Afande Sele atashtakiwa kwa kosa gani baada ya kumtukana Mungu?

Hivi ikitokea afande sele ,akatubia na kuomba msamaha kwa mola wake ,na wakamalizana kimya kimya,itakuweje na hao mashekh?

kilichopaswa kwa hawa mashekh ,ni kumlingania na kumweleza makosa yeka ,

kuna mtu alikufuru kama firauni mpaka kujiita mungu,ila mbona hakuombewa kifo?

watu wasichojua mungu ni wetu sote ,wema na waovu ,mungu huyo huyo ,na pia hata huyo muovu anaweza akamrejea mungu wake mpaka hamtaamini ,ebu warudi kwenye Tarekh(historia) ya wema waliotangulia ,wote walitokea kwenye uwovu ,

mtume alipigwa mawe twaif ,lkn hakuwaombea dua mbaya ,bado alikuwa na matumaini huwenda katika hao walompiga mawe atazaliwa wema katika wao ,

Ni vyema mashekh wapunguze jazba na mhemko ,na wawe viongozi wa kuwaongoza watu wanapopotea kabla ya kuhukumu ,bora wangemwita ama kumnasihi na kama angekataa au kupinga labda hapo wangekuwa na pakuanzia ,

mtu hujamwita hujamwelimisha au kumweleza kosa lake ,maana huwenda yeye akawa anajiona yuko sawa kwa mujibu wa imani yake ,

TUSIPENDE KUADHIBU ,MTOTO HAFUNDISHWI KWA KUMCHAPA BILA KUMWAMBIA KOSA LAKE ,MWELEZE KOSA LAKE ,MPE NAFASI YA KUJISAHIHISHA KWANZA NA KAMA ATAREJEA MAKOSA HAPO SASA MNAPO PAKUANZIA
 
Mbona mange hakufa alivosemewa Dua baada ya kumtukana shekh,,

Watu wengin hovy Sana wanajikuta wao ni wema Sana mbele y Mungu,,
Shame on them
 
Afande Sele kajificha msituni
 
Kwani c waache Mungu ahukumu mwenyewe
Kwani yeye Mungu hajasikia jinsi jamaa kamtusi au ndo mtajifanya chawa wa Sir God
 
Heri Hata ng'ombe kuliko binadamu mnafiki mkuu 🤣🤣🤣
 
Mungu wapo wengi.. Mungu yupi Sasa ametukanwa
 
😳 Ni nini?
Hayo ni maombi tu kama maombi mengine. Yaani ni dua tu.

Mwenyezi Mungu anazo namna tatu za kujibu maombi ya kila mtu.

1) Ok
2) Ok but not now
3) No, Because there is a better plan for you than what you are praying for.

Kwahiyo huyo sheikh Kishki nadhani ni hasira tu zilimzidi. Ipo ruhusa sisi waislam tumepewa ya kumuombea mtu majanga ikiwa huyo mtu amepitukia mipaka na pengine sheikh Kishki ametumia mwanya huo, ingawaje ni kheri na bora zaidi kuwaombea waliopotea uongofu ili waongoke pia.

Na Allah anajua zaidi.
 
Kila siku tunajifunza, nilikua sijui kama unaweza ukamuelekeza Mungu jinsi ya kumuhukumu mtu.
 
Huyu ni nabii sio Msomali
Jambo kuu kabisa linalosababisha chuki ndani ya jamii za watu in specific in Tanzania ni udini.

Kama hujui mambo ya watu kwa nini ujisemee tu?? Ni nani kakwambia kwenye Uislam kuna manabii zama hizi?? Unabii kwetu ulishakoma tangu kipindi cha Mtume Muhammad rehma na amani ziwe juu yake.

Refrain from doing what you are not sure of, that is much better for you if you know!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…