Kuna dogo mmoja nilikutana nae miaka ya nyuma nikamhoji akasema anatokea magomeni, sasa ilikua lusaka hapo kweli anapass ya kitabu lakini ndio anasafiri kwa kuungaunga hata hajielewi, tunavuka chirundu keshaishiwa kila kitu ikabidi nianze kusimamia show za misosi, kumuhoji sana alisema anaenda Durban mimi nilikua naishia harare, tukafika bus terminal Roadport ya zimbabwe nikaongea nae sana akasema anaenda kuuza madawa wenzake wamemwita, na nauli hana na simu za anaowafuata south hazipatikani ikabidi tumchangie nauli japo apande roli asogee hata mesina mimi na jamaa wa Mabasi ya taqwa alikua zimbabwe jina lake anaitwa S , sasa nikajisemea huyu kajipanga naenda kufanya issue za kihalifu, sikuwahi tena kujua yuko wapi maana ni miaka mingi sana imepita,