Laana, mkosi, gundu ni maneno yenye connotations za super natural forces.
Yani, unajiondolea responsibility wewe mwenyewe, unasingizia mkosi, gundu, nuksi.
Ni aina fulani ya kukwepa ukweli kwamba huyo anayesema ana laana ana matatizo fulani anayotakiwa kuyachunguza na kuyatatua, na kuishia kusema kuna tatizo lilitokea vizazi vingi limemfunga.
Hakuna laana, ila hizi fikra za laana zinaweza kutengeneza kitu kinaitwa "self fulfilling prophecy".
Yani ni hivi, hakuna laana, ila, ukiamini Waafrika wana laana, unaitengeneza hiyo laana kichwani kwako mwenyewe halafu kwa sababu umeiamini, matokeo ya imani hiyo yanakuwa sawasawa na hiyo laana unayoiamini iwe ipo.
Ni kama vile, mwanafunzi ana uwezo wa kusoma na kufanya vizuri, halafu anaamini ana laana, halafu, kwa kuamini ana laana, anakosa kuweka juhudi kwenye kusoma, halafu anafeli, halafu anasema mnaona nimefeli, nina laana mimi.
Hili la laana ni tatizo la kisaikolojia zaidi.