Asante Profesa Jay, Majani na Ulamaa
Mmegusa nnapo’pataka
Name kwenye mtazamo’ na jambo nataka’ kuweka
Maana kila kukicha ma-emcees wanaongezeka
Nasema very nice!
Yes! Rap kama dhehebu
Wingi wa wasanii’ inaonesha ni dini swafi
Yaani imekubalika’ waumini tuko wengi’
Lakini bado na shaka’ sijapata uhakika
Wote tumesadiki?
Au wengine ni feki’ mmetumwa kama mamluki
Manake hamna maana
Maana mna rap na (?)
Mistari imekosa vina’
Yenye vina’ haina maana
Na kila mnapokaa
Mnapenda kusengenyana
Mnapenda kutetana na’
Mnapenda kulumbana
Mimi naogopa sana’ kwa jinsi ninavyo elewa
Mwishoni mtatukanana
Ama inawezekana’ mwishoni mkaja chinjana
Na wote tuna rap tuonekane’ hatuna maana
Wapi ilipo Taarabu? Ilikuja kwa kishindo hata wagumu walishaihusudu
Kwa ajili ya malumbano’ mwishoni ikafa kibudu
Shabiki piga simu’ changia mawazo yako, ni nani tutamlaumu?
Nani tumchune ngozi? Prodyuza aliyerekodi?
Ama labda DJ anayeipiga kwenye kipindi?
Wengi wanaipenda rap
Japo rap haiwapendi
Waungwana’ wanaicha
Wapumbavu hawa ambiliki
Hivi kwani lazima tuwe wote wanamuziki?
Mi nadhani ingetosha wengine mmbaki ushabiki
Huu ni wangu mtazamo
Masela’ msijenge chuki