Afrika tunashindwa na nchi za Asia tulizopata uhuru muda sawa. Shida ni nini?

Very weak argument, nasema very weak kwa sababu Tanzania rasilimali zipo, wananchi wengi tunaleta janja janja kwenye elimu, na viongozi wao ndo wameshika mpini kabisa kutudidimiza.( Na bado tumewashikiliantu)
Rasilimali zipi? Tanzania Haina rasilimali za maana acheni kujidanganya.
 
Tatizo la hawa jamaa ni corrupt. Scandinavian countries is the best.
Scandinavian zimefanikiwa lakini mifumo yao maisha haipishani sana na west Europe individualism ndio imetawala katika maisha yao jambo ambalo kwetu halipo kabisa.

Hao East Asians kidogo tuna shabihiana kwenye mfumo wa maisha hasa kwenye collectivism.

Maisha yetu tulipo hapa tuna hitaji kupelekwa kwa kasi, kwa lazima na kwa roho ngumu haswa jambo ambalo hao watu East Asia hivyo vitu wanaweza.

Corruption inabidi ikabiliwe na sheria kali Lee Kuan Yew alizungumza hili kuhusu Singapore yake akasema when you are in Singapore obey the laws hii ndio sheria ya kuwa salama Singapore.
 
Tuna changamoto nyingi sana ambazo inabidi tuzitatue ambazo zinatuathiri na kuonekana hatuja kamilika

Kiukweli kuwa Muafrika na kuukubali uafrika ni suala gumu sana kwa mtu anaye jitambua
Ndio maana waafrika wengi wanapambana kulikimbia kabisa hili bara.

West Africans na North Africans kila mara hujaribu kuvuka bahari ya mediterranean wakijaribu kuingia Ulaya. Licha ya wengi kufa maji, lakini hawa achi kujaribu bahati yao ya kuvuka bahari.

Vijana wengi wa Afrika, hupambana kwenda kusoma bachelor degrees, Masters na PhD kwenye vyuo vya Ulaya, America na Asia waki target kubakia huko huko kufanya kazi na kuishi, ila si kurudi Afrika.

Wachezaji wa mpira kutoka Afrika, wakifika ulaya hubadilisha kabisa uraia wao na kuomba uraia wa nchi za Ulaya. Mfano mzuri ni timu ya taifa ya Ufaransa.wachezaji wengi ni kutoka Afrika.

Mpaka hapa unaona kwamba kuwa Mwafrika na kuishi Afrika ni ngumu sana, kutokana na mifumo mibovu iliyopo.
 
Hata kwao, hata Europe na USA Kuna corruption kubwa sana.
Ni nchi gani isiyo na corruption ?hakuna mahali niliposema hakuna corruption hizo nchi ila nimezungumzia viwango.

Kiasili binadamu ni muovu no way unaweza kosa corruption na aina yoyote ya uovu nchi yoyote duniani ila unaweza kupunguza kiwango cha corruption katika eneo husika
 
Ndio maana waafrika wengi wanapambana kulikimbia kabisa hili bara.

West Africans na North Africans kila mara hujaribu kuvuka bahari ya mediterranean wakijaribu kuingia Ulaya. Licha ya wengi kufa maji, lakini hawa achi kujaribu bahati yao ya kuvuka bahari.

Vijana wengi wa Afrika, hupambana kwenda kusoma bachelor degrees, Masters na PhD kwenye vyuo vya Ulaya, America na Asia waki target kubakia huko huko kufanya kazi na kuishi, ila si kurudi Afrika.

Wachezaji wa mpira kutoka Afrika, wakifika ulaya hubadilisha kabisa uraia wao na kuomba uraia wa nchi za Ulaya. Mfano mzuri ni timu ya taifa ya Ufaransa.wachezaji wengi ni kutoka Afrika.

