Afrika Kusini waanza kupitishia mizigo yao yakiwemo magari katika bandari ya Dar es Salaam

Afrika Kusini waanza kupitishia mizigo yao yakiwemo magari katika bandari ya Dar es Salaam

Fuatilia habari kwa umakini angalia ulivyoandika kwa haraka!
Hiyo mizigo inatoka nje unapita Dar alafu ndo inaenda huko kusini mwa Africa au
inatoka huko kusinj mwa Africa inakuja kwetu
Au inatoka kusini mwa Africa inapita kwetu alafu inaenda mbele zaidi

Maelezo yaliyonyooka tafadhari.
 
Nchi ya Afrika Kusini imeanza kupitishia mizigo yake katika bandari ya Dar es salaam baada ya ufanisi kuongezeka bandarini hapo.

Msemaji wa TPA amesema jambo kama hili zamani lisingewezekana lakini sasa shughuli za kutoa mzigo bandarini hazichukui zaidi ya siku tatu jambo lililowavutia sana wafanyabiashara wa South Africa

Source ITV habari
Durban?
Port Elizabeth?
Port Sherpstone?
Port Alfred?
 
Siku tatu? Kwani ile meli ya mafuta ya kula imekaa muda gani pale hadi bei zimepanda.

Kuna gharama [demurrage charges] kwa mizigo kukaa sana bandarini kabla ya kuchukumiwa na wenyewe. Gharama hizi huongeza bei za Bidhaa.
 
Wewe Bavicha kinakushangaza nini hapo?

Kwani wafanyabiashara wa Tanzania hawatumii bandari ya Mombasa?
Wanaopinga ujinga wa CCM siyo wote ni wapinzani hata CCM napo kuna wapinzani wa ndani kwa ndani wasiopenda ujinga na wao hutumia hili jukwaani kukataa uzushi wa CCM yao inayotumia zidumu fikra za mwenyekiti wa CCM pasipo kutumia Akili zao binafsi
 
Nchi ya Afrika Kusini imeanza kupitishia mizigo yake katika bandari ya Dar es salaam baada ya ufanisi kuongezeka bandarini hapo.

Msemaji wa TPA amesema jambo kama hili zamani lisingewezekana lakini sasa shughuli za kutoa mzigo bandarini hazichukui zaidi ya siku tatu jambo lililowavutia sana wafanyabiashara wa South Africa

Source ITV habari
Hii taarifa haijakaa sawa,SA ina Bandari kubwa tu,kwenye bahari ya hindi,na atrantic sasa wanapitisha mizigo Dar kutokea wapi?au kwenda wapi?Kama mzigo unatoka SA kwenda Burundi au Rwanda,unaweza ukaja kwa njia ya bahari mpaka Dar,then kutoka Dar unasafirishwa kwa njia kavu,
 
Wanazo Bandari kubwa nne Darban, Capetown, East London na port Elizabeth na pia zipo Bandari nyinginezo kibao huko South Africa ndiyo maana inashangaza kupitisha mizigo yao Tanzania
Inashangaza Sana
 
Back
Top Bottom