ina 2M pouplation.

Mapato ya Zanzibar kwa mwaka yanazidiwa hata na mapato ya Manispaa ya Ilala.

Hao wataweza kuendesha serikali ya shirikisho kama EU?

Benefits as Muungano wanazifaidi zaidi Zanzibar kuliko Tanganyika.

Imagine fedha za Uviko kiasi walichopata ni karibia mapato yao ya mwaka mzima.

Wakienda kwenye mfumo wa EU kesho na keshokutwa watataka watoke kwenye Muungano kisa wameshindwa kuchangia uendeshaji wa serikali ya pamoja.

Bila shaka kina Zitto wanapiga zomari kwa wimbo wasioujua, au wanaujua ila wanafanya siasa za hadaa.
Kama ni hivyo kwanini serikali ya tanzania bara na viongozi wake wasi iachie zanzibar ?
Acha kuongea usilolijua mzee. Ngoja nifumbe mdomo wangu. Endelea kuongea kwa mihemko.
 
Logic ndogo anae ukumbatia muungano ndio mnufaika mkubwa, sasa Tanzania bara na Zanzibar nani yuko tayari kuua watu kuulinda? jibu ni rahisi Tanzania bara, ndio maana hata Rais wa Zanzibar mnachagua kutoka Dodoma ili mfanye mtakavyo kuulinda muungano

Ukweli ni kwamba viongozi wa juu wa smz ndio wanao upigania muungano hata ikibidi kuua ndugu zao,ndio huomba msaada wa kijeshi pia ndio waliomtumia jecha kuvuruga uchaguzi,wanufaika wakuu wa huu muungano wa mchongo ni tabaka tawala la smz.
 
Back
Top Bottom