Afrika Kusini sio salama, kuna Watanzania wameuawa siku za karibuni

Afrika Kusini sio salama, kuna Watanzania wameuawa siku za karibuni

Teko Modise

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2017
Posts
2,331
Reaction score
7,733
Ndugu zetu, kama maisha ni magumu bora upambane ukiwa hapa na usifikirie kwenda Bondeni, Southa Africa.

Kuna jamaa, amepost kwenye ukurasa wake wa kijamii Watanzania wenzetu kadhaa waliopoteza maisha huko South kwa kuuawa.

Sijajua walikuwa wanajishghulisha na kazi gani hawa ndugu zetu, lakini kwa kifupi itoshe kusema South Africa hakufai hata kidogo.

FA960DBB-375D-4802-B98F-542FC6F78EFA.jpeg
 
Kuwa salama au kutokua salama kunategemea na mazingira ya shughuli zako. Hao wote ni kazi chafu.

Mimi nina mbwa nilimpeleka huko namuita mbwa kwa sababu kafanikiwa na amepata uraia, na maisha yamenyooka, lakini mbwa yule kasahau fadhila nilipokwama nikahitaji msaada wake.
 
Mtoa hoja, usiitoe hoja kwa upande mmoja,be fair na sio kuwa ni watanzania pekee wanaouliwa na wazawa hapo SA, wazimbabwe na wapopo wengi tu wamepoteza maisha, watanzania sio kwamba ndio wanajihusisha na biashara haramu, wengi wana maisha yao ya kihalali kama huyu aliyeuawa na police joberg, na ninaamini mpaka umetoa picha zao humu hawa wote wanafamilia wana taarifa za misiba hii,usitishe watu na ifanyie heshima avatar yako, mchezaji huyu aliyechukua Jina lake alikuwa respected hadi leo anaheshima sana,guy's maisha popote kuna watanzania wapo Columbia sembuse hapo Durban
 
Kuna dogo mmoja nilikutana nae miaka ya nyuma nikamhoji akasema anatokea magomeni, sasa ilikua lusaka hapo kweli anapass ya kitabu lakini ndio anasafiri kwa kuungaunga hata hajielewi, tunavuka chirundu keshaishiwa kila kitu ikabidi nianze kusimamia show za misosi, kumuhoji sana alisema anaenda Durban mimi nilikua naishia harare, tukafika bus terminal Roadport ya zimbabwe nikaongea nae sana akasema anaenda kuuza madawa wenzake wamemwita, na nauli hana na simu za anaowafuata south hazipatikani ikabidi tumchangie nauli japo apande roli asogee hata mesina mimi na jamaa wa Mabasi ya taqwa alikua zimbabwe jina lake anaitwa S , sasa nikajisemea huyu kajipanga naenda kufanya issue za kihalifu, sikuwahi tena kujua yuko wapi maana ni miaka mingi sana imepita,
 
Back
Top Bottom