Afrika Kusini wasijaribu kutaka kuzichapa na Rwanda. Watachakazwa vibaya sana

Afrika Kusini wasijaribu kutaka kuzichapa na Rwanda. Watachakazwa vibaya sana

Kagame ana watu huko SA. AMBAYO NI KAMA STATE ILIYO FAIL. NIMEKAA MIAKA 3 SA. naifahamu. Kagame alishaingia SA. AKAUA MTU ALIYETAKA NA AKAONDOKA BILA SHIDA. ANAIJUA SA. Wewe hujui kitu.

Nimefanya kazi mataifa makubwa 7 hapa Afrika na matatu madogo ikiwemo Rwanda. Naelewa. Kwa sasa nipo MAREKANI mwaka wa ...... Huu. Kagame nafahamu kwa nini anadindisha kwa Sa. Sasa wewe sema ni kahawa. Wala sikukatazi.
Rwanda inazakisha siraha gani?
 
South Africa akiamu kutumia ndege hata 50 hiyo Rwanda itakuwa wapi?

Kuna vitu mjaribu kuvifikiria!
Ndo maana anapigana proxy war ..utamvamia Rwanda kwa lipi we kama unamtaka nenda kapambane na M23,,jamaa anatumia vizuri strategy za mabeberu wakina USA na UK ,hawapigani vita nchini kwao ila kwenye maslahi yao ndo wanapopeleka vita
 
1000019674.jpg
 
Ujumbe mzito

Ujumbe Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Afrika ya Kusini - SANDF kuhusu mzozo wa DRC

View: https://m.youtube.com/watch?v=bLVHHfupmJA

General Rudzani Maphwanya
Mkuu wa SANDF.

Jenerali Rudzani Maphwanya alizaliwa tarehe 23 Novemba 1960 katika Mkoa wa Limpopo, Afrika Kusini. Alimaliza shule yake ya sekondari katika Shule ya sekondari ya Mphaphuli huko Limpopo mnamo 1978 na muda mfupi baadaye alijiunga na Umkhonto we Sizwe (MK), tawi la kijeshi la chama cha ukombozi cha African National Congress- ANC.

Kazi ya kijeshi ya Maphwanya ya MK ilianza mwaka 1978 hadi 1994 ambapo alikuwa amepata mafunzo katika taasisi mbalimbali za bara la Afrika na nje ya nchi.

Jenerali Maphwanya alijumuishwa rasmi katika Jeshi la Ulinzi la Kitaifa la Afrika Kusini mwaka wa 1994.

Aidha, alimaliza Kozi zake za kijeshi ngazi za junior command na staff Command katika Chuo cha Staff College cha Zimbabwe mwaka 1993.

Aliendeleza mafunzo yake ya kijeshi kwa kumaliza safu ya kozi za kukuza na kukuza.

Maphwanya alimaliza Kozi yake ya Senior Command na senior staff katika Chuo cha Staff College cha Kenya mwaka wa 2000.

Kozi ya mwisho ya kijeshi ambayo Maphwanya alimaliza ilikuwa ni Programu ya Kitaifa ya Usalama wa Taifa mwaka wa 2004

Maphwanya alishika nyadhifa mbalimbali katika Jeshi la Ulinzi la Taifa la Afrika Kusini SANDFkuanzia mwaka 1994 hadi sasa.

Alipewa kazi katika Kampani ya A katika Kikosi cha 1 cha infantry cha battalion ya Jeshi la Afrika Kusini baada ya kuhitimu Mafunzo ya Madaraja 1995 na baadaye kuhamishiwa Makao Makuu ya Kamandi ya Far North huko Musina ambapo alihudumu kama Kamanda wa Kampani katika kipindi cha 1995 hadi 1996.

Zaidi ya hayo, alihudumu kama Staff Officer Daraja la 2 Uendeshaji, Ufuatiliaji na Tathmini na Mafunzo katika taasisi hiyo hiyo katika kipindi cha 1997 hadi 1999.

