Hao talibani kuna mambo wanafanya ambayo sio katika sheria za kiislamu kabisa au kinyume na uislamu,kama mtu anauona uislamu kupitia talibani hakika hatapata uislamu sahihi,hao asilimia kubwa mambo yao kama wanaharakati
Uislamu haujakataza wanawake kuongea na wanawake wenzao na wala si sunna ya Mtume wala maagizo ya Allah. Wake za Mtume tu walikuwa wanaongea na wanaume nyuma ya pazia katika kuwaelekeza mambo fulani fulani ya dini,kama hiyo haikuruhusiwa je ilikuwaje wakeze wakafanya hivyo?
Kuhusu wanaume kunyoa nywele au ndefu wanaruhusiwa sana,ila si katika uislamu sijui kunyoa kiduku na stahili za ajabu ajabu,kama unaondoa nywele zote basi ondoa na kama unanyoa kawaida basi nyoa kwa heshima
Kuhusu kufuga ndevu hiyo ni sunna sio lazima kwa wanaume kufuga ndevu,ingawa ni bora kufuata sunna ya Mtume,binafsi nanyoa ndefu,sio agizo la lazima la dini
Kuhusu wanawake kwenda saluni,wanawake wanatakiwa kujipamba kwa ajili ya waume zao,wapendeze na wanoge,ila naona kuna namna labda hizo saluni zimeonekana ni sehemu ambazo kuna ajenda nyingine zinafanyika
Kuhusu wanawake kuongea kwenye redio au television,kwa mfano katika tv yapaswa mwanamke ajistiri anapokuwa hewani na si kuwa uchi kwa mujibu wa uislamu,kuhusu kuongea kwenye redio,hiyo hata huku Tanzania kuna redio moja Redio imani nayo kipindi fulani fulani walikataza lakini wakapewa hoja mbona wake za Mtume Muhammad (s.a.w) walikuwa wanaongea na wanaume nyuma ya pazia,kwahiyo hapo hoja nzito ilipatikana
Kwahiyo si kila linalo fanywa na hivi vikundi vyenye misimamo mikali ni uislamu bali mengine ni taratibu zao binafsi
Asante