Mpaka hapa unaona kwamba kuwa Mwafrika na kuishi Afrika ni ngumu sana, kutokana na mifumo mibovu iliyopo.
Pamoja ya kwamba wanaikimbia Afrika ila hawaikimbii asili yao upuuzi wao wanaubeba kutoka Afrika na kuupeleka huko ng'ambo. Nigerians mpaka kuingia Saudia wamezuiliwa kwa sababu ya upuuzi wao.
 
Tuna changamoto nyingi sana ambazo inabidi tuzitatue ambazo zinatuathiri na kuonekana hatuja kamilika

Kiukweli kuwa Muafrika na kuukubali uafrika ni suala gumu sana kwa mtu anaye jitambua
Nili angalia habari ya hawa Wa Nigeria waliozamia meli kwenda kutafuta maisha ulaya, Waka okolewa na mapolisi wa Brazil

Nika gundua kwamba kweli watu wamechoshwa na hili bara la Afrika, to the point of being ready to die, wakitafuta njia ya kwenda ughaibuni.

Mmoja wapo wa wahamiaji hawa alipo hojiwa na wana habari Alisema kwamba, mapolisi walivyo mwambia kwamba wapo Brazil, alifurahi sana na kushukuru sana, Angalau amefika Brazil.

Walipewa chakula na maji, waka endelea na hatua za kuomba makazi.
FB_IMG_1691410052640.jpg
 
Pamoja ya kwamba wanaikimbia Afrika ila hawaikimbii asili yao upuuzi wao wanaubeba kutoka Afrika na kuupeleka huko ng'ambo. Nigerians mpaka kuingia Saudia wamezuiliwa kwa sababu ya upuuzi wao.
Ndiyo maana Mwafrika akifika ughaibuni anakutana na vigezo vingi sana vya kuthibitisha uaminifu wake,

Pia kuna kuwa na sheria kali sana za ku monitor mienendo yetu, ili kudhibiti hizi janja janja zetu za kipuuzi.

Maana Worldwide wana tujua sisi tumejaa janja janja za kiwizi wizi.
 
Jamani tuongee serious, nchi Kama India, Singapore, Malaysia, Indonesia zimepata uhuru almost the same time na nchi za kiafrika. Cha ajabu wenzetu wameendelea Sana halafu sisi bado tuna umaskini wa kutupa.

Afrika jamani shida ni Nini?
Ufisadi
 
Kama nchi kuendelea ni vigumu saana. Lamsingi ni kutafuta maendeleo yako binafsi na familia yako.
True na hakuna Mwafrika anaeweza mletea maendeleo mwafrika mwenzake huu ndio ukweli pambana kivyako
 
Nili angalia habari ya hawa Wa Nigeria waliozamia meli kwenda kutafuta maisha ulaya, Waka okolewa na mapolisi wa Brazil

Nika gundua kwamba kweli watu wamechoshwa na hili bara la Afrika, to the point of being ready to die, wakitafuta njia ya kwenda ughaibuni.

Mmoja wapo wa wahamiaji hawa alipo hojiwa na wana habari Alisema kwamba, mapolisi walivyo mwambia kwamba wapo Brazil, alifurahi sana na kushukuru sana, Angalau amefika Brazil.

Walipewa chakula na maji, waka endelea na hatua za kuomba makazi.View attachment 2731615
Afrika kuna changamoto nyingi sana ambazo sisi wenyewe waafrika kwa mikono yetu tumezitengeneza.

Kuna member kwenye moja ya nyuzi zangu alisema ili uweza kuishi kwa furaha Afrika inabidi ukubali kuwa mjinga na hii ni kweli hakuna mwenye akili timamu ataishi kwa furaha Afrika
 
Ndiyo maana Mwafrika akifika ughaibuni anakutana na vigezo vingi sana vya kuthibitisha uaminifu wake,

Pia kuna kuwa na sheria kali sana za ku monitor mienendo yetu, ili kudhibiti hizi janja janja zetu za kipuuzi.