Mwaka 1999 Maphwanya alihamishiwa Brigedia ya Kikosi Maalum cha Afrika Kusini ambako aliteuliwa kuwa staff officer Daraja la 1 wa Operesheni, Ufuatiliaji na Tathmini hadi 2001.

Mwaka 2002 hadi 2003 aliteuliwa kuwa Afisa Mwandamizi Senior Staff Officer wa Ufuatiliaji na Tathmini na muda mfupi baadaye Mkuu wa Wafanyakazi wa Kikosi Maalum (South African Special Forces Brigade) cha Afrika Kusini katika kipindi cha 2003 hadi 2005.

Akiwa katika nafasi ya Mkuu wa Majeshi, alihudhuria na kukamilisha Programu ya Usalama ya Taifa katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi cha Afrika Kusini mwaka wa 2004.

Aliteuliwa kuwa Afisa Mkuu wa Vikosi Maalum vya Afrika Kusini mwaka wa 2006 na alihudumu katika nafasi hiyo hadi 2016. alipoteuliwa na kupandishwa cheo na kuwa Meja Jenerali kama Afisa Mkuu Mnadhimu wa Jeshi la Wanajeshi la Afrika Kusini.

Mnamo Novemba 2019, Maphwanya aliteuliwa kuwa Mkuu wa Operesheni za Pamoja na baadaye kupandishwa cheo hadi Luteni Jenerali.

Kufuatia uteuzi wa wajumbe wapya wa Kamandi ya Kijeshi (joint chief of staffs) kama ilivyotangazwa na Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Rais Ramaphosa baada ya kustaafu kwa baadhi ya Maafisa Wakuu wa SANDF, Maphwanya anateuliwa kuwa Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Taifa la Afrika Kusini kuanzia kuanzia tarehe 1 Juni 2021 na kupandishwa cheo hadi kuwa Jenerali.

Luteni Jenerali Maphwanya alipata Shahada ya Kwanza ya Biashara mwaka 1994 katika Chuo Kikuu cha Kaskazini na Cheti cha Usimamizi wa Ubora wa Jumla mwaka 2003 katika Chuo Kikuu cha Afrika Kusini (UNISA). Mnamo 2005 pia alikamilisha Mpango wa Usimamizi wa Mkakati katika Chuo Kikuu cha Pretoria; alihitimu Stashahada ya Uzamili ya Usimamizi wa Usalama katika Chuo Kikuu cha Witwatersrand (WITS) mwaka 2012 na baadaye kuhitimu Shahada ya Uzamili ya Usimamizi katika Chuo Kikuu cha Witwatersrand (WITS) mnamo 2015.

Maphwanya ameoa mke Bi. Masindi Mulayo Maphwanya na ana mtoto wa kiume na wa kike.
 
Kagame ana watu huko SA. AMBAYO NI KAMA STATE ILIYO FAIL. NIMEKAA MIAKA 3 SA. naifahamu. Kagame alishaingia SA. AKAUA MTU ALIYETAKA NA AKAONDOKA BILA SHIDA. ANAIJUA SA. Wewe hujui kitu.

Nimefanya kazi mataifa makubwa 7 hapa Afrika na matatu madogo ikiwemo Rwanda. Naelewa. Kwa sasa nipo MAREKANI mwaka wa ...... Huu. Kagame nafahamu kwa nini anadindisha kwa Sa. Sasa wewe sema ni kahawa. Wala sikukatazi.
Unaongelea vitu kirahisi sanaa kama layman vita ni zaidi ya wanajeshi wanao ishi mstuni, Vita ni uchumi mkuu, Rwanda huwezi kuiweka sawa na SA hata kama imepenyeza watu wake ndani SA, wanao winda SA sio Rwanda huyu anatumika tu kama Zelezkky alivyo tumika na atachwa avetually kama tunavo elekea, wewe kama unajua siasa za kimataifa jiulize anae tafuta SA kupitia Rwanda ni nani?
 
