Afande Sele: Magufuli alikopa na kufanya makubwa, sasa hivi wanakopa na hakuna linaloonekana

Afande Sele: Magufuli alikopa na kufanya makubwa, sasa hivi wanakopa na hakuna linaloonekana

Watekelezaji nani kawateua?
Wako chini ya Mamlaka ipi?
Yeye mwenyewe kupitia washauri wake,lakini haohao washauri wake,labda wanafanya kolabo na wateuliwa,matokeo yake,wanamhujumu MAMA.
 
View attachment 2351368

"Unajua kwenye each one teach one hatupingi mikopo, lakini tunapinga aina ya mikopo na kile ambacho kinatumika kupitia hiyo mikopo. Yaani, hiyo mikopo ina impact gani kwa wananchi inayoeleweka. Ni kama vile wewe umeenda kwa bwasheee kukopa unga au mafuta kwa sababu watoto wako wale"

"Sasa wewe unakopa halafu watoto wako bado wanakaa na njaa, sasa wewe umekopa ya nini? Tunasema nchi kubwa zinakopa, Magufuli alikopa, lakini Magu alipokopa tuliona. Miradi ya kimkakati mikubwa alijenga, mipya akaianzisha, ya zamani akaiboresha, ma reli yaliyokufa miaka na miaka yanayoenda huko Arusha kayafufua, reli kigoma inaishia Dodoma kaifufua mpaka Dar es salaam, akajenga na reli mpya, miundombinu ya umeme akaanzisha na mambo mengi mengi alifanya kwa muda mfupi aliotumikia nchi hii."

"Ko tunasema, ok alikopa lakini alifanya hiki. Ila kwenye kukopa kwake pia Magufuli hatukuona tozo zikiongezeka, hatukuona makodi ya ajabu ajabu, yaani tuliona kwamba mambo yanakwenda hata kwenye kipindi cha CORONA, kipindi kigumu dunia nzima imefungiwa ndani yeye bado aliendelea kupambana."

"Hatukuona matozo wala makodi ya ajabu yakiletwa nchi hii"
Kila siku nawambia ukitaka kuongoza Nchi zenye wajinga wengi piga Pini mdomo mdomo..

Mjinga unampa uhuru? Si unaona huyu anaongea utadhani hiyo miradi ya Mwendazake aliimaliza au alikopa akafanha ikaisha on time..
 
Mkuu kumbuka kuna kurudisha mikopo. JPM alikopa mikopo ya kibiashara ya muda mfupi na riba kubwa. Sasa hiyo mikopo inatakiwa kurejeshwa na miradi yoote mikubwa aliyoanzisha kuanzia ununuzi wa midege, SGR, bwawa la umeme n.k hakuna hata mmoja umeweza kurudisha hata shilingi. Mambo siyo rahisi kama tudhanivyo.
Hata alipokopa,miradi ilimalizika?
 
Huyu jamaa ametumia nini hadi bange hazina uwezo tena wa kiathiri ubongo wake?

Mbona kasema ukweli mtupu?
 
Kwamba wakati jpm anaingia aliikuta reli ya kigoma imeishia dodoma na yeye ndo akaileta dar es salaam?!!!! Nilikuwa sijajua hili.

Sijajua afande sele ana nini na baadhi ya marais fulani fulani hivi maana nilishawahi kumsikia katika mahojiano ya radio kipindi fulani hivi (kabla jpm hajafariki) akimponda mno kikwete. Alikuwa anasema kuwa kikwete hakufanya lolote katika kipindi chake na kwamba jpm aliikuta nchi ikiwa haina mradi wowote ule na hivyo kila mradi alioufanya jpm ameuanzisha mwenyewe. Leo anasema jpm aliiendeleza vema miradi aliyoikuta. Sasa sijui miradi ipi na sijui iliachwa na mkapa au nyerere?!!!!

Alipofariki jpm, afande sele ni mmojawapo kati ya watu kadhaa wachache waliofanya jitihada za kutaka kuiaminisha jamii kuwa jpm aliuawa, na bila aibu, huruma wala shukrani alimlenga kikwete moja kwa moja.

Leo amemvaa mama, akisema hakuna mradi wowote unaoendelea. Anayasema haya huku tulio binadamu wa kawaida (tusio na chuki, hila, ukanda au udini) tunajua, kusikia na kuona maendeleo ya miradi km madaraja (eg wami linafunguliwa hivi karibuni, lile la iringa etc); viwanda vinaonekana na kuendelea kujengwa; mabarabara; hilo bwawa walilokuwa wanajifichia haters ukweli umeanikwa live kuwa limeendelea hadi 67%; mashule maalum (ukiacha haya madarasa yanayoongezwa) yanajengwa mikoa mingi tu n.k. Tatizo la tozo (ukweli na kuelewa vs uwingi na ukubwa wake) lipo lakini ni vipi linamfanya afande huyu adanganye?!!!!!! Ni dhahiri ana kitu, very unhealth, na baadhi ya maraisi.

Sijajua chanzo cha hili ni nini au inawezekana kule kubadilika kwake kumemuathiri maana nasikia alibadili na siku hz ni mlokole................
 
Kwamba wale watu laki 5 waliokufa kwa korona kule marekani nao waliamin ushirikina?
Hao walikufa vifo vya kawaida kama ambavyo mpaka leo watu wanakufa. Ila Jiwe alikufa kwa laana ya Watanzania.
 
Kwamba kina Makamba kuzungukuza huku wakigawa Majiko ya Gesi na Bungeni kusimamisha shughuli ili kusifia Royal Tour unaita nini kama sio Propaganda ?!!!

Kila mgeni aliyekuja baada ya ile tamthiliya alihusishwa na Royal Tour..., If that's not Propaganda tell me what Is !!!, Kina Afande Sele na wengine tunao-criticize ndio tunaitakia mema nchi bila kusema hiki hapana walamba asali wanaweza kuona ni sawa...
So tatizo lako wewe ni kukosa mrija wa kulambia asali, enzi za mwendakuzimu ulikuwa kimya
 
Sawa, kwaiyo Iyo mikopo imeanza kulipwa baada tu ya mama kuingia madarakani????

Kama sivyo, Jpm aliwezaje kuendesha nchi bila tozo huku akiendelea kulipa mikopo yake ya kibiashara yenye riba kubwa?????

Juhudi kubwa ambazo Jpm aliwekeza ni ukusanyaji wa kodi na sote tuliona ambavyo hakukuwa na masihara kwenye hilo,

Sasa hivi ulipaji wa kodi umeshuka wafanyabiashara wengi hawalipi kodi.
Tatizo lako wewe kubwa ni usukuma gang
 
Amna mtu aliyeporwa pesa yake, ila walinyang'anywa pesa ya serikali.

Wewe uliporwa sh ngapi???
Mbona nchi hii ina machizi kiasi hiki! So hujui kuwa watu walikuwa wanaporwa pesa zao kwa sababu wewe hukuporwa?
 
Huu ni uongo kabisa. Kwamba hakuna kinachofanyika tangu mwezi March 2021 hadi hii September 2022? Huu ni upotishaji mkubwa!
Toka mungu afe sukuma gang mmechanganyikiwa kabisa
 
Back
Top Bottom