Meneja Habari na Mawasiliano Simba Ahmed Ally Amekiri wachezaji wa Timu hiyo kudai bonasi.
" kweli wachezaji wanadai Bonasi zao za mechi kadhaa, Kuna wakati taasisi inakuwa na fedha inalipa madeni yote Kuna wakati haina fedha inalimbikiza madeni Mzigo ukipatikana watu wanalipwa"
Hivi hawa si ndio wale walikataa udhamini ili waweke nembo ya " Visit Tanzania"...?
Sasa watani mmeona jinsi siasa zinavyo wavua nguo? Haya timu haina pesa ya kulipa wachezajli Bonasi, mtatoa wapi pesa za kuwavunjia mikataba wachezaji hewa ambao wengi wao wamebakiza mwaka mmoja mmoja kwenye mikataba yao?
Pia mtapata wapi pesa za kusajili mmbadala wa wakina Onyango, Putin na Baleke?
Upi umuhimu sasa wa kuwapo kwa Mo Dewji (Rais wa. heshima) klabuni kwenu?
Mnakosaje tupesa tudogo tudogo twa kuwalipa wachezaji bonas zao.
Mechi ya Yanga mliwaahidi kuwalipa wachezaji mil 350 kama tu wakiwafunga Yanga SC. Mpaka sasa hivi Boss Mo ndo kagoma kaabisa kupokea simu.
Try Again na genge lake wako bize kwenye ofisi za Mbet wakiomba mkopo wa kumaliza maadeni ya Bonasi kwa Wachezaji. Wakati huo huo Mo anawaangalia tu, Ni tajiri gani huyo?
Anyway sioni wa humzuia Yanga SC kutwaa ubingwa msimu ujao wa 2023/24.