Majeshi yenye nguvu Afrika
Tz ya 15 na SA ni ya 4
Kwenye nchi 145 duniani SA ni ya 40
Na hizi nchi mbili zitachapania wapi?
Au uwanja wa mapigano ni DRC?
Mara nyingi hizo rank zinaangaliaga bajet, mavifaa yako na mazaga mengine,,,ila vita ya msituni usiombee ukutane na wataalam na hilo eneo wao ndo wawe wenyeji...Mmarekani alipambana na Vietnam na ubabe wake wote ila ikafika mahali ikabidi aondoke tu sio kwamba alishindwa, ila ile kitu unajua umemaliza adui kumbe bado inatesa sana hadi unaamua mwenyewe unasepa, ndo kama M23 wakipatikana wanachapika unajua umemaliza kumbe wanarudi kujipanga wakikaa sawa wanarudi tena , kumaliza hizo vita ni ngumu hadi watu waamue kukubaliana kuyajenga................modern warfare imebase sana kwenye miji na jangwani bado hatujaona mapambano makubwa ya kivita msituni,,,,ndo maana unaweza ukawa na mavifaa ya kutosha ukienda kichwakichwa unakalishwa
 
Ndo maana anapigana proxy war ..utamvamia Rwanda kwa lipi we kama unamtaka nenda kapambane na M23,,jamaa anatumia vizuri strategy za mabeberu wakina USA na UK ,hawapigani vita nchini kwao ila kwenye maslahi yao ndo wanapopeleka vita
Kule huwa haipiganwi vita bali ni kulinda amani na kuweka mambo sawa.

Aliyekuwa kwenye vita ni Rwanda na M23. Ndiyo maana wanatumia kila silaha kwa ukubwa.

Wenzao wapo kwenye military operation.

Uliza kipindi cha Kabila pale Rwanda na Uganda ilipoivamia Congo na majeshi ya Afrika yalivyoingia kwa Full scale war huyo Rwanda aliishia wapi? Alipoteana yeye na Uganda.
 
Mara nyingi hizo rank zinaangaliaga bajet, mavifaa yako na mazaga mengine,,,ila vita ya msituni usiombee ukutane na wataalam na hilo eneo wao ndo wawe wenyeji...Mmarekani alipambana na Vietnam na ubabe wake wote ila ikafika mahali ikabidi aondoke tu sio kwamba alishindwa, ila ile kitu unajua umemaliza adui kumbe bado inatesa sana hadi unaamua mwenyewe unasepa, ndo kama M23 wakipatikana wanachapika unajua umemaliza kumbe wanarudi kujipanga wakikaa sawa wanarudi tena , kumaliza hizo vita ni ngumu hadi watu waamue kukubaliana kuyajenga................modern warfare imebase sana kwenye miji na jangwani bado hatujaona mapambano makubwa ya kivita msituni,,,,ndo maana unaweza ukawa na mavifaa ya kutosha ukienda kichwakichwa unakalishwa
KAbisa. Ndo wanachojivunia M23. Wame imaster Congo porini huko. Ni kugumu sana. Na ndo kilimshinda Usa huko Vietnam. Ni vita ngumu sana na inataka wenyeji.
 
Mara nyingi hizo rank zinaangaliaga bajet, mavifaa yako na mazaga mengine,,,ila vita ya msituni usiombee ukutane na wataalam na hilo eneo wao ndo wawe wenyeji...Mmarekani alipambana na Vietnam na ubabe wake wote ila ikafika mahali ikabidi aondoke tu sio kwamba alishindwa, ila ile kitu unajua umemaliza adui kumbe bado inatesa sana hadi unaamua mwenyewe unasepa, ndo kama M23 wakipatikana wanachapika unajua umemaliza kumbe wanarudi kujipanga wakikaa sawa wanarudi tena , kumaliza hizo vita ni ngumu hadi watu waamue kukubaliana kuyajenga................modern warfare imebase sana kwenye miji na jangwani bado hatujaona mapambano makubwa ya kivita msituni,,,,ndo maana unaweza ukawa na mavifaa ya kutosha ukienda kichwakichwa unakalishwa
Hivi nyinyi mnajua vita au mnajiandikia andikia tu?