Maana Worldwide wana tujua sisi tumejaa janja janja za kiwizi wizi.
Kwa kweli ujanja janja wa kijinga sisi ndio tunaona ndio maisha wakati ni upuuzi tu
 
Africa viongozi wa sasa hawana uwezo wa akili kuongoza. Ni wazee wanaopeana madaraka ili kula mema ya nchi. Africa haina dira ya kujikomboa yenyewe. Hao wanaoitwa viongozi wanaona sifa kila siku kurudi kwa mabeberu kuomba misaada hadi ya neti za mmbu.

Kuna hawa wa kwetu hapa utakuta mtu kamteua yeye tena kesho anasimama kulialia jukwaani kusema aliyemteua hafanyi kazi. Usanii na ujinga mwingi.
 
Scandinavian zimefanikiwa lakini mifumo yao maisha haipishani sana na west Europe individualism ndio imetawala katika maisha yao jambo ambalo kwetu halipo kabisa.

Hao East Asians kidogo tuna shabihiana kwenye mfumo wa maisha hasa kwenye collectivism.

Maisha yetu tulipo hapa tuna hitaji kupelekwa kwa kasi, kwa lazima na kwa roho ngumu haswa jambo ambalo hao watu East Asia hivyo vitu wanaweza.

Corruption inabidi ikabiliwe na sheria kali Lee Kuan Yew alizungumza hili kuhusu Singapore yake akasema when you are in Singapore obey the laws hii ndio sheria ya kuwa salama Singapore.
Scandinavian na West Europe kuna individualism? Kwetu kuna collectivism? Kwenye mambo gani? Labda tumepishana kidogo. Mimi nasema sisi tuna ubinafsi, umimi. Ile mtu anataka apate yeye na hajali wengine. Kuhusu corruption: tatizo siyo sheria bali ni sheria zinamhusu nani na tunazitekelezeje! Kwa mfano Bongo viongozi na wenye fedha sheria za corruption haziwahusu. Hata ukiweka sheria kali ni kuwa wadogo tu ndiyo watauawa.
 
True na hakuna Mwafrika anaeweza mletea maendeleo mwafrika mwenzake huu ndio ukweli pambana kivyako
Yes. Watu wenye maisha mazuri hawajawahi kuona kuwa afrika ni tatizo instead wanatumia umasikini wetu Kama fursa
 
Majibu kimsingi ya swali kama hili yametolewa sana humu.

Wapo waliosema ni laana, wapo walio toa sababu mbalimbali za kitaalamu.

Kiukweli inaumiza sana na kuudhi ndiyo kama hivyo wengine wanachezea rasilimali za TAIFA kujali matumbo yao na kuumiza kundi kubwa.

Itoshe kwa kumalizia na ujumbe huu [emoji116]Nothing moreView attachment 2731228
Nothing more to add !!! That's a reality !!
 
Yes. Watu wenye maisha mazuri hawajawahi kuona kuwa afrika ni tatizo instead wanatumia umasikini wetu Kama fursa
Umasikini ni matokeo ya fikra zaidi na Sio mazingira.
Thus mgeni anakuja na akili Africa anaodoka na utajiri
 
Africa viongozi wa sasa hawana uwezo wa akili kuongoza. Ni wazee wanaopeana madaraka ili kula mema ya nchi. Africa haina dira ya kujikomboa yenyewe. Hao wanaoitwa viongozi wanaona sifa kila siku kurudi kwa mabeberu kuomba misaada hadi ya neti za mmbu.

Kuna hawa wa kwetu hapa utakuta mtu kamteua yeye tena kesho anasimama kulialia jukwaani kusema aliyemteua hafanyi kazi. Usanii na ujinga mwingi.
Hata wa zamani yaan wapigania Uhuru walipigania maslai Yao binafsi na Sio maslai ya waafrika wote thus hadi kesho hakuna familia ya mpigania uhuru inalia njaa wote ni walamba asali.
 
Back
Top Bottom