Afrika bado safari ni ndefu sana: Mtoto wa rais Museveni aamuru Kizza Besigye apewe dhamana.

Imeloa

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2013
Posts
17,999
Reaction score
21,560
Katika hali inayoonyesha kwamba mkuu wa majeshi nchini Uganda Jenerali Muhozi Kainerugaba ambaye pia ni mtoto wa rais wa nchi hiyo Bw. Yoweri Museveni, ndiye kwa sasa anaiongoza nchi ya Uganda, ameamua kumpatia dhamana kiongozi mkongwe wa upinzani wa Uganda Bw. Kizza Besigye.

Juhudi za kutafuta suluhu kuhusu hatima ya mwanasiasa huyo mkongwe wa upinzani nchini Uganda, Dkt. Kizza Besigye, zimechukua mwelekeo mpya baada ya Jenerali Salim Saleh kufichua kuwa ameanza kushughulikia suala hilo kufuatia ombi kutoka kwa Mkuu wa Majeshi (CDF), Jenerali Muhoozi Kainerugaba, huku matokeo yakitarajiwa kupatikana ndani ya miezi mitatu hadi sita ijayo. Saleh, ambaye ni mshauri mkuu wa Rais kuhusu masuala maalum na Mratibu Mkuu wa mpango wa 'Operation Wealth Creation', alisema kuwa amerejea kuwasiliana na Besigye baada ya miaka kadhaa ya kutokuwa na uhusiano wa karibu kutokana na tofauti zao za kisiasa.

Nchi zetu zina katiba za hivyo sana
 
Ijumaa Lissu atakua ulaiyani Wala usitie shaka Lissu sio mhaini Lissu Hana kesi
 
Ila wakuu, kifo ndo mchongo pekee lazima utik kwa kila mtu.

Ruka ruka weeeeee ila Bw kifo akikufikia, hutomeza hata mate, unavuta.
 
Kama sijaelewa vile, hiyo dhamana ndio itachukua miezi mitatu mpaka sita kutolewa?!
 
Uganda na Tanzania zinafanana sana hii ni kwa sababu Kikwete na Samia wamemuiga Museveni anavyoendesha nchi hadi jinsi ya kuwashughulikia wapinzani, waandamaaji, utekaji, kufungia vyombo vya habari, utesaji, wizi wa mali za umma. Serikali ya Tanzania imeizidi kwenye ulawiti, mauaji ya wenye nchi.

Museveni anamfunga Kizza Besigye, mtoto wake anasimamia utekaji, utesaji wake baadaye anamuomba baba yake mdogo, tajiri namba moja Uganda, mdogo wake Museveni Salim Saleh amwachie. Tanzania iko chini ya familia mbili, tatu za Kikwete, Samia, Rostam.

Wengine wote hata Makamu wa Rais, Waziri mkuu, mkuu wa majeshi wanaweza kufanywa chochote.
 
Hiyo kesi ni masuala ya kifamilia zaidi

Dr Besigye alikuwa daktari wa Museveni wakati wa vita
Aliwahi kumtibu Maj Gen Salim Saleh wakati alipojeruhiwa vitani
Maj Gen Saleh kwa jina la asili Caleb Akwendanaho ni mdogo wake wa mwisho Yoweri Museveni

Mke wa Dk Besigye, Engineer Winnie aliwahi kuwa girlfriend wa Museveni kabla ya kuolewa na Dr Besigye baada ya baba yake Winnie kumkataa Museveni akimuona hana muelekeo katika maisha akiwa anapenda sana kushiriki vita
Museveni kwa historia yake akiwa UD kipindi cha likizo alikuwa anasafiri kwenda nchi zenye migogoro hasa Mozambique, Angola na North Korea kupata uzoefu vitani

Juzi Gen Saleh alipoenda kumuona Dr Besigye kamkuta hali mbaya akaamua kumchukua kumpeleka hospitali jambo ambalo Gen Muhoozi hawezi kumzuia

Gen Muhoozi kwa Uganda ukiacha baba yake, mtu pekee anayeweza kufanya au kusema jambo kinyume na amri yake na asimguse ni huyo baba yake mdogo Gen Saleh ambaye anasimamia mali zote za familia ya Museveni kwa sasa na inasemekana ndiyo mtu tajiri kuliko wote Uganda
 
Marais wengi wa kiafrika ni wezi tu, sasa Museveni hiyo mali ameipatia wapi wakati hajulikani kufanya biashara yoyote.

Kama ilivyo desturi akitolewa madarakani wala hiyo mali haitakuwepo tena na ndivyo uzoefu unavyoonyesha, tumeona kwa madikteta wengi huko nyuma.
 
Katika hali inayoonyesha kwamba mkuu wa majeshi nchini Uganda Jenerali Muhozi Kainerugaba ambaye pia ni mtoto wa rais wa nchi hiyo Bw. Yoweri Museveni, ndiye kwa sasa anaiongoza nchi ya Uganda, ameamua kumpatia dhamana kiongozi mkongwe wa upinzani wa Uganda Bw. Kizza Besigye.

Juhudi za kutafuta suluhu kuhusu hatima ya mwanasiasa huyo mkongwe wa upinzani nchini Uganda, Dkt. Kizza Besigye, zimechukua mwelekeo mpya baada ya Jenerali Salim Saleh kufichua kuwa ameanza kushughulikia suala hilo kufuatia ombi kutoka kwa Mkuu wa Majeshi (CDF), Jenerali Muhoozi Kainerugaba, huku matokeo yakitarajiwa kupatikana ndani ya miezi mitatu hadi sita ijayo. Saleh, ambaye ni mshauri mkuu wa Rais kuhusu masuala maalum na Mratibu Mkuu wa mpango wa 'Operation Wealth Creation', alisema kuwa amerejea kuwasiliana na Besigye baada ya miaka kadhaa ya kutokuwa na uhusiano wa karibu kutokana na tofauti zao za kisiasa.

Gen. Muhoozi is the de facto ruler of the Republic of Uganda. Hilo ni muhimu kulielewa.
 
Back
Top Bottom