Wewe unajua hata hiyo vita ya kisasa msituni inapigwanaje?

Au nikikuuliza hiyo vita hata hiyo unayoisema unajua inapiganajwe?
 
Kagame anajiamini anajua anachofanya. Kumwambia SA kuwa "ukitaka kupigana njoo...... " Anajua kuwa SA. hawana jeshi lenye nidhamu na pia hawaifahamu Congo na Misitu yake. Huwezi pigana na Kagame katika misitu ya Congo atakuchapa. Anaifahamu vizuri.

Labda sasa mpigane kwa kurushiana mabomu tu juu kwa juu. Lakini mimi nimefanya kazi na jesh la SA. wa hovyo sana wale jamaa hawana nidhamu kabisa. Watu wa starehe kinyama. Piga sana pombe na mademu. Halafu hawataki shida.

Tofauti na M23 na Kagame.hawa jamaa ni wabishi sana. Nimeona kazi zao hasa huko maporini. SADC na MONUSCO wanapata kipigo sometimes hawaelewi wafanye nini. Wanachoka. Hali ni mbaya kwao.

Ramaphosa ni mmoja ya Maraisi Bwege sana. Ni kama tutusa tu. Ndo maana Kagame hamwogopi. Na hana uungwaji mkono mkubwa huko SA. Basi tu wananchi wa SA ndo wale wale wanaumizwa na ukabila.

Soma pia:
Usimpoze mti mkavu akadandia mtumbwi wa vibwengo.. achezee kichapo hadi achakae
 
Mara nyingi hizo rank zinaangaliaga bajet, mavifaa yako na mazaga mengine,,,ila vita ya msituni usiombee ukutane na wataalam na hilo eneo wao ndo wawe wenyeji...Mmarekani alipambana na Vietnam na ubabe wake wote ila ikafika mahali ikabidi aondoke tu sio kwamba alishindwa, ila ile kitu unajua umemaliza adui kumbe bado inatesa sana hadi unaamua mwenyewe unasepa, ndo kama M23 wakipatikana wanachapika unajua umemaliza kumbe wanarudi kujipanga wakikaa sawa wanarudi tena , kumaliza hizo vita ni ngumu hadi watu waamue kukubaliana kuyajenga................modern warfare imebase sana kwenye miji na jangwani bado hatujaona mapambano makubwa ya kivita msituni,,,,ndo maana unaweza ukawa na mavifaa ya kutosha ukienda kichwakichwa unakalishwa
Ni kweli unachosema ila kwenye vita ya miguu kukwama ni lazima kama utamfuata adui kwake na mahali ambapo anapajua zaidi
Ni kama mtu aingie kwako

Hata US huko Iraq walishinda kwa ndege za kivita
Kama unampiga adui kutoka angani sawa ila kwa ardhi ni ngumu labda uwe na mapandikizi kwa miaka mingi
 
Labda sasa mpigane kwa kurushiana mabomu tu juu kwa juu.
Mbona unaweka labda tena? Nilikuwa nakushangaa unatajataja misitu, kumbe mawazo yako yalifungwa na vita ya ardhini. Vitani huwezi ukampangia adui yako namna ya kupigana, ukisema unaweza kupigana basi jiandae kwa lolote, usilete zile za watoto wa enzi zetu kwamba mnapocheza mechi, kama nyie hamna viatu basi mnawalazimisha na wapinzani wenu wavue viatu ili mcheze kwa usawa 😂
 
Back
Top Bottom