Afghanistan: Talibani imepiga marufuku wanawake kuongea ama kubadilishana mawazo. Marufuku mwanamke kuongea na mwanamke mwenzie

Afghanistan: Talibani imepiga marufuku wanawake kuongea ama kubadilishana mawazo. Marufuku mwanamke kuongea na mwanamke mwenzie

Nikiwa kama redpilled guy najua watalebani wanachokifanya na nnawaunga mkono kabisa.
downloadfile-5.jpg
 
Serikali inayoongozwa na Talibani nchini Afghanistan imepiga marufuku wanawake kuongea ama kubadilishana mawazo. Ni marufuku wanawake kuongea na mwanamke mwezake na kumuelezea mawazo ama maoni yake.

Khalif Hanif, waziri wa tabia njema na mwenendo mwema katika jamii amesema ni marufuku wanawake kuongea wenyewe kwa wenyewe kwa sababu ni kinyume na mafundisho ya kiislamu hasa ya Mtume na Allah. Mwanamke aongee na mumewe tu.

Kumbuka hivi karibuni Talibani ilipiga marufuku saluni za kike na za kiume na kutangaza kwamba ni marufuku kwa mwananchi wa Afghanistan kunyoa nywele na ndevu kwani ni kinyume na mafundisho ya kiislamu. Pia Talibani ilipiga marufuku wanawake kupiga simu redioni ama mwanamke kuongea sauti yake ikasikika public.

View: https://x.com/HabibKhanT/status/1850241627530424578?s=19

duh kwahiyo hata sokoni aisee.........haya watu na dini zao
 
Mnapata tabu sana kutafuta cha kuuchafua Uislamu

Viongozi wenu wa dini kila siku wanahalalisha mpigane miti wenyewe kwa wenyewe na nyie bado mnakosa haya na kuendelea kudanganya watu kwa propaganda za kutunga dhidi ya Uislamu!

(Quran 2:18) صُمُّۢ بُكۡمٌ عُمۡيٞ فَهُمۡ لَا يَرۡجِعُونَ
Deaf, dumb and blind – so they will not return [to the right path].
 
Ili uwe mwisalmu kamili inatakiwa uwehuke kwanza...

Haiingii akili eti mwanaume usinyoe ndevu ...si uchafu huo
Umeshahau, wamesema na nywele za kichwa pia zisinyolewe. Tusije shangaa siku kichaa cha dini kikipanda tena wakaagiza na nywele za Ikulu nazo zisinyolewe! Watakuwa wakifanya ukaguzi wa kushitukiza. Ole wako ukutwe na msitu eneo la Ikulu!

Ee Mungu tunaomba uiponye Afghanistan na ukatili wa hawa Majahili wa Taliban.
 
M
Hao talibani kuna mambo wanafanya ambayo sio katika sheria za kiislamu kabisa au kinyume na uislamu,kama mtu anauona uislamu kupitia talibani hakika hatapata uislamu sahihi,hao asilimia kubwa mambo yao kama wanaharakati

Uislamu haujakataza wanawake kuongea na wanawake wenzao na wala si sunna ya Mtume wala maagizo ya Allah. Wake za Mtume tu walikuwa wanaongea na wanaume nyuma ya pazia katika kuwaelekeza mambo fulani fulani ya dini,kama hiyo haikuruhusiwa je ilikuwaje wakeze wakafanya hivyo?

Kuhusu wanaume kunyoa nywele au ndefu wanaruhusiwa sana,ila si katika uislamu sijui kunyoa kiduku na stahili za ajabu ajabu,kama unaondoa nywele zote basi ondoa na kama unanyoa kawaida basi nyoa kwa heshima

Kuhusu kufuga ndevu hiyo ni sunna sio lazima kwa wanaume kufuga ndevu,ingawa ni bora kufuata sunna ya Mtume,binafsi nanyoa ndefu,sio agizo la lazima la dini

Kuhusu wanawake kwenda saluni,wanawake wanatakiwa kujipamba kwa ajili ya waume zao,wapendeze na wanoge,ila naona kuna namna labda hizo saluni zimeonekana ni sehemu ambazo kuna ajenda nyingine zinafanyika

Kuhusu wanawake kuongea kwenye redio au television,kwa mfano katika tv yapaswa mwanamke ajistiri anapokuwa hewani na si kuwa uchi kwa mujibu wa uislamu,kuhusu kuongea kwenye redio,hiyo hata huku Tanzania kuna redio moja Redio imani nayo kipindi fulani fulani walikataza lakini wakapewa hoja mbona wake za Mtume Muhammad (s.a.w) walikuwa wanaongea na wanaume nyuma ya pazia,kwahiyo hapo hoja nzito ilipatikana

Kwahiyo si kila linalo fanywa na hivi vikundi vyenye misimamo mikali ni uislamu bali mengine ni taratibu zao binafsi

Asante
Mimi ni mkatoliki ila nimekuelewa umeitetea dini kwa staha na heshima.
 
Back
Top Bottom