Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Mbunge Ado Shaibu Ado alipiga simu Waziri wa Maji Aweso wakati wa mkutano na wananchi katika kijiji chake ili kuwasilisha changamoto kubwa za maji.Wananchi walikuwa wamelalamika kwa muda mrefu kuhusu maji machafu yanayotolewa kwenye visima, hali iliyowafanya kunywa maji yasiyo safi.
Waziri Aweso alikuwa ameona pia malalamiko hayo mitandaoni kutoka kijiji cha machemba, ambapo raia walionesha kisima wanachotumia kwaajili ya maji kikiwa na maji yaliyochafuka.
Kupitia simu hiyo iliyosikika hadharani, Waziri Aweso aliahidi kwamba serikali haitaruhusu wananchi kuendelea kutumia maji machafu. Alisema atatuma timu ya wataalamu kutoka wizara kufanya utafiti na kuchimba visima vya dharura ili maji safi yapatikane haraka.Alisisitiza kuwa maji ni suala nyeti na hatua za dharura zitachukuliwa bila kuchelewa.
Pia soma ~ Wanakijiji wa Machemba - Tunduru wamwambia Ado Shaibu kuwa hawana huduma ya maji safi
Baada ya majibu hayo, Mbunge Ado Shaibu Ado aliwashukuru Waziri na Mwenyezi Mungu. Alisema suala la maji limetatuliwa vizuri na sasa serikali itatoa suluhisho za kudumu. Hata hivyo, aliahidi yeye mwenyewe, kupitia mfuko wa jimbo au mchango wake binafsi, atawanunulia wananchi pampu (mota) ili waweze kupata maji mara moja bila kungoja.
“Mambo yanayowezekana tutayamaliza wenyewe hapa hapa. Yasiyowezekana tutasubiri kidogo,” alisema Ado huku akiwataka wananchi kuvumilia.
Mkutano huo ulifanyika katika kijiji cha ngapa ambapo kilihudhuriwa na umati mkubwa wa wananchi waliokuwa wakisikiliza kwa makini.