ACT Wazalendo wataka Zanzibar ipewe mamlaka kamili

ACT Wazalendo wataka Zanzibar ipewe mamlaka kamili

Nimeliona hili la mimi...yanataka mamlaka kamili ndani ya muungano...na tafsiri yake ni kwamba hali ya muundo wa serikali 2 iendelee...katika setup ya serikali 2 tayari Zanzibar inamamlaka....hivyo Tanganyika utaendelea kufyonzwa
Yaani muungano wa Sasa Kuna masuala ya muungano, masuala yasiyo ya muungano bara, na masuala yasiyo ya muungano Zanzibar.

Sasa katiba inasema serikali ya muungano ni both masuala ya muungano na masuala yasiyo ya muungano ya bara.

Na Zanzibar inasimamia masuala yasiyo ya muungano kwa upande wake.

ILA

Tanganyika (Ambayo ndio hiyo hiyo muungano) inawaamulia mambo yasiyo ya muungano.

So wanachotaka mfano michezo sio suala la muungano why hawawezi kushiriki Olympic au AFCON!! n.k so wao wanataka hicho tu Cha kujiamulia wenyewe mambo yasiyo ya muungano kama afya, elimu n.k

Cc Mohamed Said
 
Kwani msimamo wa Zitto kuhusu Muundo wa muungano ni upi?

Maana tunajua wapemba hawataki muungano.
Kwenye bunge la Katiba Zitto alionyesha kutaka Muungano wa serikali moja.

Ila sasa hivi hawezi kuleta huo msimamo mbele ya kina Jussa.

Kifupi Zitto ni tapeli la kisiasa.

Sasa mamlaka kamili ndani ya Muungano yanapatikanaje ?
 
Sasa watakuwaje wanachama wa WHO wakati kwa mujibu wa Montevideo Convention Zanzibar is not a state ?
Ndio maana wanataka mamlaka kamili kama ambavyo Tanganyika Ina mamlaka kamili chini ya "koti" la muungano.

So mambo ya muungano tu ndio yawe yanafanywa pamoja ila yasiyo ya muungano Kila nchi iwe na Hadhi ya NCHI kama katiba Yao ya Zanzibar inavyosema. Sasa kama hiyo italazimu tuwe na mfumo kama wa EU it's well and good iwe federation tu sio nchi Moja Tena.
 
Yaani kustuka kwamba wananyonywa, wanatawaliwa, kwamba hawautaki muundo wa serikali mbili bora ziwe tatu, au iwe moja au muungano uvunjwe kila mtu arudi kwao aanze mambo upya ndiyo unaita chuki zilizomo mioyoni?
-Wewe una maoni gani kuhusu muundo wa muungano unaofaa au kuhusu kuuvunja huu muungano?
Soma comment za wenzako kuanzia mwanzo ndo utajua na hutaona maneno wanayoandika au utaona yapo sawa bas na ww ni wale wale tu.
 
Ipewe mamlaka haraka Sana. Mkoa unakua nchi ndani ya nchi. Katiba ije tutoe huu muungano tujue Kama tutakua na serikali moja, tatu au tuutupilie mbali. Eti wanataka gawio sawa na Tanganyika.
Acheni kuongea msiyoyajua.
 
Tunataka watu wenye nidhamu ya pesa na hofu ya mola na ujasiriamali kama wapemba watawanyike mikoa yote ya tanzania bara ili tujifunze kwao wakishirikiana na wakinga na wachagga.sisi makabila mengine tuwaige hawa watu.
 
Ndio maana wanataka mamlaka kamili kama ambavyo Tanganyika Ina mamlaka kamili chini ya "koti" la muungano.

So mambo ya muungano tu ndio yawe yanafanywa pamoja ila yasiyo ya muungano Kila nchi iwe na Hadhi ya NCHI kama katiba Yao ya Zanzibar inavyosema. Sasa kama hiyo italazimu tuwe na mfumo kama wa EU it's well and good iwe federation tu sio nchi Moja Tena.
Yaani hatua kubwa ya kufikia serikali moja tuliyopiga turudi kwenye shirikisho tena ?

Muungano wa Tanzania hauwezi kabisa kufit kwenye mfumo EU.

Hata katika logic ya kawaida huwezi kutengeneza equal share of responsibility na rights kwenye nchi mbili moja ina 58 M population na nyingine ina 2M pouplation.

Mapato ya Zanzibar kwa mwaka yanazidiwa hata na mapato ya Manispaa ya Ilala.

Hao wataweza kuendesha serikali ya shirikisho kama EU?

Benefits as Muungano wanazifaidi zaidi Zanzibar kuliko Tanganyika.

Imagine fedha za Uviko kiasi walichopata ni karibia mapato yao ya mwaka mzima.

Wakienda kwenye mfumo wa EU kesho na keshokutwa watataka watoke kwenye Muungano kisa wameshindwa kuchangia uendeshaji wa serikali ya pamoja.

Bila shaka kina Zitto wanapiga zomari kwa wimbo wasioujua, au wanaujua ila wanafanya siasa za hadaa.
 
