Afande Sele hafahamu kuwa miradi iliyotekelezwa na Rais Samia kipindi hiki ni mingi kuliko wakati mwingine wowote?

Kuna wanafunzi walikuwa wanafaulu lakini wanabaki majumbani kwa kuwa tu madarasa yalikuwa hayatoshi na wengine kwenda muhula wa pili unapoanza Hadi watoto wengine wa kike walikuwa wanajikuta wanaolewa au kupata ujauzito wakiwa bado wapo majumbani mwao na kuishia kukatisha ndoto zao za Kuendelea na masomo
Kwamba walikuwa wanaishi huko watu saiv madarasa ndo wanasoma na huko nyuma walikuwa hawasomi? Umetumwa wewe
 
Watanzania wanataka barabara nzuri za juu na chini, wanataka reli ya kisasa, wanataka huduma bora za afya na elimu bure, wanataka mbolea na mafuta kwa bei nafuu, hapo bado wanataka na ajira yenye mishahara minono na wale walioajiriwa na Serikali wanataka nyongeza mara dufu, lakini hawataki kulipa kodi wachangie.

Cha kushangaza pia hawataki Serikali yao ikope kwa ‘mabeberu’ hawataki pia tupewe misaada, wanataka tax base ile ile iendelee kuhenyeka kuwapa yote haya, hata kodi kama withholding tax on rent ambazo zilikuwepo miaka nenda rudi bado watu waliopangisha majumba hawataki kulipa wanataka walipe walewale wa siku zote alafu wenyewe waendelee kufaidi. Mambo ya ajabu sana.
 
Ni kweli zipo shule zimejengwa na madarasa yameongezwa lakini sio hela za tozo ni pesa zilizotokana na mkopo/msaada kutokana na COVID sasa wasitake kutuongopea sisi ni watu wazima

Asante
 
Huyo mvuta bangi muda huu ilitakiwa awe central police , Ni mchochezi
 
Hao Watanzania wanaomshangaa Sele ni wa wapi!!!??? Nchi hii ina vijana wa ovyo sana, eti na wewe umeanzisha uzi!!!?? Aya, kachukue buku 7 yako.
 

Watanzania mnawapenda wakati wa kulipa Kodi ila wakidai mambo yao mnawaona hawana maana. Watanzania hawakatai kulipa Kodi Bali hawataki tozo za michongo.
 
Acha upumbavu we kiumbe......
 
Mtu akisoma replies za hii thread ataelewa fika watanzania wana hasira na hawataki ujinga tena, wameshachoka siasa za bei rahisi. Wanataka siasa zenye tija, na kiongozi aliyepo keshafeli kwenye kigezo hicho.
 
Angalau kidogo hapa umeandika, huko kwingine ni TAKATAKA tupu!
 
Panapohitaji maboresho patarekebishwa lakini wajibu wa kuijenga nchi yetu utabakia mikononi mwetu Watanzania.
Ikiwa kweli tunataka kuijenga Nchi kwa pamoja....ni wajibu kufunga mkanda kwa pamoja,kuanzia Kiongozi Mkuu wa Nchi mpaka raia wa mwisho.
Kadhalika,tunahitaji kuwachukulia hatua kali kila mwizi kikamilifu tena bila kificho.

Ila kwasasa
Tunaona kinyume,wakiongezeana posho za safari,wakiendesha magari ya gharama,wakiiba kwa msemo wa kila mbuzi ale kwa urefu wa kamba yake.............

Chief...kuwa makini
 
Nashukuru ndugu yangu, Naomba utambue kuwa Mh Rais wetu Amekuwa na mtizamo huo wa kutaka kuona kuwa kuanzia viongozi mpaka mtanzania wa kawaida tunaishi katika maisha yanayofanana na uchumi wetu, anataka kuona kuwa katika wakati huu wa ujenzi wa Taifa tunajibana kwa kadri ya uwezo wetu huku shughuli zote za kumgusa na kumpunguzia mtanzania mnyonge kero zinafanyika, Tozo na Kodi zetu haziendi katika kununua magari ya kifahari Bali kutatua kero kwa mtanzania
 
Hatua zinachukuliwa kwa uharaka Sana Mara tu inapobainika kuwa mahali fulani pana harufu ya ubadhilifu wa fedha za umma, lakini pia Ni jukumu letu wananchi kutoa taarifa pale tutakapokuwa na mashaka Napo juu ya matumizi ya Fedha zetu, mtu unaweza kutoa hata kupitia jukwaa Hili na viongozi wetu naamini watapata ujumbe, maana tumeona Mara nyingi mijadara ikitokea humu na kuilazimu serikali kutoa ufafanuzi, lazima Tuwe na uchungu na jasho letu kwa mtu anayetaka kuchezea nguvu zetu za pamoja
 
Panapohitaji maboresho patarekebishwa lakini wajibu wa kuijenga nchi yetu utabakia mikononi mwetu Watanzania.
Na viongozi pia wanahuo wajibu. Wao wanatakiwa kupunguza matumizi. Sio kungojea kila toleo la v8 wanunue. V8 moja ni shule nzima na chenji inabaki.
 
Ndugu amka!! Unatetea mabandiko yao hutaki kuona matendo yao. Siasa inataka raia aamini lakini walioaminiwa wanaenda kinyume na walioahidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…