Yesu hajawahi kuchinja mtu katika uhai wake duniani!Husipende kupotosha na kupindisha ukweli kama Shetani Ibilisi! Ni wazi Yesu aliongea kwa kutumia mifano na illustrations. Katika Luka 19:12-27 Yesu aliongea hiyo story kwa mfano siyo uhalisi.
Soma kuanzia Luka:19.12-13
Basi akasema, Mtu mmoja, kabaila, alisafiri kwenda nchi ya mbali, ili ajipatie ufalme na kurudi.13 Akaita watu kumi katika watumwa wake, akawapa mafungu kumi ya fedha, akawaambia, Fanyeni biashara hata nitakapokuja.
Ukisoma kuanzia Luka 19:12 na 13 inaonyesha huyo kabaila alikuwa ana fedha, watumwa na alikwenda kujipatia ufalme. Yesu hajawahi kuwa na mapesa ya kugawa, kuwa na watumwa wala kuchukua mtu yeyote kulingana na Luka 19:27.
Luka:19.27
Tena, wale adui zangu, wasiotaka niwatawale, waleteni hapa mwachinje mbele yangu.
[emoji115]
Hayo hayamaanishi kwamba Yesu ndiye aliyechinja ila anazungumza kwa kutumia mfano wa huyo kabaila, kwamba kama ukishindwa kwa kutokufanya kazi ili kuongeza utajiri wa ufalme wa bwana, basi watumwa watakuwa ndiyo losers.
Mfano huo unalenga Mitume ambao wanategemea kuwa watawala na Yesu katika Ufalme wa Mungu. Kwa kutokufanya kazi ili kuongeza utajiri wa ufalme wa bwana, watumwa watakuwa ndiyo losers. Mitume wa Yesu walikuwa wanategemea ufalme wa Mungu chini ya uongozi wa Yesu. Hivyo kama hawafanyi bidii hawatokuwa na mahala pao katika ufalme.