Unadhani kutakuwa na faida gani kwa Tanganyika nchi kwenda kwenye federation badala ya nchi moja?

Kwa sasa nani ni mnufaika wa Muungano katika ya Zanzibar na Tanzania bara ?
 
Ndio maana wanataka mamlaka kamili kama ambavyo Tanganyika Ina mamlaka kamili chini ya "koti" la muungano.

So mambo ya muungano tu ndio yawe yanafanywa pamoja ila yasiyo ya muungano Kila nchi iwe na Hadhi ya NCHI kama katiba Yao ya Zanzibar inavyosema. Sasa kama hiyo italazimu tuwe na mfumo kama wa EU it's well and good iwe federation tu sio nchi Moja Tena.
Tanganyika ina mamlaka kamili yapi wakati haipo hata katika ramani ya dunia? Ikibalika kuwa na serikali tatu(though kwa mtazamo wangu either iwe serikali moja au muungano uvunjwe, one the two) ndipo utabaini jinsi Tanganyika ilivyomezwa kijinga na hilo la eti Tanganyika ina mamlaka kamili chini ya koti la muungano hata zuzu ajafahamu ya kuwa that shit doesn't exist.
 
Soma comment za wenzako kuanzia mwanzo ndo utajua na hutaona maneno wanayoandika au utaona yapo sawa bas na ww ni wale wale tu.
First and foremost sina 'wenzangu' humu na second ukishindwa kuijibu swali you either admit it or just ignore the question, kuja useless blah blahs ni ujuha uliopitiliza.
 
Nimekuuliza wewe uliyesema Tanzania bara inanufaika zaidi na Muungano kuliko Zanzibar
Logic ndogo anae ukumbatia muungano ndio mnufaika mkubwa, sasa Tanzania bara na Zanzibar nani yuko tayari kuua watu kuulinda? jibu ni rahisi Tanzania bara, ndio maana hata Rais wa Zanzibar mnachagua kutoka Dodoma ili mfanye mtakavyo kuulinda muungano
 
Huu ni utapeli

Screenshot_20230227-200807.jpg
 
Huu muungano either uvunjwe or uwe wa serikali 3 ili Tanganyika nayo itambulike na sio kuendelea na huu muuondo wa kipumbavu wa serikali 2 unaoibeba Zanzibar
Tuwe na Tanganyika yenye mamlaka kamili, sio Zanzibar yenye mamlaka kamili na Tanzania huo utakuwa upuuzi. Na ikiwa hivyo wazanzibar wote waliopo kwenye serikali ya tanganyika wote kurudi kwao itawahusu. Hatuwezi kwenda kwa style hii ya muungano wa nchi mbili kuwa nchi mbili. Better tuwe nchi moja au nchi mbili kila nchi kivyake.
 
Yaani hatua kubwa ya kufikia serikali moja tuliyopiga turudi kwenye shirikisho tena ?

Muungano wa Tanzania hauwezi kabisa kufit kwenye mfumo EU.

Hata katika logic ya kawaida huwezi kutengeneza equal share of responsibility na rights kwenye nchi mbili moja ina 58 M population na nyingine ina 2M pouplation.

Mapato ya Zanzibar kwa mwaka yanazidiwa hata na mapato ya Manispaa ya Ilala.

Hao wataweza kuendesha serikali ya shirikisho kama EU?

Benefits as Muungano wanazifaidi zaidi Zanzibar kuliko Tanganyika.

Imagine fedha za Uviko kiasi walichopata ni karibia mapato yao ya mwaka mzima.

Wakienda kwenye mfumo wa EU kesho na keshokutwa watataka watoke kwenye Muungano kisa wameshindwa kuchangia uendeshaji wa serikali ya pamoja.

Bila shaka kina Zitto wanapiga zomari kwa wimbo wasioujua, au wanaujua ila wanafanya siasa za hadaa.
Wao wanasema Mapato hayakui sababu ya muungano. Mfano wao wanataka benki za Zanzibar ziwe kama za visiwa vya Jersey, Curacao, Seychelles ambako Kuna sheria rafiki za Kodi Ili wanaotunza mabilioni wakayafiche huko!!

Sasa wanasema wanashindwa kuweka sheria hizo rafiki sababu masuala ya fedha na kodi ni ya muungano!!

Wanasema pia Mapato hayakui sababu muungano hauja factor in kuwa Zanzibar ni service-sector based economy. Kwa hiyo ilibidi flexibility kwenye sheria za Kodi, fedha, uwekezaji n.k Ili yaendane na nature ya Zanzibar ambayo Haina rasilimali kma za bara.

So kwa hoja hizo according to Jussa Ladhu ni kwamba kwa mamlaka huru wataweza fikia hizo targets kuliko kwa Sasa ambako ni kama wilaya tu hivi ya Tanganyika.

Kuhusu ukubwa wa nchi mbona Nauru au Gambia Ina kura Moja UN sawa sawa tu na ma-nchi makubwa kama India!! So ukubwa inaweza isiwe challenge kama muundo uko well defined.
 
Back
Top Bottom