Uchaguzi 2020 Adam Mchomvu ampiga mtama Emmanuel Mbasha stejini kwenye tamasha la CCM uwanja wa Uhuru

Uchaguzi 2020 Adam Mchomvu ampiga mtama Emmanuel Mbasha stejini kwenye tamasha la CCM uwanja wa Uhuru

Huyu jamaa kaacha maswali mengi ukichukulia ni mtu wa Arusha kule inakotoka CHADEMA.

Alikuwa na nia ya kuchafua tamasha la CCM ? Maana sasa tamasha halijadiliwi, linajadiliwa tukio hilo tu?

Kwa nini baada ya tukio alisifiwa sana na makada wa CHADEMA?

Ccm ndio wajilaumu kwa kulazimisha kupendwa, mpaka wamejikuta wanaanza kampeni mapema.
 
Matope,
Reaction ya Adamu haikuwa sahihi kwa namna ambavyo tukio lilikuwa likionyeshwa katika media nyingi tena moja kwa moja,naungana na wewe kusema kwamba Adamu ndio kajishushia heshima kwa kitendo kile huku Mbasha akionyesha ukomavu kwa kujikausha.

Sijui aliambiwa nini sekunde za mwisho ambacho hatukukisikia kwa maana ile 'unajua wewe bangi sana',ni msemo wa kawaida ambao hata tusio tumia huambiwa na naamini Adamu anaujua vizuri.

Adamu kajiharibia sana,kuna deals naamini zitamkimbia kwa ile tabia ya ajabu mbele ya kadamnasi,Mbasha nae inabidi akue na kuacha shobo zisizo na msingi(naamini Frola alimkimbia kwa mengi sana tusiyoyajua).
Kabisa. Huo msemo mbona hata mimi huwa naambiwa na sijui hata bangi inafananaje
 
Wakuu,

Jana tumeona Mtangazaji Adam Mchomvu akimpiga buti Bwana Emmanuel Mbasha Jukwaani, kama vile haitoshi, Adam akamfuata Backstage na kutaka kuendelea kumpa kichapo.

Hii ni Baada ya Mbasha kumusema "Adam unajua wewe Banghe" sana Jukwaani.
Kitendo kile cha aibu na kihuni kimetokea kwenye tukio lilirotabiwana Chama cha Mapinduzi CCM

Sio Ustaarabu na wala sio Maadili ya ki Tanzania Mtu kumuita mwenzake Banghe Kwenye kadamnasi, yaani unamuita Mwenzako anatumia mihadarati, tunajua Banghe ni haramu kwa Sheria zetu,na iko kwenye category ya Madawa ya Kulevya.

Pia Kitendo cha Adam kumchapa Mbasha pia ni cha kihuni na ni jinai,japokuwa ni dhahiri alikuwa provoked na Mbasha.

Kama Wananchi wenyeMapenzi Mema na Taifa letu, Tunamtaka Msajili wa vyama vya Siasa kukiandikia Chama cha Mpinduzi Barua kuonesha na kukuchukulia hatua kali za Kinidhamu kwa tukio la Jana.

Tunajua ingekuwa ni CHADEMA tayari Msajili angeshatia neno
 
Yaani aibu sana, chadema sehemu mbalimbali nchini wameanza kutumia kiashiria cha ngwala kwamba katika uchaguzi watawapiga ngwala CCM kama mbasha alivyopigwa na Mchomvu
Kwani mmetetemeshwa ?
 
Kwa nini asilaumiwe yule shost aliyemchokoza? Wacheni kuisingizia Chadema kila mnapoharibikiwa. Yule fala ndiyo maana ngwaji alikuwa anamtafunia mkewe
He he he! Ngwaji alitafuna kondoo? Huyu huyu mgombea wa Kawe?
Yaani sifa kuwa ya maccm ni kutafuniana, hasa wale viherehere wanatafuniwa hakuna mchezo
 
Boonge la USHAMBA kwa wote wawili ![emoji849]
Mshamba ni yule aliyemwita mwenzake Bangi kwani kiuhalisia toka moyoni mbasha ni ccm damu lakini Adam siyo ccm damu kaamua tu kuvaa shati la ccm kizushi
 
Mkuu Kwa hiyo wewe unakubali kuwa kuna Jambo la aibu limetokea ila utaona sio kitu, ile ni aibu kubwa Mkuu, ni Aibu Ya Karine na kuna Jambo la MUNGU hapo ni ishara kuwa MUNGU hana Baraka na udhalimu unaofanywa Ndugu na huenda kukaja kutokea Jambo baya zaid na kupelekea hali ikabadilika watu wakaachwa midomo wazi, Mkuu MUNGU anambinu zake zakuwwadhibu watu wanaojificha kwenye pesa na kwenye bunduki za umma

Joyce acha basi mawazo ya kijinga aisee. Yani watu kupigana kwa sababu ya akili zao wewe unahusisha na Mungu? Unafikiri kama ingekuwa Mungu hapendezwi angefanya kitu cha kibinadamu hivyo? Ingekuwa jukwaa limeanguka ghafla, au kupiga radi, upepo mkali, basi hata vifaa kutofanya kazi bila sababu hapo tungeona mawazo yako yana maana, sasa mchomvu kupigana na mbasha na unajua fika wote ni walevi wale, we unasema eti kuna jambo Mungu kaonyesha, kha!
Hata kama ni imani, hiyo yako ni ya kinyumbu kabisa
 
Back
Top Bottom