Ndio mrundi alianza kutoka nje na ndani ya afrika kitambo hiyo america kwao sio issue. Europe huwakosi nchi yoyote then wanyarwanda nao kitambo wanasafiri tena kihalali halafu wanaitana kwenye dili za kueleweka, wabongo uoga na maisha marahisi yalitulemaza sana hata wanaotoka wengi hawakujua waanzie wapi, juzi nimeona mtu anazingumzia mtumba mnazi mmoja nikakumbuka miaka ya mtumba wa magendo unatoka burundi kurudi bongo, yaani michoro wengine waliipata kitambo, kama wazimbabwe zamani walifuata bidhaa Zanzibar enzi south yupo mkaburu, mrundi aliingia nairobi anachukua oil za magari anapeleka kuuza harare hadi bulawayo, kwahiyo sisi tukaingia kichwakichwa na kurithishana dili za magumashi mtu akienda bondeni akirudi na raba na jinzi basi unatamani na wewe kumbe jamaa mwenyewe ni mwizi tu hiyo mbaya sana