Adha kubwa tuipatayo abiria tunaosafiri na mabasi ya mikoani

Utaratibu ulikuwa basi kuingia stendi kwenye mji ambapo abiria watachagua mojawapo ya hotel zilizopo karibu kupata huduma ya chakula. Huu utaratibu wa kuingia kwenye hotel iliyojengwa porini naona ni utaratibu mpya ambao mamlaka itabidi ziukemee...
 
Suluhisho hapo ni kubeba chakula chako cha njiani.
 
Huyo mama ulimsaidiaje na watoto?Hicho ndio cha msingi utuambie maana hata mimi roho imeniuma!Ila mimi nikiona watoto nanunua chakula kama nina uwezo kwa siku hiyo.Nakumbuka nilikuwa naenda songea,kufika Tunduru dogo mmoja akaomba nimnunulie msosi tulikuwa naye kwenye basi,ikabidi nimnunulie!Ila chakula Tunduru ni kichafu sana!Nakumbuka kuna siku nilinunua korosho nikawa nakula nikamgaiya na jirani yangu,mdada hivi,nilijuta saana yule dada alitapika saaana mpaka nikaogopa nikajisemea hapa nakamatwa kwa kuhisiwa najaribu kumlewesha nimuibie.
 
Hahahha mimj niliwahi kununua keki Masasi aisee nilipokula moja kwanza ladha yake mbaya kishenzi kufika Tunduru haraka sana chooni toa uharo wa hatari mpaka nafika Songea nikawa nimeshakoma
 
Mkuu ili mradi cha moto kwangu fresh ukimchunguza sana bata hutamla.

Nb:Ni lazima chakula kiwe cha moto
Kaka jiongeze. Huo mshkaki wa jero sio kabisa. Ingekua sehemu yanye mifugo mingi ningekuelewa
 
Kwa dhuluma zao ndio maana utagundua kuwa hizo hoteli nyingi huwa zinakufa baada ya muda mfupi,usicheze na Mungu hata kidogo...
 
Sijawahi kula njiani pindi nipo safarini, hiyo adha hainihusu.
Ila kuwe na ustaarabu ktk hili kunaumiza abiria wanyonge.
 
Kuwa kama wapare .... wakifika liverpool wanatoa Makande yao kwenye Hotpot na kujisevia kwa gharama sawa na Bure [emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] lol
 
Kama ni wewe tu ndo ulishindwa kula bas nakushauri siku nyingine ubebe makande yako mkuu usije kufa njaa wahudum wa bus wao wanapewa posho kwenye hzo sehem na wanapewa chakula maji bure
Si rahisi kubadilika ikiwa Wengi wanakula hayo maeneo na wachache pia mnanunua soda Ni bora mgome wote ndo watabadilika
 
Kweli kabisa basi Vyakula viwe Graded ili kila mtu aweze kumudu kwa Kipato chako.
Wale matajiri wale pakitajiri ambao wengi wao ndo wako humu JF.
Maskini Kama sisi tutakula vya Buku 3000 Afu mbele.
 
Sijawahi kula njiani pindi nipo safarini, hiyo adha hainihusu.
Ila kuwe na ustaarabu ktk hili kunaumiza abiria wanyonge.
Tunaobebaga eet som more na kusubiri soda za kwenye bus haya hayatuhusu.
 
Kweli kabisa basi Vyakula viwe Graded ili kila mtu aweze kumudu kwa Kipato chako.
Wale matajiri wale pakitajiri ambao wengi wao ndo wako humu JF.
Maskini Kama sisi tutakula vya Buku 3000 Afu mbele.
Ubaya hata hawakubali kukuuzia chips kavu.
Sambusa buku, soseji imesinyaa buku yani pale Liverpool na kule Hill ni majanga kwa Dar Arusha.
 
Tamaa tu Mafinga niliuliza Sambusa nikaambiwa Buku nikageuza japo mfukoni nilikua na hela ya kutosha nikampigia simu jamaa angua aninulie wali pale Iringa mjini kuna mama anapika wali samaki mzuri kishenzi akaniletea ipogolo.
Kwa Dar - Songea VIA lindi kupo vizuri ktk suala la bei ya vyakula,. tatizo lipo VIA Moro, pale mafinga na kitonga comfort, uwiiii bei ghali afu vyakula venye vya juzi aaaah. Kero tupu.
 
Mimi huwa napenda sana kusafiri Mchana ,kuna siku nilikua naenda zangu Njombe nikatoka na Upendo ya Mafinga kwenye saa asubuhi nafika Morogoro kabla ya msamvu kuna hotel hapa nyuma chuma ikaingia pale kaah hako kawali na nyama cha buku 5 dah jau kishenzi nilisonya tu.

Sehemu nyingine Doma nao wana bei vyakula vyao kiufuli hiyo njia imeoza kwa tamaa na ukiangalia ni njia kuu ya vyakula basi tu.
 
Tamaa tu Mafinga niliuliza Sambusa nikaambiwa Buku nikageuza japo mfukoni nilikua na hela ya kutosha nikampigia simu jamaa angua aninulie wali pale Iringa mjini kuna mama anapika wali samaki mzuri kishenzi akaniletea ipogolo.
Me nikiwa nasafiri kutoka Dar kwenda Songea au Songea kuja Dar huwa sipati shida, maana nina matatizo yangu binafsi sili chakula njian, hiyo adha hainikuti huwa nawaonea huruma abiria wanyonge.
 
MIE huwa nakulaga matunda basi,maji, Katanga,korosho ama na biscuit kidogo. Huko kwa mahoteli najisaidia tu. Nawauliziaga being naishia kuwaambia kuwa mbona mnauza kama vile mnauzia watalii amani au kama mko mgodini vile.
Eti ninunue wali alfu 5 jamani na humu kilo moja ni buku kwa hapa Mza.
 
Songea sehemu gani unaendaga?
Me nikiwa nasafiri kutoka Dar kwenda Songea au Songea kuja Dar huwa sipati shida, maana nina matatizo yangu binafsi sili chakula njian, hiyo adha hainikuti huwa nawaonea huruma abiria wanyonge.
 
Dereva akiingiza gari hotelini kwanza yeye na staff wenzake wanakula chakula na vinywaji bure na wanapewaga posho(allowance) inategemea na makubaliano yao wengine wanalipwa kila wakileta gari, wengine kwa wiki na wengine kwa mwezi

Ni noma jombaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…