kamilisha habari.
Hii tabia ya kugombania magari na siti za kukaa kwenye daladala au costa inapoingia stendi au popote ni tabia mbovu sana.
kuna siku tulikuwa pahala tunasubiri gari aise!!!! ilipoingia watu wanakimbizana kwa nguvu zote na kugombania waingie huku gari ikiwa bado ipo kwenye mwendo, afu ni kundi kubwa la watu.
nilikaa pembeni nikatafakari na kujiuliza sana maswali mengi. Yani hata itokee sasahivi niko stendi, siwezagi gombania magari, heri ukeshe kuliko kuumizwa vibaya au kufa kabisa.
Hivi mnapogombania gari likiwa kwenye mwendo ikatokea mtu kaanguka tairi ikampitia kichwani na ukute ni wewe itakuaje?
Hivi hatakama gari imesimama, ninyi mnaigombania, ukianguka ukakanyagwa na kundi la watu wote hao na ukute ni wewe itakuaje?
wakati mnakimbizana kupanda gari watu hutumia nguvu sana, mtu anakimbia huku anarusha mikono, ukapigwa ngumi ya uso na ukute ni wewe itakuaje?
haya mambo heri uwe mstaarabu kuepusha majanga. Kaa pembeni kabisa wanaogombania wasije wakakupamia, wasio waelewa waache wagombanie siku la kuwakuta likiwakuta ndo akili itawakaa sawa.