Nchi zetu zina katiba za hivyo sanaKatika hali inayoonyesha kwamba mkuu wa majeshi nchini Uganda Jenerali Muhozi Kainerugaba ambaye pia ni mtoto wa rais wa nchi hiyo Bw. Yoweri Museveni, ndiye kwa sasa anaiongoza nchi ya Uganda, ameamua kumpatia dhamana kiongozi mkongwe wa upinzani wa Uganda Bw. Kizza Besigye.
Juhudi za kutafuta suluhu kuhusu hatima ya mwanasiasa huyo mkongwe wa upinzani nchini Uganda, Dkt. Kizza Besigye, zimechukua mwelekeo mpya baada ya Jenerali Salim Saleh kufichua kuwa ameanza kushughulikia suala hilo kufuatia ombi kutoka kwa Mkuu wa Majeshi (CDF), Jenerali Muhoozi Kainerugaba, huku matokeo yakitarajiwa kupatikana ndani ya miezi mitatu hadi sita ijayo. Saleh, ambaye ni mshauri mkuu wa Rais kuhusu masuala maalum na Mratibu Mkuu wa mpango wa 'Operation Wealth Creation', alisema kuwa amerejea kuwasiliana na Besigye baada ya miaka kadhaa ya kutokuwa na uhusiano wa karibu kutokana na tofauti zao za kisiasa.
Kitendo cha wakili kukataa fungu alilompa wenje kumpatia kilimuudhi sana dullieHuku tunasubiri dulie nae aseme jambo!
Marais wengi wa kiafrika ni wezi tu, sasa Museveni hiyo mali ameipatia wapi wakati hajulikani kufanya biashara yoyote.Hiyo kesi ni masuala ya kifamilia zaidi
Dr Besigye alikuwa daktari wa Museveni wakati wa vita
Aliwahi kumtibu Maj Gen Salim Saleh wakati alipojeruhiwa vitani
Maj Gen Saleh kwa jina la asili Caleb Akwendanaho ni mdogo wake wa mwisho Yoweri Museveni
Mke wa Dk Besigye, Engineer Winnie aliwahi kuwa girlfriend wa Museveni kabla ya kuolewa na Dr Besigye baada ya baba yake Winnie kumkataa Museveni akimuona hana muelekeo katika maisha akiwa anapenda sana kushiriki vita
Museveni kwa historia yake akiwa UD kipindi cha likizo alikuwa anasafiri kwenda nchi zenye migogoro hasa Mozambique, Angola na North Korea kupata uzoefu vitani
Juzi Gen Saleh alipoenda kumuona Dr Besigye kamkuta hali mbaya akaamua kumchukua kumpeleka hospitali jambo ambalo Gen Muhoozi hawezi kumzuia
Gen Muhoozi kwa Uganda ukiacha baba yake, mtu pekee anayeweza kufanya au kusema jambo kinyume na amri yake na asimguse ni huyo baba yake mdogo Gen Saleh ambaye anasimamia mali zote za familia ya Museveni kwa sasa na inasemekana ndiyo mtu tajiri kuliko wote Uganda
Gen. Muhoozi is the de facto ruler of the Republic of Uganda. Hilo ni muhimu kulielewa.Katika hali inayoonyesha kwamba mkuu wa majeshi nchini Uganda Jenerali Muhozi Kainerugaba ambaye pia ni mtoto wa rais wa nchi hiyo Bw. Yoweri Museveni, ndiye kwa sasa anaiongoza nchi ya Uganda, ameamua kumpatia dhamana kiongozi mkongwe wa upinzani wa Uganda Bw. Kizza Besigye.