Adha kubwa tuipatayo abiria tunaosafiri na mabasi ya mikoani

Adha kubwa tuipatayo abiria tunaosafiri na mabasi ya mikoani

Tengeneza chakula chako nyumbani, kifunge vizuri, utakula popote, muda wowote.

Mimi huwa nafunga ugalo wa LOYE
Yani unaanza safari na mahotpot ya kutosha kwani unahama? Ujikute una watoto watano, Swala hapo serikali ingilie kati
 
Hivi mleta mada lengo lako huwa ni kusafiri au kula njiani hotelini? Naona kula umekuvalia njuga kama ndio lengo lako kuu la kusafiri. Kwenu huwa huli au?
Mleta mada ana hoja yenye mashiko, kwani wasafiri ni watu wazima tu kuwa wanaweza vumilia njaa, matazamio makubwa ni kwa watoto si jitu kama wewe na mindevu kama kambale
 
Kabisa mkuu. Hoja yako ina mashiko sana. Hawa wamiliki wa hizi sehemu za chakula wanaibia pakubwa sana abiria. Vichips vya 5,000 huwezi hata kushiba. Mshikaki wa 5,000 hata haufanani na hiyo bei. Bei zao zimekaa kuwaumiza abiria. Wanafanya hivyo wakijua lazima ule tu kwa sababu huna sehemu nyingine ya kwenda kula. Serikali tafadhali wasaidieni hawa wanyonge.
Wew safarini unataka ushibe ili uanze kutusumbua sisi madereva tusimamishe gari ili uende haja kubwa ?
 
Hivi zile dakika 10 mbona ni za mchaka mchaka sana unaweza ukala bila mvurugono wa tumbo kwa wale wanaonunua wali au ugali, angalau wa chips na ndizi roast unachukua unaenda kukaa nacho kwenye bus
 
Utaratibu wa Mabasi kuingia Hotelini umekuja miaka ya karibuni wakati Waziri Mwawasiliaoni na Uchukuzi akiwa Mwakyembe
alizuia kuchimba dawa popote tu basi linasimama
pia kulizuka wizi hasa mabasi yakisimamam stend kuu,wezi walikuwa wakiingia ndani km abiria na kushuka na mabegi abiria wanapokuwa wakila Hotelini huko mitaani
Ndipo wakaiga baadhi ya hotel zinazolisha abiria zikiwa nje ya mji
Faida waliyoiona ni huduma ya choo huwa ni bure kwa hiyo utalipia kwenye chakula,
na wale wote wanaofanya biashara hapo wanamlipa mwenye Hotel
Juzi Rais JPM amepiga marufuku uuzaji wa bei juu chakula hicho, karuhusu abiria wanunue popote wasilazimishwe Hotel hizo, sasa hapo dereva anahusika bado kuzichagua Hotel hizo
 
Hii imetulia meku
 
Ndio maana mimi usafiri wangu ni hakuna kulala japo nasikia kuna kampeni ya kuyapiga marufuku.
 
Uwe unafiri na package yako ya msosi,,hizo hotel zilizoko point of no return,mara nyingi utauziwa hata kuku wa juzi,anawekwa kwenye microwave tu,,utaharisha sana,
Madereva kila wakipaki hizo hoteli analipwa chakula of his choice na tsh 10,000.
 
Kesho nasafiri,nanunua mbuzi nusu kg aliyechomwa.Mbele kwa mbele ntanunua chips kavu,nyama ndo hupandisha bei
 
Back
Top Bottom